Sitta: Msiisubiri Serikali kutaja walioficha mabilioni...

Sitta: Msiisubiri Serikali kutaja walioficha mabilioni...

Sita mnafiki mkubwa anataka watajwe, chenge alitajwa na akakiri kuwa ni vijisenti tu akiwa na maana kuna wezi wenzake wameiba zaidi yake na kama hawatamlinda ataoa siri, mbona hujashinikiza ashitakiwe? Au ndio mnatufanya watanzania wajinga, kwa taarifa tu sita na baraza la mawaziri akiwemo mwenyekiti mnahusika, kama hamhusiki wapelekeni mahakamani, nini maana ya kuwaja?
 
Swali je kuna haja gani ya kuwataja wezi ambao hata wakishajulikana hawachukuliwi hatua zozote za kisheria?.
Nchi hii imekuwa na watu wa ajabu sana hawa watu wakishajulikana watapanda chati katika siasa za Taifa hili.

Tumeshuhudia wengine wakituambia dola 1.5m ni vijisenti bila hata kuguswa na Mamlaka za kisheria kujua walizipataje na sasa ni wenyeviti wa kamati nyeti za Bunge ambazo ndizo zina wajibika kufuatilia fedha hizi nje ya nchi na kwa wale mnaofuatilia mambo huyo jamaa huko kwao Mkoa mpya wa simiyu jamaa amesimikwa kuwa Mtemi wa jamii ya huko.

Katika hali ya namna hii ambapo Masikini ni wengi wakiwa hawana Elimu,Mahitaji muhimu ya kijamii kama uwezo wa kupata chakula na huduma za Matibabu kuna hitajika nguvu ya ziada ili kuleta utambuzi wa kuelewa Madhari ya wizi huu kwa jamii ya Watanzania.
 
Serikali imeshindwa kuwataja kwa sababu wao ndo wanaunda hiyo serikali. CHADEMA ilishawahi kuwataja lakini hawajachukuliwa hatua na juzi Raisi Kikwete amemsafisha fisadi mwingine waziwazi. Sasa inaonekana hata wakitajwa hatutegemei serikali ichukue hatua.

SItta mwenyewe kashindwa kutaja, Mwakyembe baada ya kujua ni serikali yake mwenyewe ameamua kukaa kimya. Laiti angekuwa ni mtu nje ya chama na serikali, wangeshamfukua kokote alipo, Taifa zima lingejua.

Sasa hivi naona CHADEMA wameamua kuwashitaki hao mafisadi kwa WANANCHI kupitia mikutano yao, cha kushangaza serikali tena badala ya kuwafanyia uchunguzi (kama Sitta anavyojaribu kujishaua hapa), wao wanakuwa mstari wa mbele kuwaita CHADEMA
wachochezi!!!
 
Mimi ninavyojua kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa na sio kwa kuropoka tuu. Serikali inauwezo wa kuwataja, lakini kama mtendaji mkuu naye ni mtuhumiwa, chombo gani cha kujitegemea kinatakiwa kuwataja na kuchukua hatua zaidi hapo ndio sijui. Kutaja peke yake bila kuwashitaki haitasaidia chochote, na kumshitaki mtu ushahidi wa kutosha unahitajika ndiyo maana Mzee wa vijisenti hakushitakiwa.
 
Hivi Kama JK yumo ambapo naona kuna posibilities kuwa kwamba yumo hamjui kuwa Zomba atakuwa anahangaika na intelegensia yake kuchafua zaidi maana hawako smart enough kwenye issue sensitive. Mpeni muda Zomba harafu mje mmlipue na yeye
 
So strange......hata gazeti (Mwananchi) pia limeshindwa kuwataja!
 
hii serikali imeoza inanuka! na NSSF yetu bado wameikalia! ni mashetani yaliyo hai! hayastahili hata kuitwa WATANZANIA maana wanashibisha matumbo yao kwa jasho na kipato kidogo cha MTANZANIA!
 
Mh Sita acha uoga, source zako zinawajua na hata wewe umekua Waziri tangu awamu ya Kwanza, lazima unawajua. Tanzania haitajengwa na waoga kama wewe, wapenda vyeo
 
Mh Sita acha uoga, source zako zinawajua na hata wewe umekua Waziri tangu awamu ya Kwanza, lazima unawajua. Tanzania haitajengwa na waoga kama wewe, wapenda vyeo

hivi kumbe ni mwoga eeh! halafu kasema uongo kivipi si kweli?
 
Wa kwanza atakuwa Chenge mzee wa vijisenti
je Kalamagi aliyekwenda kusaini mkataba wa Buzwagi Uingereza atapona?
Na vipi Mhe Lowasa (Nyerere alisema kwa pesa alizokuwa anamiliki wakati ule atakuwa alikuwa na pori la ng'ombe)
Nina mashaka kama rais mstaafu Mkapa atasalimika..
endelea ku speculate
 
Kwa hiyo sitta anamaanisha selikali yake ni dhaifu mpaka inaitaji msaada wa watu binafsi kuwataja hao watu? Waachie ngaz kwanza ndo tuwasaidie
 
Haitoshi...lazima wahusika wachezee mvua za kutosha vingivevyo hili tatizo sugu la mafisadi ndani ya Serikali kamwe halitakwisha. Wale wa EPA, Kigoda, Meremeta, Rada n.k. mpaka kesho kutwa bado wanapeta na mabilioni yao.


JK alisema hamna sababu ya kuwafunga wanachotakiwa warudishe fedha nchi yetu wanahuruma sana wezi wanabembelezwa. ngoja tuone na hawa wenye mafedha yao huko nje
 
sita namkubali yuko juu maana huko CCM hawampendi kwa sbb ni mkweli na utasikia wakimwambia kwa nini ameyasema hayo hadharani na asiseme kwenye vikao vya baraza au vya chama
 
Six nae anamiliki mbona kati ya mawaziri wote yeye ndio kajistukia? please Membe/Dkt Slaa hebu tutajieni
 
Duh!hii inchi mimi ndio maana nasema tunavumilia kuwa kuwa watz na wala hatujivunii
 
Kwa hiyo unataka awataje hata kama hawajui?
Usiwe mvivu wa kufikiri, hakuna mnafiki kama Sitta. Unakumbuka alipokuwa Spika? Alitoa kauli gani orodha ya Mwembeyanga ilipowekwa hadharani? Alitoa kauli gani list ya wezi wa EPA ilipoanikwa hadharani? Je unakumbuka siku mkewe alipotajwa kushiriki katika kitendo cha rushwa alivyong'aka?

Leo anatajwa kama mpiganaji ndani ya CCM na yeye eti anajipambanua hivyo...je anapambana hasa na nani? Mbona kila siku anakula nao na kulala nao? Mbona hadi leo hajawataja waliompa sumu Mwakyembe aliodai kuwafahamu? Mbona mchana kweupe na macho makavu aliikana CCJ huku akitajwa kuwa kinara katika kuianzisha? Halafu kuna watu wanamwona kama shujaa wao...ni katika nini? Katika wizi na ufisadi au katika unafiki na ulafi?

Watu kama Sitta CCM ndicho chama chao kwani usalama wao upo ndani ya CCM...nje ya CCM watakuwa kama samaki kumtoa majini, kwisha habari yake. Pamoja na wao kuihitaji CCM ili wawe salama ndivyo na CCM inavyowang'ang'ania kwa mtindo wa nikune nikukune kwa sababu inajua udhaifu wao. Kama vile mtoto mdogo akilia kidogo tu hiyoo chupa ya maziwa mdomoni kimyaa na usingizi hapo hapo.

Sitta anawajua sana wenye pesa benki za Uswisi lakini eti awataje, thubutu! Huo ujasiri atautoa wapi? Angekuwa jasiri angekubali rushwa ya kupewa uwaziri Afrika Mashariki? Acheni kusifia watu waliotanguliza matumbo yao na wasio hata na chembe cha uadilifu, kuweni na huruma na taifa letu tafadhalini. Eti Sitta, mtu mzima ovyooo!
 
Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Fedha la Global Financial Integrity, unaonyesha kuwa tatizo la utoroshaji wa fedha nchini limekuwapo katika awamu zote za Serikali zilizoiongoza Tanzania, lakini Awamu hii ya Nne imetia fora.

Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 1970 hadi 2009, unaonyesha kuwa katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).

Now we know why Tanzanians are poor, even Mr. President must know why his people are poor! He once said ' I do not know why Tanzanians are poor'. For sure his government knows and has the details of alleged Tanzanians to possess the whole amount in Suiss. My advice to Chadema, pls do not rush to mention names of the account bearers for Tanzanians' money abroad. Keep digging the whole saga and as times approach to 2013-5 this will be great agenda for Tanzanians to know why we need revolution.

Colleagues,

Is there a way that our new constitution can reflect measures (including death sentence for leaders who have been trusted to such extent and yet misuse their powers? I think it is possible-I will suggest this ‘kwa tume ya kukusanya maoni ya katiba’. I pursue others to forward the same suggestion.
 
Back
Top Bottom