Sitta anasema jahanamu kuna sehemu ina moto mkali sana na hii imeandaliwa kwa ajili ya watu wanafiki. yeye anasema hakutegemea kama Lowassa angejiuzulu. Hivi ni kweli hakujua ama ni unafiki? Kuna maswali mengi kuhusu jinsi alivyoli-handle hili swala Bungeni, hivi ni kweli alikuwa na ugomvi na Lowassa na pengine ametuingiza kwenye hasara hii kwa kupika jungu ama kweli Lowassa alishiriki kwenye ufisadi? Hivi ni kweli kwamba Sitta alitumwa na JK aifupishe safari ya ENL kisiasa? Inasemekana huyu Mzee ni bingwa sana wa fitna, ukiunganisha na JK si inakuwa balaa kabisa hapo?
Hivi ni kweli huyu bwana anaamini kwa dhati katika kutetea wanyonge? Hii falsafa alianza kuitetea lini? Je anaishi maisha ya kutetea wanyonge.
Kuna fununu kuwa eti kuna watu wanamshawishi achukue Urais, je ni kweli atatufaa? Hivi akiwa Rais huyu si atawafunga akina Lowassa?
Ahsanteni,
Zul.