Sitta kuongoza shughuli za Serikali Bungeni wiki hii

Sitta kuongoza shughuli za Serikali Bungeni wiki hii

Hii ni sehemu ya "intrigues" za siasa za magogoni. Hii ni body language kwa Lowassa! Sitta kukaimishwa u-PM haiwezi kufanyika bila approval ya JK mwenyewe.

Baada ya Lowassa kutunisha misuri yake bungeni kwa kushangiliwa sana na wabunge wa CCM, mheshimiwa JK anamuonesha kuwa naye bado analo rungu linaloweza kumwangamiza. Rungu hilo ni madaraka na jinsi anavyoweza kucheza nayo kadri mazingira yanavyoruhusu. Kuteuliwa Sitta kukaimu u-PM ni mojawapo ya lugha za kiuongozi za JK kwa Lowassa.
 
Duh hii imekaa kimtego sijui mkuu wa malaigwanani AM anajisikiaje ?.
 
Sina nia mbaya na mtoto wa mkulima ngoja naye afurahi, maana na rais wetu aliwahi kuulizwa kwanini ziara zake nje ya nchi zinakuwa nyingi?.Mh. akajibu "jamani ndugu zangu mnataka nibaki hapa kila siku tu kula mihogo".
 
sitta wakomeshe, usikiachie hiki cheo - akirudi safari atajua pa kukaa. lol
 
Imagine hiyo ofisi ingeachiwa kambi ya upinzani kwa wiki moja mambo yangekuwaje lets say Zitto nafikiri siku Pinda anarudi suala la posho lingekuwa historia.

hahahahahah tehe tehe teh teh yaani angekuta hadi suala la umeme limepatiwa ufumbuzi hahahahahahah
 
Bila shaka, kwa mara nyingine tena, hakuna maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wiki hii....
 
Ofisi ya Waziri Mkuu ingawa haina Naibu Waziri Mkuu lakini ina mawaziri walioko chini yake kama Bw. Lukuvi, Wasira na Bw. Mwanri,
Kwanin asishike mmoja wao?

mkuu kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kama waziri mkuu hayupo basi 'the most senior minister' kwenye cabinet ndiye anayekaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, na kwa muktadha huo, inaonekana Mh Sitta ndo anaqualify

hata hivyo ameanza kuonyesha cheche zake kwa kupingana na Spika kuhusu suala la mizani ya kupimia pamba inayowaibia wakulima huko shinyanga...wakati Mh Spika akitaka kanuni za Bunge zitumike kuwasilisha hoja hiyo hasa baada ya waziri husika kuonekana kutojua kama msimu wa kununua pamba umeanza, Sitta alisimama na kusema kuwa serikali ya CCM haiwezi kusubiri kanuni wakati wakulima wanaibiwa so watalifanyia kazi mara moja...
 
mkuu kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kama waziri mkuu hayupo basi 'the most senior minister' kwenye cabinet ndiye anayekaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, na kwa muktadha huo, inaonekana Mh Sitta ndo anaqualifyhata hivyo ameanza kuonyesha cheche zake kwa kupingana na Spika kuhusu suala la mizani ya kupimia pamba inayowaibia wakulima huko shinyanga...wakati Mh Spika akitaka kanuni za Bunge zitumike kuwasilisha hoja hiyo hasa baada ya waziri husika kuonekana kutojua kama msimu wa kununua pamba umeanza, Sitta alisimama na kusema kuwa serikali ya CCM haiwezi kusubiri kanuni wakati wakulima wanaibiwa so watalifanyia kazi mara moja...
Kwa kipindi hiki cha Sitta kuongoza shughuli za Serikali, Makinda asipobadilika basi hatobadilika kamwe. Sitta ni Chuo kwake!
 
Labda ziara ya Mhe.Pinda huko Brazil atabadirisha Tanzania kuitwa "Shamba la bibi" anataka angalau akumbukwe kwa kitu kimmoja alichofanya vizuri kama PM.
 
Imagine hiyo ofisi ingeachiwa kambi ya upinzani kwa wiki moja mambo yangekuwaje lets say Zitto nafikiri siku Pinda anarudi suala la posho lingekuwa historia.

Magwanda bana, wanapenda madaraka. Ombeni na nyie wananchi wawachague mshike dola acheni kuwa na tamaa !
 
Ofisi ya Waziri Mkuu ingawa haina Naibu Waziri Mkuu lakini ina mawaziri walioko chini yake kama Bw. Lukuvi, Wasira na Bw. Mwanri,
Kwanin asishike mmoja wao?
Hapo penye red, huyu bwana huwa analala tu bungeni.
 
FEEDBACK: acha kuwadanganya watu! Pinda anaenda Korea na sio Brazili. Majitu mengine bwana
 
mkuu kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kama waziri mkuu hayupo basi 'the most senior minister' kwenye cabinet ndiye anayekaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, na kwa muktadha huo, inaonekana Mh Sitta ndo anaqualify

hata hivyo ameanza kuonyesha cheche zake kwa kupingana na Spika kuhusu suala la mizani ya kupimia pamba inayowaibia wakulima huko shinyanga...wakati Mh Spika akitaka kanuni za Bunge zitumike kuwasilisha hoja hiyo hasa baada ya waziri husika kuonekana kutojua kama msimu wa kununua pamba umeanza, Sitta alisimama na kusema kuwa serikali ya CCM haiwezi kusubiri kanuni wakati wakulima wanaibiwa so watalifanyia kazi mara moja...

Mkuu hata nami nimei note hiyo. Ex-Naibu Spika imebidi akubali yaishe kwa kuyeyushia nyundo toka kwa Mr Six ambaye bado ana dungu na kiti kile.
 
yaani wanamuogopa LISSU mpaka wanaanza kumrudisha Sitta ki nyemela nyemela - duh hii kali sana.

Ningekuwa mimi Samweli SIX ningeomba posho ya consultation - sifanyi kazi ya bure si walinitoa u-spika wenyewe.
 
Kwa taarifa zisizo rasmi ni kuwa ile takwimu ya safari 312 iliyotolewa hapa jf kuwa mkulu kavunja record ya Vasco Dagama imeanza kuleta manung'uniko ndani ya magogoni na ktk baraza la mawaziri!

Inawezekana nimoja ya sababu za mkwele kuipotezea safari ya kwa Gaucho!

NB: Sisi wadau na watz kwa ujumla tutaendelea kupinga kwa nguvu zote ufujaji wa pesa za umma kwa mambo ya anasa unaofanywa na serikali ya ccm!
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta atakahimu nafasi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuongoza shughuli za Serikali bungeni kwa kuwa anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kwenda Brazil kikazi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge mjini Dodoma, ziara ya Pinda ina lengo la kuvutia uwekezaji wa nishati ya gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba tayari Brazil imeonyesha dhamira ya kutafiti nishati ya gesi katika Ukanda wa Kusini na katika mpango huo nchi hiyo imekusudia kuweka mtambo mkubwa wa kutafiti gesi ukanda wa Mtwara ili kumaliza tatizo la nishati ya umeme.

Kufuatia ziara hiyo ya kiserikali, Waziri Sitta atakaimu nafasi yake bungeni kwa wiki nzima mpaka Julai 11, mwaka huu.Mkutano wa Bunge unatarajiwa kuendelea baada ya mapumziko ya mwisho mwa wiki na wabunge leo watapokea makadirio ya bajeti katika wizara mbili zilizopo chini ya Ofisi ya Rais.

Wizara zinazotarajia kuwasilisha hotuba zao ni pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu ambazo mjadala wake utakwenda pamoja.

Wiki iliyopita wabunge walipitisha makadirio ya matumizi katika wizara na idara zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Sh 197 bilioni zilipitishwa.

Leo wabunge wataanza kupokea makadirio ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira kuwasilisha na zote zitajadiliwa kwa siku mbili.

Jumatano mpaka Ijumaa Bunge litakuwa likijadili makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambazo zitajadiliwa kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Jamani shamba la bibi!!

Hivi bado wanafanya utafiti tu?

Kwa nini isiwe kuchimba gesi iendelee kuwa utafiti jamani?

Hapo napo nahisi jamaa watapewa msamaha wa kodi, MUNGU wangu hii nchi bwana kazi kweli kweli!!!
 
Back
Top Bottom