Sitta: Msiisubiri Serikali kutaja walioficha mabilioni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Msiisubiri Serikali kutaja walioficha mabilioni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 21, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  - AWASHANGAA WANAOIPA MUDA HUKU WAKIWAFAHAMU WAHUSIKA
  - ASEMA HAIWEZEKANI MWANASIASA KATIKA NCHI MASKINI AWE BILIONEA
  - ATAKA WAKAMATWE WAFIKISHWE MAHAKAMANI


  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewataka wanaotangaza kuwafahamu vigogo walioficha mabilioni ya fedha nje ya nchi kuwataja mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao badala ya kuisubiri Serikali kufanya hivyo.

  Kauli hiyo ya Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), imekuja wakati baadhi ya wanasiasa, wakiwamo wabunge kutishia kuwataja watu hao, lakini wakisisitiza kuwa ni pale tu Serikali itakaposhindwa kufanya hivyo.

  Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Fedha la Global Financial Integrity, unaonyesha kuwa tatizo la utoroshaji wa fedha nchini limekuwapo katika awamu zote za Serikali zilizoiongoza Tanzania, lakini Awamu hii ya Nne imetia fora.

  Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 1970 hadi 2009, unaonyesha kuwa katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).

  Akizungumza katika mahojiano maalumu, kuhusu nini kifanyike ili kuiokoa Tanzania isiendelee kufilisiwa na watu wachache, Sitta alisema anasikitishwa na watu hao kuogopa na kuwaficha watu wanaofisadi mali za nchi na hasa pale inapokuwa wahusika ni vigogo wa Serikali.

  Alisema vigogo hao ni sababu ya watu kupata kigugumizi katika hili akihoji: “Kwanini linapokuwa ni suala linalowahusu hawa wanaoitwa vigogo hawatajwi?”

  Sitta ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini katika awamu tofauti, alisema haoni kama kuna kosa kumtaja hadharani mtu aliyeficha fedha nje ya nchi huku akisababisha Watanzania kuendelea kukabiliwa na maisha magumu.

  “Watajwe! Kama ni Samuel Sitta ameficha fedha nje atajwe. Kwa kweli mimi sioni kama kuna dhambi yoyote kumtaja,” alisema Sitta huku akisisitiza kwamba huo ni msimamo wake binafsi unaotokana na uzoefu wake kwenye uongozi wa nchi na siyo kwa mamlaka aliyonayo ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Alisema njia nzuri ya kukomesha tabia hiyo ni kuwataja na vyombo husika kuwafikisha mahakamani kwa kuzingatia kuwa sheria ni msumeno, haipaswi kubagua aliye mdogo au mkubwa kwa maana ya wadhifa katika nchi.

  Sitta ambaye pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema: “Swali la kwa nini hawatajwi, ni jambo la kushangaza.”

  Alisema amesikia na kuwasoma baadhi ya wanasiasa wakitishia kuwa watawataja wahusika iwapo Serikali haitafanya hivyo, lakini akasema haoni sababu yoyote ya mtu kusita katika kuokoa taifa dhidi ya wizi wa fedha za umma.

  “Haiwezekani kwa mwanasiasa yeyote katika nchi maskini kama Tanzania au kiongozi wa Serikali kuwa na utajiri wa mabilioni ya fedha.”

  Alisema hata kama anafanya biashara, siyo rahisi kuwa na utajiri wa kiwango hicho hasa ikizingatiwa kuwa hutumia muda mrefu kulitumikia taifa.

  “Sisi tunaofanya kazi serikalini, tunatoka saa moja usiku. Sasa muda huo wa kufanya biashara ni saa ngapi?”

  Tuhuma hizo ziliibuka bungeni Jumatano iliyopita baada ya Kambi ya Upinzani kudai kwamba inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali haitafanya hivyo.

  Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kambi yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha alisema miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Benjamin Mkapa.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba kuna Watanzania 27, wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara walioficha mabilioni ya fedha huko Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

  Katika uchunguzi huo ilibainika pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (takriban Sh300 bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1,600 kwa Dola ya Marekani.

  Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne huku anayefuatia akiwa anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki dola milioni 10 (Sh16 bilioni).

  Hiyo inamaanisha kwamba vigogo watano tu katika kundi hilo, wanamiliki Dola milioni 126 (Sh201.6 bilioni) sawa na asilimia 67.74 ya fedha hizo, wakati wengine 22 waliobaki wanamiliki Dola milioni 60 (Sh96 bilioni) sawa na asilimia 32.25.

  Kwa hesabu za kawaida, kiasi cha Sh300 bilioni, kinaweza kugharimia ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 33,300, ikiwa chumba kimoja kinagharimu kiasi cha Sh9 milioni.

  Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wafanyabiashara wanaomiliki kiasi cha dola kati ya milioni mbili na milioni saba. Kadhalika, wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere ambao akaunti zao zina kiasi kisichozidi Dola 500,000 kwa kila mmoja.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  ....Nakubaliana na Sitta kwamba wahusika wote walitakiwa wawe rumande kusaidia katika uchunguzi, lakini wanapeta tu kutokana na kuwepo Serikali DHAIFU.
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,529
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  BAK, inaonekana na yeye anawajua, si awataje basi !!
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Sasa Sitta, unaposema serikali isisubiriwe kuwataja... Unamaanisha nani atawaburuza mahakamani? Serikali ndo imeibiwa fedha, na inawajibika kuwapeleka mahakamani wahusika. Ndio maana upinzani inatia pressure kwa serikali kuwataja ili iwapeleke mahakamani. Viini macho.com
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ...Alisema njia nzuri ya kukomesha tabia hiyo ni kuwataja na vyombo husika kuwafikisha mahakamani kwa kuzingatia kuwa sheria ni msumeno, haipaswi kubagua aliye mdogo au mkubwa kwa maana ya wadhifa katika nchi.Sitta ambaye pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema: “Swali la kwa nini hawatajwi, ni jambo la kushangaza.”
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  JW ashinikizwe awataje hakuna sababu yoyote ya kuwakingia vifua mafisadi hawa.
   
 7. W

  Wajad JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 1,130
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 180
  Akaunti zikafungwe, fedha zirudishwe nchini
   
 8. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,918
  Likes Received: 12,136
  Trophy Points: 280
  Ukweli husemwa:

  Kwani kulikuwa na kigugumizi gani kwa zitto Kabwe kuwataja hao wezi.
  Kama ameweza kutaja ni watu wa aina gani kwa nini hakutaja majina yao. Kwa kutokufanya hivyo, inaonyesha kama hana uhakika na kila alichokuwa anakisema ama ana waogopa.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Sitta amenena. Kama unawajua wataje yaishe mambo ya kusema serikali iwataje yanatupotezea muda.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Haitoshi...lazima wahusika wachezee mvua za kutosha vingivevyo hili tatizo sugu la mafisadi ndani ya Serikali kamwe halitakwisha. Wale wa EPA, Kigoda, Meremeta, Rada n.k. mpaka kesho kutwa bado wanapeta na mabilioni yao.

   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Utawala huu wa JK unategemei nini
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kulindana hadi mwisho...Membe njia ya kukutoa ndio hiyo..nenda kazidai hizo pesa zije kujenga madawati faster
   
 13. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sitta wewe ni serikali maana kwanza ni waziri na pia ni mwanasiasa kwa nini usiwataje hadharani? ulichosema nikizuri ila chama chako kina uchafu ulio kithiri kupita maelezo ndio maana hata wewe tunashindwa kukuamini ukiwa uko ndani ya ccm
   
 14. d

  dada jane JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hali hii inaleta kiburi sana hata kwa watendaji wadogo. Tuko huku jwenye halmashauri hali ni mbaya. Fedha zinatafunwa kama watu hawana akili nzuri. Hii ni kutokana na uzembe na udhaifu ulioko huko juu. Nchi imetolewa utumbo na nyamanyama zote linatembea lidubwasha tupu ambalo wakati wowote litadodoka.
   
 15. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Ngoja sisi tupost post hapa tu tutoe mapovu lipite kama yalivopita mengine tusubiri skendo nyingine!
   
 16. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Andrew Chenge aliwahi kukiri kumiliki vijisenti huko nje, vijisenti hivyo hivikutolewa chanzo chake! Serikali ilichukua hatua gani? CHADEMA ilishawahi kutoa majina ya mafisadi hadharani mchana kweupe, jee hatua gani serikali ilichukua hatua gani? Nyimbo za Samweli Sita ni za bure kabisa,mbona yeye na rafiki yake Mwakyembe hawakumalizia ile "single" yao sumu!
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yeye SITTA kwanini hawataji,Anataka nani awataje?Hebu awe mzalendo bana
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kama tunajua serikali haiwezi kuchukua hatua sasa ya nini tuitake tena ndio itaje? Wanaowajua wawataje wananchi watachukua hatua.
   
 19. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wacha tumwombe Julian Assange wa Wikileaks atutumie hayo majina mara moja.
   
 20. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hii ndio namna nzuri sana ya kuiwajibisha serikali ya kifisadi ili ijue kwamba mambo yake yako nje.
   
Loading...