Sitta kuendeleza moto bungeni.................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,272
911,155
Gazeti la Mwananchi limetuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Spika Mstaafu Mzee Sitta akiaahidi ya kuwa ataendeleza moto ule ule aliokuwa nao katika kutetea haki za wanyonge...............

Vile vile, gazeti la Nipashe limeripoti ya kuwa Mheshimiwa Sitta kaahidi ya kuwa ataendelea kuwa mkweli na unafiki kwake ni mwiko...............

Nionavyo huu ni ujumbe mzito kwa JK kama alifikiri Mzee wetu Sitta sasa amemziba mdomo kwa kumkata ngwala ya Uspika lakini Bungeni Mzee wetu Sitta atachachamaa kuhakikisha haki za wanyonge zinalindwa...............Hongera Mzee Sitta kwa huo ujasiri uliouonyesha kwetu......maana huko bungeni hatuna makimbilio mengi tukizingatia Chama cha mafisadi ndicho kimekamata hilo bunge na sijui tutaponea wapi..............na hivi sasa wanakazana kuanzisha hoja za udini ambazo hazipo ili tusahahu matabaka ya kimapato ambayo ndiyo chimbuko la migawanyiko kwetu.............
 
Mr 6 ni mjanja!!!! Hapa anamwambia JK kwamba usiponiteua kuwa waziri, nitakuwa mwiba kwa kambi ya mafisadi, JK akiwemo; na mkinibana zaidia nitatimkia CDM, na jimbo la Urambo kuhamia CDM!!!!!!!!!!!!!!! Can JK na sisiemu yake afford kummiss, hasa chiligatije hatatamani kumrarua??????????????????????? Tusubiri orodha ya mawaziri leo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Gazeti la Mwananchi limetuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Spika Mstaafu Mzee Sitta akiaahidi ya kuwa ataendeleza moto ule ule aliokuwa nao katika kutetea haki za wanyonge...............

Vile vile, gazeti la Nipashe limeripoti ya kuwa Mheshimiwa Sitta kaahidi ya kuwa ataendelea kuwa mkweli na unafiki kwake ni mwiko...............

Nionavyo huu ni ujumbe mzito kwa JK kama alifikiri Mzee wetu Sitta sasa amemziba mdomo kwa kumkata ngwala ya Uspika lakini Bungeni Mzee wetu Sitta atachachamaa kuhakikisha haki za wanyonge zinalindwa...............Hongera Mzee Sitta kwa huo ujasiri uliouonyesha kwetu......maana huko bungeni hatuna makimbilio mengi tukizingatia Chama cha mafisadi ndicho kimekamata hilo bunge na sijui tutaponea wapi..............na hivi sasa wanakazana kuanzisha hoja za udini ambazo hazipo ili tusahahu matabaka ya kimapato ambayo ndiyo chimbuko la migawanyiko kwetu.............

Hatakua na nguvu sana maana kuna party caucas, kama walitaka kumvua uanachama akiwa spika nini kitawazuia sasa hivi hana cheo chochote? I think he need to be very careful now maana yuko exposed sana kwa sasa. By the way nini kinamzuia kuasi na kutimka ili apambane kwa uhuru na uwazi? Sitta make up your mind now, jump the ship or keep quite. If you jump the ship ur legacy will never fade whether alive or dead, now make a decision before its too late
 
Sita ni mnafiki, anajua kabisa kuwa hana platform ya kuwa mwiba kama anavyotaka watu waamini. Kama ni mkweli akatae uwaziri ambao kuna uvumi kuwa ameandaliwa ili kumpoza. Huyu si ndiye fisadi aliyetumia mamilioni kujenga ofisi ya Spika huko Urambo wakati akijua kuwa uspika si nafasi yake ya kudumu na watoto wa wapigakura wake wakikaa sakafuni kutokana na ukosefu wa madawati. Napongeza kitendo cha mafisadi wenzake kumng'oa kwenye uspika, wacha yaendelee kutafunana.
 
Mr. Sitta unauma na kupuliza lakini sioni haja kwake kuwa waziri alifikia rank kubwa kwa nini aombe chini kama alivyo Lowasa PM urudi kuwajibika current PM uroho huo wa madaraka
 
Mr. Sitta unauma na kupuliza lakini sioni haja kwake kuwa waziri alifikia rank kubwa kwa nini aombe chini kama alivyo Lowasa PM urudi kuwajibika current PM uroho huo wa madaraka

Kama nia yake ni heshima kutoka kwa wanyonge, basi abaki mbunge!

Nilisikia kua amekataa uwaziri?
 
Akatae uwaziri??????????????????????????????!!!!!!!!!!!!!!Hebu tuhabarishe zaidi MwanaJF!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:whoo::behindsofa:
 
Hatakua na nguvu sana maana kuna party caucas, kama walitaka kumvua uanachama akiwa spika nini kitawazuia sasa hivi hana cheo chochote? I think he need to be very careful now maana yuko exposed sana kwa sasa. By the way nini kinamzuia kuasi na kutimka ili apambane kwa uhuru na uwazi? Sitta make up your mind now, jump the ship or keep quite. If you jump the ship ur legacy will never fade whether alive or dead, now make a decision before its too late

Hakuna cha party caucas wala nini mbona akina Dr. Mwakyembe wali-survive mwache abaki hukohuko ili aendelee kutu-update nyendo za mafisadi...
 
By the way nini kinamzuia kuasi na kutimka ili apambane kwa uhuru na uwazi? Sitta make up your mind now, jump the ship or keep quite. If you jump the ship ur legacy will never fade whether alive or dead, now make a decision before its too late
Sitta kamwe hawezi kuwa mwiba kwa CCM wakati ni mmoja wao..........................inabidi atoke huko halafu kura irudiwe kule Urambo Mashariki na atarudi tu bungeni kwa tiketi ya Chadema na ikibidi awashawishi wabunge wengi wa CCM kuachia viti vyao ili kukiondoa CCM madarakani................................kwa mchango huo tutamkumbuka kuwa kweli alikuwa ni jemedari wa taifa hili.......................

lakini hizi rasha-rasha nyingine sisi hatujui.......................ni za kusaidia umma au kujisaidia yeye mwenyewe......................
 
Hapa umenena Ruta, hebu wanaJF tupeleke jumbe kuhamashisha, sijui kama huy jamaa anasoma JF!!!!!!!! Hivi ana guts za kukataa uwazir????????????????????
 
JK atamnyamazisha kwa Unaibu PM au Uwaziri wowote kama tetesi zinavosema.

Akishapewa huo tu atakuwa kimya. Huwezi kuikosea Serikali ambayo wewe ni Waziri wake.Mambo ya Collective responsiblity na caucas hawezi kuyakwepa.
 
Mheshimiwa Samweli Sitta alipokosa Uspika alikuwa mwepesi kuhusisha hilo na yeye kusulubiwa na mafisadi na alidai ya kuwa hata akiwa Mbunge tu ni safi sana kwa sababu kwanza kapata fursa kubwa ya kupambana na ufisadi...........................Wengi tulimtegemea Uwaziri aukatae ili atekeleze azma yake ya kuwa huru zaidi kama Mbunge na hivyo kupambana na ufisadi................

Kwa kuukubali Uwaziri, Mheshimiwa Sitta ameapa kuwa mtiifu kwa JK na serikali na hiyo ikimaanisha uwajibikaji wa pamoja......................collective responsibility...................Hicho ni kiapo cha kulindana na wala siyo cha kupambana na ufisadi..........

Sasa leo kwenye magazeti haya ya..............Mwananchi tunasoma kichwa cha habari kisemacho.................JK kanipa nafasi nyingine ya kupambana na ufisadi .........Mheshimiwa Sitta angelikuwa ni mkweli angegundua ya kuwa JK ndiye kinara wa ufisadi na hivyo hawezi kumpa yeye nafasi nyingine ya kupambana na ufisadi ila kamwingiza serikalini ili kumziba mdomo na ashindwe kupambana na ufisadi..................

Majira inaripoti ya ...........Sitta: Vita vya ufisadi sasa kwa mawaziri..................Hivi hii kauli ni ya kweli yaani raia wa kawaida hawawezi kupambana na ufisadi ila ni kwa mawaziri tu.........Jamani Sitta ni vyema akawa mkweli kwa kutambua ya kuwa vita dhidi ya ufisadi ni vya raia wote.............

Habari Leo nako Sitta amenukuliwa akijigamba ya kuwa.............Hatutauza Nchi.................Sijui ni nani kalituhumu Baraza hili la Mawaziri kuwa litauza Nchi................Unapoona mtu anaanza kujibu maswali ambayo hajaulizwa ujue nafsi yake inamsuta....Tutegemee serikali hii kugubikwa na ufisadi na wala siyo vinginevyo......................

Nionacho mimi ni kuwa Mheshimiwa Sitta kajivalisha joho la vita dhidi ya ufisadi na hawezi kuvipigana huku hata hayupo tayari kujibu hoja za kuufunga mjadala wa Richmond bungeni wakati akiwa Spika ili kuwanusuru mafisadi...............Apaswa kuzungumzia matumizi ya ofisi ya Bunge ambako kuna tuhuma nyingi kuwa alikuwa akiendesha ka-ufisadi pale.........Hata ujenzi wa ofisi ya Mbunge kule Urambo Mashariki kwenye Jimbo lake la uchaguzi mbona wabunge wengine hawakutendewa kama yeye...........huku kujipendela kwaleta hisia ya ubinafsi na kuwa yeye ni mpenda makuu....na hivyo ni matumizi mabaya ya madaraka na ofisi ya umma.............Mheshimiwa Sitta apaswa kutujuza hivi ilikuwaje hata asikemee NEC kwa kumwibia Dr. Slaa kura kama kweli yeye ni mpambanaji wa ufisadi........................na kamwe asingekubali kujiunga na serikali ya JK ambaye inatuhumiwa kuingia madarakani kwa nguvu za ufisadi........................

Hivi serikali ya kifisadi yaweza kupambana na ufisadi.....................na sasa waanza kazi kwa kujinunulia mashangingi ya nguvu wakati magari ya zamani yapo na yanafanya kazi vizuri tu.........................Hizi ni dalili za serikali hii itakuwa ya wabadhirifu wakubwa..............Wahenga walinena dalili za mvua ni mawingu......

Mheshimiwa Sitta acha unafiki sisi twakuona undani wako.................
 
Huyu Sitta kwa watu wanaomfahamu ni mnafiki babu kubwa!! Kukubali kwake kuwa waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki, ndio mwisho wa heshima aliojijengea pale bungeni kama Sipika na pia inadhihilisha yale yaliyosemwa kuwa maamuzi yake mengi pale bungeni hayakuwa kwa sababu ya uamini wale[ principles] bali yalikuwa kuwathibiti wapinzani wake kisiasa; kama kweli angekuwa mtu mwenye msimamo asingekubali uwaziri aliopewa wakati yeye alikuwa kiongozi wa moja ya mihimili ya serikali ya jamhuri!!
 
That is very true.......................Sitta is not a principled leader...............................yupo pale kulinda masilahi yake tu..................na anatumia vita dhidi ya ufisadi kujipatia umaarufu wa bei poa kabisa...........
 
Yeye anadhani kina kikwete wamemsamehe jinsi alivyoruhusu mjadala wa richmond, hawajamsamehe na kikwete ndiye ana hasira zaidi dhidi yake ...mtaona na akiendeleza unafiki na njaa zake ATAKUFA...
 
Is there anyone ever claimed that 6 is a good leader?
Can somebody kindly tell me who is not Fisadi in CCM?

Sita got popularity because some Tanzanians are crazy! they applaused him forgetting that he is ONE OF THEM, no one is clean in CCM , I say so..

Where is 'your' mwakyembe, kilango etc?

Till when we gonna say 'some on ccm are clean and some are dirty' why these 'some' are together?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom