nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Imeandikwa tarehe 10 OCTOBER 2012 – NA ARNOLD SWAI, MOSHI
MJUMBE wa Halmashauri kuu y a Taifa ya CC (NEC), Samuel Sitta amesema kwa sasa chama hicho kiko imara zaidi ila alikiri moja ya tatizo kubwa ni mtandao iliyoanza kuundwa kwa ajili ya urais Mwaka 2015.
Hata hivyo, amedai kufkia mwezi ujao, tatizo hilo litakuwa limemalizwa, huku akiwaonya vijana wa Umojawa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) kutorubuniwa na watu walioanza kuunda mitandao midogo midogo ya kifisadi ndani ya chama kwa lengo la kugombea urais mwaka 20115.
Sitta ambaya pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ametoa kauli hiyo leo mjini Moshi wakati alipofika kuwasalimia vijana wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro walipokuwa wanafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na nafasi nyingine mbalimbali kwenye Ukumbi wa CCM Mkoa.
Amesema, mara baada ya kupatia ufumbuzi mitandao hiyo ya kuwania urais 2015, mwezi ujao chmama kitakuja na maamuzi mapya na kuzunguka nchi nzima kueleza mabadiliko na sura mpya ya chama hivyo hakuna mtu wa kukibabaisha chama hicho hata kidogo.
"Sisi sio punguani wa kuangalia vikundi vya kifisadi ili vichukue nchi, hilo hatutalifumbia macho kwa sababu kuna watu wanajaribu kuunda vimitandao tumejipanga ipasavyo na mwezi November tunakuja na maamuzi na tutazunguka nchi nzima kuelezea sura mpya ya chama", alisema Sitta.
Alisema vijana kwa sasa wanatakiwa watumie akili zaidi na si kujali matumbo yao kwa kununuliwa na baadhi ya watu, kwa sababu kiongozi wa aina hiyo hatakuwa na maslahi kwa wananchi na badala yake atakuwa mzigo wa Taifa.
Alisema chama ni imara na hakina haja ya kusumbuliwa na vijana wadogo wanaotaka urais na vyama vinavyotamba vitachukua nchi wakati vyenyewe vikiwa havina hata safu ya viongozi wa kuongoza.