Sitta afunguka kuhusu Bandari

Ana hoja nzito. Kwa ukweli kukurupuka kuna adha na kiwango fulani cha kusigina haki.

Jinsi ya kuwarudishia angalau haki na utu wao walioathirika ni vigumu.

Ni sawa na kuvua nguo wakati wa kuoga mtoni halafu kichaa akakimbia na nguo zako.
 
Hakuzungumzia kale kajumba ka spika kule Urambo? na amekwisha hama kwenye nyumba ya spika kweli huyu ndugu yangu?
 
Sitta kwa nini hutaki kupumzika?umesahau nini ujanani?kama madudu yalitokea kabla,wewe hukuyajua?hatua gani ulichukua?
 
Kaa kimya asee, kila kitu kilikuwa upande wako enzi hizo ukapotezea. Pilau iko kwa jirani wewe unakatakata kachumbari nani kakuomba ufanye hayo?
 
Hata kama hawahusiki kwani rais hawezi kuvunja na kuwekawatu anaowaone yeye ni sahihi.
 
MWANASIASA mashuhuri na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta, ameandika barua kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kueleza kuhusu mtazamo wake wa utumbuaji majipu katika Mamlaka ya Bandari za Tanzania (TPA), Raia Mwema limeambiwa.
Katika barua hiyo, Sitta ambaye alikuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne ameeleza kuwa ni vema serikali ikachunguza zaidi kuhusu Bodi ya Wakurugenzi ya TPA iliyovunjwa pamoja na menejimenti yake; kwa maelezo kwamba hawakuwa wakihusika na matatizo yaliyokuwepo kabla yao.

Katika mazungumzo yake na gazeti hili wiki hii, Sitta amesema kwamba yeye anaunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli na serikali yake; lakini anaamini kwamba kwa ujasiri uleule wa kutumbua majipu, serikali pia inapaswa kukubali kurejea maamuzi yake, pale inapobaini kuwa ilifanya makosa.

“ Katika barua yangu kwa Waziri Mkuu, kwa mfano, nimemueleza kwamba ile bodi ya TPA iliyovunjwa ilikuwa imefanya mkutano wake mara moja tu tangu iteuliwe. Kwa vyovyote vile, haiwezi kuwa inahusika na makosa yaliyotokea kabla yenyewe haijateuliwa.

“ Hivi sasa serikali ya Magufuli imebaini mianya kadhaa ya ukwepaji kodi kupitia bandari kavu yaani ICD lakini ukichunguza kwa makini, utaona kwamba ni menejimenti mpya ya TPA iliyoteuliwa ndiyo iliyofanya kazi ya kubaini mapungufu hayo. Sasa watu kama hawa, kwa maana ya bodi na menejimenti wanapoitwa majipu, inaumiza kwa kweli.

“ Kuna wanataaluma na watu ambao walikuwa wamejitolea, pamoja na vitisho na mazingira mengine magumu ya kazi, kuwa wazalendo na kutetea mali ya taifa. Hawa watu, kama wamekosea, sawa, lakini kama wamekaa kwenye bodi kwa kufanya kikao kimoja tu na baadaye kufukuzwa kwa namna ile, nadhani kuna haja ya kutazama haya mambo,” alisema Sitta ambaye sasa ametangaza kustaafu siasa.

Katika mazungumzo hayo, Sitta alisema anafahamu kuwa nia na dhamira ya serikali katika kupambana na ufisadi ni thabiti lakini yeye ametoa mawazo yake hayo kwa sababu ni mtu anayefahamu mazingira ya TPA na alihusika na uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo.

“Kuliko mtu mwingine yeyote, mimi nafahamu mazingira yaliyokuwepo pale TPA kabla ya bodi ile kuundwa. Mimi ndiye niliyevunja bodi iliyokuwepo na kuunda bodi mpya. Ninafahamu kuwa ilikutana mara moja tu, mwezi Oktoba na miezi miwili baadaye ndiyo imetangaza kuvunjwa.

“ Nyingi ya tuhuma zilizopo sasa kuhusu TPA na mambo mengine zilitokea kabla ya bodi ile kuundwa. Mimi ndiyo niliwaomba wale watu waje kusaidia kama wajumbe wa bodi. Sasa, kama mimi nisipojitokeza na kusema ninachokijua, huenda serikali isipate maelezo halisi. Ndiyo sababu nikaandika barua ile kwa Waziri Mkuu ambaye nafahamu amekuwa akifuatilia masuala ya bandari kwa karibu,” alisema.

Alisema utetezi wake kuhusu menejimenti unafanana na ule wa bodi kwa sababu ni menejimenti hiyo ndiyo iliyochunguza na kubaini matatizo –yaliyokuja kuwa sehemu ya ripoti aliyokabidhiwa Majaliwa kuhusu TPA na ambayo ndiyo inafanyiwa kazi na serikali hivi sasa.

Rais Magufuli alitangaza uamuzi wa kuvunja bodi ya TPA, menejimenti pamoja na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka. Uamuzi huo ulitangazwa na Majaliwa baada ya kufanya ziara bandarini mwezi Desemba mwaka jana.

Waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo ni Dk. Tulia Akson - Mhadhiri Mwandamizi, ambaye sasa ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Injinia Mussa Ally Nyamsigwa, Donata S Mugassa,

Haruna Masebu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa EWURA, Injinia Gema Modu, Dk. Francis Michael ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Crescentius Magori ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango (NSSF) na Flavian Kinunda Mkurugenziwa Masoko Mstaafu, Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Joseph Msambichaka, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo mwezi Januari, mwaka 2013, akichukua nafasi ya Raphael Mollel, ambaye uteuzi wake ulikuwa umetenguliwa.

Menejimenti ambayo uteuzi wake umetenguliwa na Magufuli ilianza kazi Januari mwaka jana, kwa Awadh Massawe kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, akichukua nafasi ya Madeni Kipande.

Akizungumzia siku 100 za Magufuli, Sitta alisema amebaini ni kiongozi anayekwenda kwa kasi na viwango ambavyo yeye alitamani rais wa Awamu ya Tano awe navyo, na akatoa wito kwa Watanzania kumuombea kiongozi huyo ili atomize ndoto zake za kuondoa kero za wananchi.

Sitta alisema anafahamu kuwa kuna vikwazo na vitisho mbalimbali ambavyo Magufuli atapitia katika kutekeleza majukumu yake na akamtaka asiwe muoga na awe jasiri kwani Watanzania wote wako nyuma yake.

“Ombi langu kubwa kwa wasaidizi wake ni kuwa nao wanatakiwa waende na kasi yake. Nashukuru kuwa nimeona mawaziri wake wakitembelea sehemu na maeneo ambako kuna kero za wananchi. Huu ni mwanzo mzuri kwani wakimuacha peke yake, inaweza kuonekana kuwa wanapea,” alisema Sitta
Ametoa maelekezo yake na maoni yake jinsi ilivyokuwa na ni muhimu yakaheshimiwa
 
kwa mara ya mwisho nakuunga mkono samuel kwenye hili , ila bifu la kututapeli richmond na katiba mpya liko palepale .
 
Sina haja hata ya kusoma yote yaani bodi imeundwa isimamie tpa alafu madudu yote yanayofanyika wao kimya aiseeee kweli 6 anazeeka vibaya si atulie tu aaaah.
 
Back
Top Bottom