Sitta afunguka kuhusu Bandari

Sitta afunguka kuhusu Bandari

Jamanii umesahau quotena comment ulizokuwa ukipayuka na kufoka all around ati oooh wezi sijui nini...Sasa ushasahau !!
Kwanza,
Huwa sipayuki hata siku moja haswa kwenye mambo ya msingi. Ukiona naongelea kitu Ujue nina taarifa husika. Hao " Wezi" niliokuwa napayuka kwa mujibu wako ni kina nani!?
 
Ana hoja nzito. Kwa ukweli kukurupuka kuna adha na kiwango fulani cha kusigina haki.

Jinsi ya kuwarudishia angalau haki na utu wao walioathirika ni vigumu.

Ni sawa na kuvua nguo wakati wa kuoga mtoni halafu kichaa akakimbia na nguo zako.
Sina haja hata ya kusoma yote yaani bodi imeundwa isimamie tpa alafu madudu yote yanayofanyika wao kimya aiseeee kweli 6 anazeeka vibaya si atulie tu aaaah.





huyu mzee kachoka anajipendekeza
 
Huyu mzee kama alisha wahi kuchomwa sindano ya ganzi basi dose ilikuwa kubwa sana ndio maana imeenda mpaka kuweka ganzi kwenye ubongo, uwe waziri kamili wa wizara ya uchukuzi uache ushenzi huu unaoibuliwa halafu ujitokeze kuutetea ni zaidi ya mwendawazimu. Atulie aangalie kama hawezi ainamishe kichwa chini asione uchafu wake ukiwekwa hadharani, hii ni aibu kwake bora angefumaniwa na mtoto wa shule umri huu alionao kuliko haya, na alikuwa anajitanabaisha ndie mpinga ufisadi, pumbavu.
 
Huyu mzee haoni hata aibu kwa jinsi alivyoichafua katiba ya wananchi ambayo ingekomesha ufisadi, atuombe msamaha kwanza sisi watanzania


Wakati mwingine tuwe wakweli, tusiandike humu kwa kufuata mkumbo wa wanasiasa. Hiyo katiba mpya ingekomesha vipi ufisadi?
 
Usipoteze muda wako bure kumwamini MNAFIKI!
Yaani huyu mzee ni MNAFIKI kweli kweli, wakati anazurura na Mwakyembe makanisani kutangaza amepewa sumu, na akawa ndio msemaji wa Mwakuyembe kwenye vyombo vya habari nilimtoa maanani kabisa, alikuwa anapayuka utafikiri yeye ni mke wa Mwakyembe, hovyo kweli kweli.
 
Huyu Six angetulia tu ale pensheni yake.
Katuvurugia katiba yetu leo anakuja na hoja za kujipenyeza penyeza, hovyo sana hili zee
 
Yan kati ya watu wasio na uchung na hii nchi ni huyu mzee sita. Nimeshangazwa sana na utetezi wake ambao hauna mantiki yoyote.kama bodi aliyoivunja yy aliona INA makosa kwa nn hakuichukulia hatua stahiki????? Kama pini ya kutumbulia najipu imemgusa huko bandari atulie tu hamna namna nyingine anaweza sikilizwa!!!!!! Huo ushaur wake alitakiwa autoe kipund akiwa serikalin yamkin angesikilizwa kwa huo uongo wake but now its too late
 
Ma
Huyu mzee haoni hata aibu kwa jinsi alivyoichafua katiba ya wananchi ambayo ingekomesha ufisadi, atuombe msamaha kwanza sisi watanzania
Machozi ya mamba! Mbona hiyo bodi na menejimenti mpya haijatuambia tatizo hata moja walilolikuta? Sitta mwenyewe alikuwa mbadhaifu kwa hiyo hana haki ya kutoa maoni sasa. Zile posho za bunge la katiba hazikuwa halali kwani hiyo katiba pendekezwa haitapata kwenye kura ya maoni.
 
Ni kwanini mzee Sita asingetenda kama waziri mkuu. Alikuwa anagwaya nini directly hapa anaonyesha yeye alikuwa.hana self initiatives za kujua kwa undani na kuchukua hatua.
Hizi habari bodi ilikutana mara moja walikuwa kwenye mchakato,wangeunda taskforce haya mabo yamepitwa na wakati. Hii dunia ya sasa si ya kupoteza muda chujua hatua haraka.
 
atulie kama naye yumo atatajwa tu na kama hausiki itajulikana mahakamani
 
Ameongea vizuri,ila tukumbuke JPM Na MKM ni binadam,mambo yameharibika ndani ya hii nchi kiasi kwamba wao wawili pengine hata hawajui waanzie wapi,kwa hiyo katika mazingira ya kawaida ni lazima uvunje utawala uliopo ili uanze upya!
Nilazima tukubali katika kila jambo zuri kwa wengi lazima sucrifice ya wachache ipatikane.kanyaga twende JPM.

QUOTE="Mumba Daly, post: 15356783, member: 230839"]MWANASIASA mashuhuri na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta, ameandika barua kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kueleza kuhusu mtazamo wake wa utumbuaji majipu katika Mamlaka ya Bandari za Tanzania (TPA), Raia Mwema limeambiwa.

Katika barua hiyo, Sitta ambaye alikuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne ameeleza kuwa ni vema serikali ikachunguza zaidi kuhusu Bodi ya Wakurugenzi ya TPA iliyovunjwa pamoja na menejimenti yake; kwa maelezo kwamba hawakuwa wakihusika na matatizo yaliyokuwepo kabla yao.

Katika mazungumzo yake na gazeti hili wiki hii, Sitta amesema kwamba yeye anaunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli na serikali yake; lakini anaamini kwamba kwa ujasiri uleule wa kutumbua majipu, serikali pia inapaswa kukubali kurejea maamuzi yake, pale inapobaini kuwa ilifanya makosa.

“ Katika barua yangu kwa Waziri Mkuu, kwa mfano, nimemueleza kwamba ile bodi ya TPA iliyovunjwa ilikuwa imefanya mkutano wake mara moja tu tangu iteuliwe. Kwa vyovyote vile, haiwezi kuwa inahusika na makosa yaliyotokea kabla yenyewe haijateuliwa.

“ Hivi sasa serikali ya Magufuli imebaini mianya kadhaa ya ukwepaji kodi kupitia bandari kavu yaani ICD lakini ukichunguza kwa makini, utaona kwamba ni menejimenti mpya ya TPA iliyoteuliwa ndiyo iliyofanya kazi ya kubaini mapungufu hayo. Sasa watu kama hawa, kwa maana ya bodi na menejimenti wanapoitwa majipu, inaumiza kwa kweli.

“ Kuna wanataaluma na watu ambao walikuwa wamejitolea, pamoja na vitisho na mazingira mengine magumu ya kazi, kuwa wazalendo na kutetea mali ya taifa. Hawa watu, kama wamekosea, sawa, lakini kama wamekaa kwenye bodi kwa kufanya kikao kimoja tu na baadaye kufukuzwa kwa namna ile, nadhani kuna haja ya kutazama haya mambo,” alisema Sitta ambaye sasa ametangaza kustaafu siasa.

Katika mazungumzo hayo, Sitta alisema anafahamu kuwa nia na dhamira ya serikali katika kupambana na ufisadi ni thabiti lakini yeye ametoa mawazo yake hayo kwa sababu ni mtu anayefahamu mazingira ya TPA na alihusika na uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo.

“Kuliko mtu mwingine yeyote, mimi nafahamu mazingira yaliyokuwepo pale TPA kabla ya bodi ile kuundwa. Mimi ndiye niliyevunja bodi iliyokuwepo na kuunda bodi mpya. Ninafahamu kuwa ilikutana mara moja tu, mwezi Oktoba na miezi miwili baadaye ndiyo imetangaza kuvunjwa.

“ Nyingi ya tuhuma zilizopo sasa kuhusu TPA na mambo mengine zilitokea kabla ya bodi ile kuundwa. Mimi ndiyo niliwaomba wale watu waje kusaidia kama wajumbe wa bodi. Sasa, kama mimi nisipojitokeza na kusema ninachokijua, huenda serikali isipate maelezo halisi. Ndiyo sababu nikaandika barua ile kwa Waziri Mkuu ambaye nafahamu amekuwa akifuatilia masuala ya bandari kwa karibu,” alisema.

Alisema utetezi wake kuhusu menejimenti unafanana na ule wa bodi kwa sababu ni menejimenti hiyo ndiyo iliyochunguza na kubaini matatizo –yaliyokuja kuwa sehemu ya ripoti aliyokabidhiwa Majaliwa kuhusu TPA na ambayo ndiyo inafanyiwa kazi na serikali hivi sasa.

Rais Magufuli alitangaza uamuzi wa kuvunja bodi ya TPA, menejimenti pamoja na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka. Uamuzi huo ulitangazwa na Majaliwa baada ya kufanya ziara bandarini mwezi Desemba mwaka jana.

Waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo ni Dk. Tulia Akson - Mhadhiri Mwandamizi, ambaye sasa ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Injinia Mussa Ally Nyamsigwa, Donata S Mugassa,

Haruna Masebu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa EWURA, Injinia Gema Modu, Dk. Francis Michael ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Crescentius Magori ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango (NSSF) na Flavian Kinunda Mkurugenziwa Masoko Mstaafu, Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Joseph Msambichaka, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo mwezi Januari, mwaka 2013, akichukua nafasi ya Raphael Mollel, ambaye uteuzi wake ulikuwa umetenguliwa.

Menejimenti ambayo uteuzi wake umetenguliwa na Magufuli ilianza kazi Januari mwaka jana, kwa Awadh Massawe kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, akichukua nafasi ya Madeni Kipande.

Akizungumzia siku 100 za Magufuli, Sitta alisema amebaini ni kiongozi anayekwenda kwa kasi na viwango ambavyo yeye alitamani rais wa Awamu ya Tano awe navyo, na akatoa wito kwa Watanzania kumuombea kiongozi huyo ili atomize ndoto zake za kuondoa kero za wananchi.

Sitta alisema anafahamu kuwa kuna vikwazo na vitisho mbalimbali ambavyo Magufuli atapitia katika kutekeleza majukumu yake na akamtaka asiwe muoga na awe jasiri kwani Watanzania wote wako nyuma yake.

“Ombi langu kubwa kwa wasaidizi wake ni kuwa nao wanatakiwa waende na kasi yake. Nashukuru kuwa nimeona mawaziri wake wakitembelea sehemu na maeneo ambako kuna kero za wananchi. Huu ni mwanzo mzuri kwani wakimuacha peke yake, inaweza kuonekana kuwa wanapea,” alisema Sitta[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom