Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,024
- 59,685
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Sitta ajitosa mjadala wa posho [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 27 June 2011 09:13 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta
Lilian Lucas, Morogoro
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amejitosa kwenye mjadala wa posho ulioanza bungeni hivi karibuni akieleza kuwa suala la kujadili posho za wanasiasa na watendaji wengine linatakiwa kuanzia ngazi ya chini.
Alisema juzi katika mdahalo ulioandaliwa na Jumuia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa fedha nyingi zimekuwa zikipotea na hata wananchi wanapojaribu kuhoji hakuna maelezo yanayotolewa kwao na baadhi ya watendaji wa serikali zikiwamo za vijiji.
Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alisema kuwa malumbano yanayoendelea bungeni kuhusu posho za wabunge na watumishi wengine wa serikali hayana msingi na badala yake wanataaluma ndio wangetakiwa kulipwa vizuri tena kwa fedha nzuri kuliko wanasiasa.
Alisema kuwa wanataaluma wangepaswa kulipwa zaidi kuliko wanasiasa kutokana na kuwa wamehangaikia taaluma zao kwa miaka mingi kuliko wanasiasa, akieleza kuwa siasa ni kitu cha kujitolea.
"Sioni sababu ya wabunge kuendelea kujadiliana na kubishana juu ya suala hili la posho.
"Kinachotakiwa ni kumlipa vizuri mtu aliyehangaikia taaluma yake tena kwa muda mrefu, inafaa apewe mshahara mzuri kulingana na taaluma yake, lakini kwa nchi yetu wataalamu wanalipwa mishahara midogo ambayo haikidhi hata mahitaji yao ya msingi.
"Matokeo yake, wengi wakishamaliza elimu yao wanakimbilia nje ya nchi kufanya kazi au kugeukia siasa," alisema Sitta na kuongeza:
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuambia mdahalo huo wa kujadili masuala ya Jumuia ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Jumuia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa hali hiyo haina budi kubadilishwa.
"Inashangaza kuona fedha nyingi zinapotea kuanzia vijijini na watendaji wake wamekuwa wakijilipa na kufanyia mambo yao bila kushirikisha wananchi na hata kutowasomea mapato na matumizi ya kijiji husika bila ufuatiliaji na wala hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika,"alisema.
Pia, aliwataka wananchi hususani vijana kuwa wawajibikaji zaidi na kuweka uzito katika mambo ya msingi ya taifa na kuhakikisha wanakemea wala rushwa na wale wanaojitajirisha kwa maslahi yao na kuwanyonya watu wa hali ya chini.
Alisema ndani ya Serikali ya Tanzania kuna tatizo la uwajibikaji na watumishi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kujisahau kuwa wanatakiwa kuwahudumia wananchi katika masuala ya kimaendeleo.
Kwa upande wao, wanafunzi walishiriki mdahalo huo walihoji ni jinsi gani wananchi wa Tanzania walivyoandaliwa katika kuleta ushindani katika Jumuia ya Afrika Mashariki kwani kila mara wameonekana kuwa nyuma katika ajira kwenye jumuia hiyo.
"Katika hili, wanasiasa wameonekana kuwa ndio wanaoharibu mfumo mzima kutokana na kuweka siasa zaidi mbele badala ya kutenda kazi ya kushirikisha wananchi hasa wa hali ya chini,"alisema Christian Makala, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Kitivo cha Sheria.
Alisema wanasiasa wengi wanapokuwa majukwaani hasa wakati wa kuomba kura wanaonekana wazalendo, lakini pindi wanapopata madaraka ikiwamo kuingia bungeni hubadilika na kujisahau na kukubaliana na mambo kwa maslahi ya vyama vyao[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alisema kuwa malumbano yanayoendelea bungeni kuhusu posho za wabunge na watumishi wengine wa serikali hayana msingi ....................................
Mbona Sitta kama bado haweka wazi msimamo wake juu ya posho za Wabunge!
Amezunguka zunguka tuu.
umejibiwa-----wana magamba wampe jamaa ajaribu upreda, ni mara mia yake kuliko yeyote humo CCM sio waziri mkuu huyu wa ajabu kabisa
hongera sitta umejivua gamba kiuraini katika ili safi sawa
Hivi sio huyu Jamaa aliyeongeza mishahara na POSHO maradufu....., kweli ukistaajubu ya Ngereja utaona ya Sitta...
toka zamani nilisha sema huyu mzee sina imani ne....na kwa kuupotezea mjadala wa richmond sitamsamehe maisha....hakuna zee nafiki kama hili
umejibiwa
---manashindwa kuhukumu watu ka CHEYO siku hiyo ya mjadala wa posho alikuwa wanaupigia debe kama ana akili nzuri.
kwa mfumo wa bunge wa sasa huwezi kumlaumu SITTA watu wamekuja na hoja ya kuongezewa posho na kura wamepiga hoja ikapita sasa yeye hafanyeje na spika hatakiwi kuwa na upendeleo.
---- wake wa uspika wake DR SLAA mzee wa ukweli alikuwa kinara wa hoja bungeni kwa sababu hakuwa na hupendeleo,
hapana kuna wakati hunapaswa kuwakubali baadhi ya wana magamba, UNAFIKI huo manaosema tukipima vizuri ni mbinu ya kila mwana siasa kila vita lazima inafika wakati unarudi nyuma sio kusonga tu unaweza kujikuta kwenye mitego.
he is playing very well ,
NITAJIENI MWANSIASA DUNIANI AMBAYE SIO MNAFIKI
Na ile ofisi ya Spika kujengwa kule Urambo je kuna bunge kule Urambo? au Uspika ni cheo cha kudumu? Hongera sana Mapacha watatu kwa kutuondela huyu msanii, kwani sisi tunahitaji Spika na sio mshehereshaji ( mc )
Sitta ndiye chanzo cha posho batili za wabunge, atuambie alipokuwa Spika alisaidiaje kuboresha maslahi ya wanataaluma.
Na ile ofisi ya Spika kujengwa kule Urambo je kuna bunge kule Urambo? au Uspika ni cheo cha kudumu? Hongera sana Mapacha watatu kwa kutuondela huyu msanii, kwani sisi tunahitaji Spika na sio mshehereshaji ( mc )
Hivi huyu mtu alishawahi kutoa maelezo kuhusu ile Ofisi ya Spika wa Bunge aliyoijenga Jimboni kwake?
Matola
hiyo kitu hata mimi nimewahi kuisikia lakini je hiyo hapa hapo chini umewahi kuiona pia nadhani.
ili habari yawezekana ilikuwa na makosa yawezekana ile ni offisi ya MBUNGE wa urambo
hii ni issue ya comon sense tu
kila mtu anajua haiwezekana SITTA akawa spika kwa maisha
halafu mbona hizo offisi zijengwe mbili kama mwaka mmoja urambo na DODOMA
watanzania tujifunzi utafiti wa habari na ukweli wa mambo la sivyo hii nchi itabaki hapa au kudidimia
ni sisi wananchi ndi tutaikombo nchi sio wanasiasa wao wako kazi
kama tusipo waiga wazungu kwa kutokuwa mashabiki wa vyama tumeliwa
kila mtu apewe CREDIT pale anapofanya kwa ufanisi
[h=1]Mhe. Anna Makinda atembelea ujenzi wa makazi ya Spika mjini Dodoma[/h]BY DULLONET TANZANIA – DECEMBER 27, 2010POSTED IN: HABARI KUU
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika yanayojengwa Dodoma kutoka Maafisa wa Bunge pamoja na wakandarasi kutoka Wakala wa Ujenzi (TBA). Kulia kwake ni Afisa Tawala wa Bunge, Athumani Kwikima
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika yanayojengwa Dodoma kutoka mtunza vifaa wa kampuni inayosimamia ujenzi huo mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akielekeza jambo mara baada ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika yanayojengwa Dodoma jana. walioambatana nae ni maafisa toka Ofisi ya Bunge, wakala wa Ujenzi na wakandarasi wa Kampuni inayojenga jengo hilo.
Jengo la Makazi ya Spika linavyoonekana kwa sasa.(Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)
Na ile ofisi ya Spika kujengwa kule Urambo je kuna bunge kule Urambo? au Uspika ni cheo cha kudumu? Hongera sana Mapacha watatu kwa kutuondela huyu msanii, kwani sisi tunahitaji Spika na sio mshehereshaji ( mc )