Giddy Mangi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 830
- 184
Tatizo la nchi za kiafrica ni kukumbatia wazee hata kama umri wao wa kufanya kazi umeshapitiliza mfano hai ni huyu babu Sitta
Tunachomtaka sita afanye ni kumtaja mtu/watu aliyesitiriwa na ile kamati. Sita hawezi kututaka tulaani tu, baada ya kulaani iweje??? Sita anakerwa na na wizi wa dowans wakati huohuo hataki kuweka siri za hili sakata wazi. Kama dowans wanafurahia sisi kumtaka sita awaumbue kwetu, basi kazi ipo.Sikatai kwamba labda Sita na wenzake wana personal interest katika hili, lakini akikaa kimya halafu hizo hela zikalipwa tutakuwa tumemkomoa nani, wala siyo Sita, bali kila mtanzania atasugua meno maana katika kuzilipa. Mimi nawahakikishia wenye DOWANS wanafurahi sana wakiona argument zenu, maana wanajua kumbe sasa tuna support.
Cha muhimu deni lisilipwe kwa sababu ni wazi hizo pesa tunatapeliwa, hata kichaa analijua hilo, na tusitegemee judicial system yetu itatusaidia katika hilo, tunachotakiwa ni kukomaa tu katika kukataa deni lisilipwe.
................ na yeye anajenga yake njombe !Hivi ofisi ya Spika Urambo anatumia Anna Makinda?
Sitta ni mwizi tu yeye! hana ubavu wowote au uwezo wa kufanya lolote! Kama kidume angejiunga na ccj...hahaha!
Nakuunga mkono. Pamoja na usanii na unafiki wa Sitta hastahili kushambuliwa katika kutetea Tanzania katika malipo haya (Shilingi bilioni 113) yaliyojaa ufisadi wa hali ya juu yanayotaka kufanywa dhidi ya kampuni hewa ya Dowans. Wako wapi hao Watanzania ndani ya chama ambao si wanafiki au wasanii wasimame hadharani kama alivyofanya Sitta kutoa kauli za kupinga malipo haya ya wizi wa mchana kweupe.
Watu hawajui kwamba kwa kumshambulia Sitta basi wananyamazisha sauti moja ya Mtanzania mwenzetu katika kutetea maslahi ya nchi. Inawezekana kabisa Sitta ni mwizi, msanii, mnafiki n.k. lakini katika hili la kupinga malipo yanayotaka kufanywa dhidi ya Dowans, Sitta hajakosea lolote na anastahili kuungwa mkono na Watanzania wote ambao ni wapenda haki na wako mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya nchi.
Sioni sababu yoyote ili ya kumnyamazisha Sitta na kuwarahisishia mafisadi kulipana shilingi 113 bilioni pesa ambayo hawakuitolea jasho kabisa, ikumbukwe mitambo ile inadaiwa imeshauzwa kwa Symbion kwa shilingi bilioni 120.
Kuikosoa CCM/Serikali si lazima uwe nje ya CCM, wako wanachama chungu nzima ndani ya CCM ambao wanaikosoa CCM/serikali na wengineo kati ya hao waliwahi kushika nyadhifa za juu ndani ya CCM na Serikali.
Makupa,
Issue hapa si umri.Kinachotakiwa ni HEKIMA.BUSARA na UTASHI wa kuwatumikia Watanzania/Wananchi.
Juzi kule Zambia wenzetu wamempa Bwana Michael Sata mwenye umri wa MIAKA 74 kuwa Rais wa Nchi(The highest office in the country) Watu wanaamini kuwa mtu anapokuwa mzee na busara zinaongezeka. Unaweza kuweka vijana kwenye uongozi na bado wakapwaya kama tunavyoona akina Ngeleja,Malima(Nishati/Madini),Januari Makamba(MB/M-kiti Kamati Nishati na Madini),Nape Nnauye K/Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Magamba-CCM.
Sitta ni mojawapo ya Wana-magamba ambaye anajitofautisha na mfumo mzima wa CCM. Tuliona vitu vyake wakti akiwa Spika wa Bunge lililopita. Hizi habari anazoongea ni UKWELI MTUPU.
Pengine mimi ningelipenda kumpa ushauri wa bure Mhe.Sitta kwamba anatakiwa KUJITOA CCM na kujiunga na upinzani hasa CHADEMA!