Sitta na Mwakyembe nao ni Mapacha ?

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Nimelazimika kulisema hili ili ndugu zangu tujaribu kuchanganua, leo nilikuwa napita maeneo ya chuo SUA kwa mbali nikaona poster kubwa ina bendera ya taifa ikanivutia sana na nikalazimika kuisogelea ili nisome tangazo, ilikuwa na picha mbili kubwa ya Sitta na Mwakyembe.

Tangazo linaeleza kuwa karibu Mzumbe kesho 25 June 2011 kutakuwa na mjadala wa kitaifa kuanzia saa 3. 00 asubuhi , mada ni changamoto kuelekea katika jumuiya ya Afrika Mashariki na Mwakyembe naye ana mada yake wala haiusiani na wizara yake.

Nikakumbuka kuwa ni wale wale walioendesha mjadala pale chuo cha MUCCOBs pale moshi, na nikaunganisha na lile la CCJ nako walikuwa pamoja na lingine walilomtendea stahiki yake EL walishirikiana vilevile, nani anaweza kujua kilicho nyuma ya hawa wawili ?
 
Ni kweli kabisa hawa jamaa wanashabihiana,so hawa ni mapacha wawili contrary to mapacha watatu
 
hakika wanadhihirisha wao ni mapacha wawili, ila hofu yangu ni kwamba sina uhakika kama mada zilizoandikwa pale ndizo kweli wanaenda kuzitoa ni na mpango nikipata muda niwafuatilie nijue kwa hakika ni kitu gani wanaenda kufanya
 
Back
Top Bottom