Sitta mzoefu wa kuvuruga Bunge?

Sitta sio malaika, ila anaweza kuwa mtu mwema japo kwa kipindi kifupi cha maisha yake. Ni yupi kiongozi aliye mwema? Mh! Majungu bwana! Mtu asitende chema, mnang'ang'ania historia. Mtu akiwa mdokozi utotoni, tumhalalishie sifa ya wizi?
 
John Malecela ambaye alikuwa Waziri Mkuu alilazimishwa kuachia nafasi yake na kuwa Waziri asiye na wizara maalum huku nafasi yake ikichukuliwa na Cleopa David Msuya, lakini cha ajabu Waziri wa Sheria na Katiba, Samuel Sitta ambaye kwa nafasi yake alitoa ushauri mbaya kwa serikali na hakujali chama, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na wala serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hakujiuzulu.

"Wakati akijiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa sekta husika (Nishati na Madini) walijiuzulu. Baadhi ya watu wanahoji kwa nini Sitta hakujiuzulu mwaka 1994 akaondoka na Malecela?" wamehoji watu hao.

Najibu hoja nyekundu lakini nianze kusema hivi, Mimi ningekuwa kundi la mafisadi ningewaambia wenzangu tubadili mbinu za mapambano maana kutumia magazeti ni mbinu iliyokwishagudnulika mwaka 2005. Huwezi kupigana vita yoyote kwa mbinu ileile ambayo adui yako kaishaijua.

Kwa nini Sitta hakujiuzulu uwaziri wa Sheria kuhusu G55 na suala la utanganyika? Kosa la magazeti ya mafisadi wanadhani watu hawasomi vitabu na hawana kumbukumbu.

Suala la Tanganyika na G55 lilimfanya Mwl. Nyerere aandike kitabu kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA. Ni kweli Nyerere aliiponda serikali na bunge kwa kukubali hoja ya Tanganyika na wale wabunge 55 (G55).

Lakini Nyerere alimsifia mtu mmoja tu ndani ya kitabu hicho naye ni Samwel Sitta, waziri wa sheria na katiba wakati huo. Kwa nini Nyerere alimsifia Samwel Sitta? Ninamnukuu Nyerere kwenye kitabu chake hapa chini kwenye aya ya kwanza alipoanza chapter ya USUGU WA VIONGOZI :

..."Jukumu la kueleza taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao, nilimtafutaNdugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki".

"Mapema nilikuwa nimeambiwa kwamba (Samwel Sitta) alikuwa ametamka bungeni kwamba hapo hoja ya kudai Selikali Tatu itakapoanza kujadiliwa, yeye ataipinga, maana jimbo lake la uchaguzi, Urambo, halikuwa limemtuma kwenda bungeni kudai Serikali ya Tanganyika. Wabunge wote wakweli wangeweza kusema hivyo hivyo. Hata Waziri Mkuu na katibu Mkuu wangeweza kusema hivyo hivyo. Wao ni wateuliwa na Rais, ambaye alikwisha kwenda bungeni siku chache tu zilizopita, na kupinga hoja ya Serikali Tatu. Katika kikao cha usiku wa jana yake nilikuwa nimewakumbusha hivyo viongozi wetu waheshimiwa".....Mwisho wa kunukuu.

Hivyo katika sakata zima la suala la Tanganyika Sitta anabaki kuwa waziri pekee aliyeonyesha msimamo huo ambao umetajwa na Nyerere.

Spika wa wakati huo Pius Msekwa hakusifiwa kwa msimamo ndani ya bunge au NEC. Msekwa alitajwa tu na Nyerere kwamba ndiye aliyetoboa mpango mzima wa bunge ambapo bunge lilijifanya limefunga hoja ya serkali tatu lakini kumbe kimyakimya na kijanja limeipitisha hoja hiyo kwa siri ambayo Msekwa aliitoboa kwenye vyombo vya habari. Ninamnukuu Nyerere tena hapa chini:

...Kwa sababu uamuzi wa kutaka Serikali ya Tanganyika ‘ndani ya muungano' ulifanywa na viongozi wetu kwa hila, na kupitishwa bungeni bila mjadala, sisi wengine hatukujua lililotokea. Baadaye tulifahamishwa kuwa huo ndiyo ulikuwa uamuzi wa ‘bunge zima" kutokana na kauli ya Pius Msekwa aliyekuwa msimamizi wa kikao cha Bunge kilichofikia uamuzi huo....Nadhani viongozi wetu walitaka kuendelea kuficha na kuuvuga vuga, lakini yeye akatoboa. Nasikia baadaye aliitwa akakemewa. Sijui kwa nini...".....Mwisho wa kunukuu.

Hivyo tunaona kuwa ushujaa wa Samwel Sitta hata Nyerere aliujua na aliuandika. Mwandishi wa makala hii hana kumbukumbu ya kitabu hiki kwa sababu full time anasubiri kuneemeshwa na mafisadi. Na kama hakununua kitabu hiki mwaka 1994 basi aende kwenye makumbusho pale Butiama kuna vitabu zaidi ya 8000 vya iliyokuwa library ya Baba wa Taifa Julius Nyerere.
 
Wadau mnaichukuliaje hii. Inaashiria nini katika miaka mitano ya Spika Sitta hadi sasa!

Sitta mzoefu wa kuvuruga Bunge

MWANDISHI WETU

Imebainika kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta ni mwanasiasa mzoefu wa kuvuruga Bunge.

Siri hiyo nyeti imebainika kufuatia matukio mbalimbali ambayo Spika huyo amewahi kuyafanya katika kipidi chake cha uongozi wa kisiasa nchini.

Uchunguzi wa waandishi wetu umebaini kuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alishawahi kukasirishwa na mwenendo wa Sitta, ambapo alielezea maono yake kupitia kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania.

Imebainika pia kuwa suala la kutaka mashauriano na mwafaka ili kuzuia mgawanyiko katika asasi nyeti ambazo anaziongoza au anafanyia kazi si jambo kubwa kwa mheshimiwa Sitta.

Kupitia dondoo mbalimbali zilizotumika katika kufanya uchunguzi, lililo kubwa kwa mheshimiwa Sitta ni kupambana na kupima mambo kwa viwango na mizania yake kama anavyoona.

Aidha, imebainika kuwa kama mheshimiwa huyo angelikuwa anatambua ukubwa na hadhi ya ofisi yake, basi angelikuwa bahiri wa kufanya siasa zake kwenye vyombo vya habari na katika makanisa.

Inaonyesha kuwa kwa wale wanaojua historia ya Sitta, yanayotokea leo hii na yeye akiwa katikati ya matukio hayo, hawawezi kushangaa.

Uchunguzi wetu unarudi katika miaka ya nyuma ambapo kama kiongozi wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Samuel Sitta alishiriki na kupanga maandamano ya kupinga kuanzishwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Hata hivyo, tukio hilo liliishtua serikali aliyoongoza Mwalimu Julius Nyerere, serikali ya TANU na pia Taifa zima, ambapo vijana wake waliotumia pesa za wakulima na wafanyakazi walitakiwa kuwa na moyo wa kujitolea kuijenga nchi yao na pia kuchangia kwa namna yoyote maendeleo ya nchi.

Watu mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili ambao wanalikumbuka tukio hilo walisema kuwa wanafunzi hao walioandaliwa na akina Sitta waandamane walibeba mabango ya kuikejeli serikali ya Mwalimu Nyerere na mabango yenyewe yalikuwa na maandishi yaliyosomeka, "Afadhali ya mkoloni".

"Tukio hilo lilimuudhi sasa Mwalimu Nyerere mpaka akakifunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," anakumbusha profesa mmoja wa Chuo Kikuu ambaye alilishuhudia tukio hilo wakati huo.

Wakati Samuel Sitta anasema alitaka kunyang'anywa kadi ya Chama cha Mapinduzi na anamtaka Edward Lowassa awaombe radhi Watanzania kwa sakata la Kampuni ya mkataba wa kufua Umeme ya Richmond, yeye mpaka sasa hajaomba radhi kwa yale yaliyotokea 1966 ambapo taifa na serikali ilidhalilishwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kukosa uzalendo.

Aidha, uchunguzi wa gazeti hili unabainisha kuwa, akiwa Waziri wa Sheria na Katiba, katika Serikali ya Awamu ya Pili, chini ya uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi, Samuel Sitta alishiriki kwa kiasi kikubwa kulivuruga Bunge, kwa kuishauri serikali kukubali hoja za kundi la G 55 la kubadilisha Mfumo wa Muungano na kuanzisha Mfumo wa Shirikisho wa serikali tatu, ikiwa ni pamoja na kufufua serikali ya Tanganyika.

Taarifa hizo za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa kiini cha pendekezo hilo kilitokana na fikra za wanasiasa na wabunge ambao walikuwa na kiburi cha kuona kwamba Wazanzibar wanabebwa na kuwa na kauli kubwa kwa uongozi na utawala wa sehemu hii ya Jamhuri na hivyo kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kungelikomesha hali hiyo.

Matatizo yanayojitokeza leo hasa kuhusiana na Muungano ni matokeo ya Wazanzibari walijifunza nini kutokana na matukio katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa kuhusiana na jinsi kundi la wabunge (G 55) lilivyoibuka na jinsi serikali ilivyoshughulikia suala hilo.

John Malecela ambaye alikuwa Waziri Mkuu alilazimishwa kuachia nafasi yake na kuwa Waziri asiye na wizara maalum huku nafasi yake ikichukuliwa na Cleopa David Msuya, lakini cha ajabu Waziri wa Sheria na Katiba, Samuel Sitta ambaye kwa nafasi yake alitoa ushauri mbaya kwa serikali na hakujali chama, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na wala serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hakujiuzulu.

"Wakati akijiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa sekta husika (Nishati na Madini) walijiuzulu. Baadhi ya watu wanahoji kwa nini Sitta hakujiuzulu mwaka 1994 akaondoka na Malecela?" wamehoji watu hao.

Nafasi ya Waziri wa Sheria na Katiba ni nafasi nyeti hasa katika kipindi cha mabadiliko ya kusimika mfumo wa demokrasi ya vyama vingi, maandiko yote ya kubadilisha mfumo wa jamii, ambayo ni pamoja na mfumo wa vyama vya siasa na uongozi wa dola.

Inaonyesha kuwa kilichokuwa kimetokea mwaka 1993 ni sawa na yale yaliyokuwa yametokea mwaka 1968 ambapo wabunge wa chama cha TANU walikuwa wanataka bunge na serikali kuwa juu ya chama na kukinyima chama tawala nafasi ya kuelekeza siasa na sera za nchi.

Wabunge, akina marehemu Wilfrem Mwakitwange na Dk. Lyantika Masha na wengine walifukuzwa kwenye nyadhifa zao, wabunge walifanya hivyo kwa kutaka kuiga mfumo wa demokrasi wa nchi za Magharibi, bila kujali nafasi ya chama katika kuleta uhuru na pia kuelekeza taifa katika kuamirisha uhuru.

Akina Mwakitwange na wenzake walikumbatia matakwa ya demokrasi ya Magharibi bila kujali tofauti zilizopo katika nchi ambazo ubepari na matabaka yamekomaa na demokrasi kujengeka kwa zaidi ya miaka 300 na nchi changa ambapo maendeleo ya nchi hizo ni duni.

"Baada ya miaka 15, wanasiasa wa mrengo wa kulia ndani ya Bunge wakiongozwa zaidi na hisia zao, bila kujali nini kitatokea kuhusiana na umoja wa chama na Bunge, walijichukulia dhamana ya kuanzisha zali kubwa kutishia muungano na mustakibali wa nchi kwa ujumla, kilichowatuma kufanya hivyo ni kiburi cha baadhi ya wabunge na mawaziri wa serikali kujiona ni bora kwa kupanga hoja na kuamini katika mantiki ya hoja zao," anakumbusha mchambuzi mmoja wa masuala ya siasa nchini aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mchambuzi huyo anasema, Wabunge na baadhi ya mawaziri walinogewa dhana ya utanganyika na hivyo kuanzisha na kuridhia hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Kuwa na Rais wa Serikali ya Muungano Mzanzibari na pia kuwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ambaye ni Mzanzibari na madai mengine kutoka kwa viongozi wa siasa uchwara kutoka Zanzibar kuliwasumbua sana baadhi ya viongozi kutoka Tanzania Bara ambao waliona wajipatie madaraka kwa kuvunja misingi ya Muungano. Vile vile waliuona uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi, kwa haiba yake, kama Kiongozi Mkuu mwenye uwezo pungufu.

Mwalimu Nyerere katika kitabu chake anawalaumu sana aliyekuwa Waziri Mkuu wakati ule, Mzee John Samuel Malecela ambaye alikuwa Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni na Horace Kolimba, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri wa Serikali ya Muungano kwa kutojali maslahi ya chama na hatima ya Taifa.

Katika kuchambua mlolongo wa matukio, ni wazi baadhi ya wabunge na mawaziri walifanya makusudi na kusaidia kupitishwa kwa Azimio ambalo lilitaka muundo wa Muungano ubadilishwe na kutaka Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ikubali hoja ya wabunge.

Kutokana kwamba Mhe. Samuel Sitta alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba, maandiko makuu mawili yaani "TAARIFA YA SERIKALI JUU YA AZIMIO LA BUNGE KUHUSU HAJA YA KUUNDA SELIKALI YA TANGANYIKA NDANI YA MUUNDO WA MUUNGANO" na hotuba ya Waziri wa Sheria na Katiba ya kuwasilisha makadirio ya Wizara ya Sheria na Katiba katika kikao cha bajeti 1993/94 ambapo "Serikali ilielezea kusudio la kuandaa Waraka wa Serikali (White Paper) kutafuta maoni ya wananchi kuhusu Muundo wa Muungano".

"Ni jambo la ajabu katika historia ya Tanzania kwa serikali kukitaka chama kiridhie maamuzi ya kisiasa ambayo hayakutokana na vikao vyake vikuu vya Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa," anasema mwanasiasa mmoja mkongwe ndani ya CCM.

Aidha, anasema kilichokuwa kinaendelea ni kutafsiri matukio kisheria bila kujali athari zake kisiasa kwa kuzingatia matakwa ya mshikamano wa chama na uongozi wa dola kwa ujumla.

Serikali ya Rais Mwinyi ilikuwa ni serikali iliyogawanyika na pia chama kilikuwa kimetekwa na urasimu kiasi kwamba dhana ya dola kushika hatamu ndiyo ilikuwa imetamalaki.

Ni dhahiri kwamba ukuu wa chama katika kuonyesha dira na mwelekeo wa taifa ulikuwa unakabiliana na changamoto kubwa.

Inaelezwa kwamba ni katika kipindi hiki ambapo Chama kilianza kupoteza nafasi yake ya kuwa chama cha wanachama na badala yake kikaanza kuwa chama cha viongozi.

Hoja za wabunge kutaka kubadilishwa muundo wa Muungano na kupelekea kuundwa kwa serikali tatu ikiwemo serikali mpya ya Tanganyika ni jambo lililotazamwa kirasimu bila wahusika kuingia kwenye mjadala wa kina na kuibua sababu zenye uzito wa kubeba hoja.

Mwalimu Nyerere alishindwa hoja zilizokuwa na utaratibu uliokuwa unatumiwa na serikali kuhusiana na kuwasilisha hoja hiyo nzito.

"Kwanza lazima ieleweke kwamba Muungano ni wa pande mbili, kwa vipi Bunge la Jamhuri ya Muungano lilikuwa linajichukulia mamlaka bila kujali kwamba kuna Baraza la Wawakilishi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wa Zanzibar ambao wana nafasi yao katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano hasa kuhusu mabadiliko katika mfumo wa muungano?" anahojia mchambuzi wa masuala ya siasa.

Pia ikumbukwe kwamba kabla hoja haijaingia katika utaratibu wa kutungiwa sheria lazima kuwepo na mashauriano na wadau mbalimbali ndani na nje ya mfumo wa dola.

"Hayo yote Mheshimwia Sitta ambaye alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya ufundi (ya kisheria) hakuyaona na badala yake akagubikwa na ushabiki wa kisiasa pamoja na uhafidhina wa kuamini kwamba sheria ndiyo mwanzo na mwisho wa mambo yote," anaongeza.

Hivyo, Sitta hawezi kukwepa lawama kazi zile walizotupiwa akina Malecela na Kolimba na kwa hakika Sitta ilikuwa ajiuzulu au aondolewe kwenye nafasi yake kama waziri wa Sheria na Katiba kama Malecela alivyo ondolewa kwenye nafasi ya Waziri Mkuu.

Mapungufu ya serikali ya awamu ya pili chini ya Rais Mwinyi kwa kiasi fulani yalikuwa yanachochewa na baadhi ya mawaziri waliokuwa na agenda zao binafsi ambao walikuwa wanajiona kwamba wao ni bora kuliko wengine.

Na wakati huo huo kama siyo Mwalimu Nyerere kuingilia kati na kunusuru hali basi upepo mbaya lazima ungezamisha jahazi na vinginevyo tungekuwa tunagawana mbao.

Mwalimu Nyerere analiweka vizuri suala hilo pale anaposema: "13 Kwa kuwa suala la muundo wa nchi ni zito na ni la Kikatiba ushirikishwaji wa wananchi ni jambo lisiloweza kuepukwa.

Aidha, kwa uzoefu wetu na hali halisi ya nchi yetu ni lazima utaratibu wowote utakaokubalika uwezeshe Serikali ya Jamhuri ya Muungano kushauriana na chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar".

Haya tunayoyaona katika Bunge la sasa linaloongozwa na Spika Samuel Sitta, yanaturejesha nyuma kwamba Sitta ana mwelekeo wa siasa za kirasimu, ambazo daima hupendelea kukitupa chama kando bila kujali matokeo yake ya muda mrefu.

Ni wazi jambo la Bunge kuwa na makundi na Chama Cha Mapinduzi kudhoofika, havimsumbui Sitta.

"Tunachopata kutoka kwake ni kwamba yeye yuko sahihi, wengine wote wanaompinga ni mafisadi na kwa namna yoyote ile "anaongozwa na Yesu". Yesu, wa wote anaweza kubinafsishwa?" anahoji Profesa wa Chuo Kikuu.

SOURCE: TAIFA TANZANIA
Zina sound kama Siasa za maji taka hivi!!!!!!!!!!
 
Najibu hoja nyekundu lakini nianze kusema hivi, Mimi ningekuwa kundi la mafisadi ningewaambia wenzangu tubadili mbinu za mapambano maana kutumia magazeti ni mbinu iliyokwishagudnulika mwaka 2005. Huwezi kupigana vita yoyote kwa mbinu ileile ambayo adui yako kaishaijua.

Kwa nini Sitta hakujiuzulu uwaziri wa Sheria kuhusu G55 na suala la utanganyika? Kosa la magazeti ya mafisadi wanadhani watu hawasomi vitabu na hawana kumbukumbu.

Suala la Tanganyika na G55 lilimfanya Mwl. Nyerere aandike kitabu kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA. Ni kweli Nyerere aliiponda serikali na bunge kwa kukubali hoja ya Tanganyika na wale wabunge 55 (G55).

Lakini Nyerere alimsifia mtu mmoja tu ndani ya kitabu hicho naye ni Samwel Sitta, waziri wa sheria na katiba wakati huo. Kwa nini Nyerere alimsifia Samwel Sitta? Ninamnukuu Nyerere kwenye kitabu chake hapa chini kwenye aya ya kwanza alipoanza chapter ya USUGU WA VIONGOZI :

..."Jukumu la kueleza taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao, nilimtafutaNdugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki".

"Mapema nilikuwa nimeambiwa kwamba (Samwel Sitta) alikuwa ametamka bungeni kwamba hapo hoja ya kudai Selikali Tatu itakapoanza kujadiliwa, yeye ataipinga, maana jimbo lake la uchaguzi, Urambo, halikuwa limemtuma kwenda bungeni kudai Serikali ya Tanganyika. Wabunge wote wakweli wangeweza kusema hivyo hivyo. Hata Waziri Mkuu na katibu Mkuu wangeweza kusema hivyo hivyo. Wao ni wateuliwa na Rais, ambaye alikwisha kwenda bungeni siku chache tu zilizopita, na kupinga hoja ya Serikali Tatu. Katika kikao cha usiku wa jana yake nilikuwa nimewakumbusha hivyo viongozi wetu waheshimiwa".....Mwisho wa kunukuu.

Hivyo katika sakata zima la suala la Tanganyika Sitta anabaki kuwa waziri pekee aliyeonyesha msimamo huo ambao umetajwa na Nyerere.

Spika wa wakati huo Pius Msekwa hakusifiwa kwa msimamo ndani ya bunge au NEC. Msekwa alitajwa tu na Nyerere kwamba ndiye aliyetoboa mpango mzima wa bunge ambapo bunge lilijifanya limefunga hoja ya serkali tatu lakini kumbe kimyakimya na kijanja limeipitisha hoja hiyo kwa siri ambayo Msekwa aliitoboa kwenye vyombo vya habari. Ninamnukuu Nyerere tena hapa chini:

...Kwa sababu uamuzi wa kutaka Serikali ya Tanganyika ‘ndani ya muungano’ ulifanywa na viongozi wetu kwa hila, na kupitishwa bungeni bila mjadala, sisi wengine hatukujua lililotokea. Baadaye tulifahamishwa kuwa huo ndiyo ulikuwa uamuzi wa ‘bunge zima” kutokana na kauli ya Pius Msekwa aliyekuwa msimamizi wa kikao cha Bunge kilichofikia uamuzi huo....Nadhani viongozi wetu walitaka kuendelea kuficha na kuuvuga vuga, lakini yeye akatoboa. Nasikia baadaye aliitwa akakemewa. Sijui kwa nini...".....Mwisho wa kunukuu.

Hivyo tunaona kuwa ushujaa wa Samwel Sitta hata Nyerere aliujua na aliuandika. Mwandishi wa makala hii hana kumbukumbu ya kitabu hiki kwa sababu full time anasubiri kuneemeshwa na mafisadi. Na kama hakununua kitabu hiki mwaka 1994 basi aende kwenye makumbusho pale Butiama kuna vitabu zaidi ya 8000 vya iliyokuwa library ya Baba wa Taifa Julius Nyerere.
Asante sana Kieleweke kuna wengi wanafikiri mbinu ya magazeti bado ina nguvu sawa kama miaka ya 80s na 90s wakati sources za habari zimekuwa nyingi na uelewa wa watu umeongezeka hicho kitabu nafikiri ni muhimu maana kuna watu humo waliitwa wahuni Nyerere aliwajua lakini bado wanang'ang'ania madaraka kwa udi na uvumba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom