Sitta afunguka kuhusu Bandari

Sitta afunguka kuhusu Bandari

Mara anasema anapumzika siasa mara tena ameanza kumwandikia Majaliwa barua kutaka kuwatetea watu aliowateua yeye kwa kuwaondoa wa Mwakyembe ili wamtafutie ngawira ya kuusakia urais.

Nadhani huyu mzee mboko za baba wa taifa akiwa UDSM zilimtia wazimu, katiba ya watanzania milioni 45 aliipuuza akaitia najisi leo analeta habari ya bodi ya watu kumi aliojifungia akawateua akisaidiana na mwalimu Magreti.

Kapumzike kwenye hilo jumba lako la spika bila uspika usubiri na wewe kutumbuliwa kwa kutumia madaraka yako vibaya.

Kwanza umenikumbusha nikuulize, kwenye ile nyumba ya spika uliyokuwa unaing'ang'ania kule Dar umeishahamako?
 
Imenishangaza sana Mr six kuingilia zama hizi za utawala mpya,better stay cool and watch how men work! bana....!
 
Hakuzungumzia kale kajumba ka spika kule Urambo? na amekwisha hama kwenye nyumba ya spika kweli huyu ndugu yangu?

Nadhani bado atakuwa huko huko kwenye nyumba ya serikali ilyotengwa kwa ajili ya spika wa jamhuri. Tena wasipomwahi atakuwa alishajiuzia kinguvu hiyo nyumba. Wazri unaehusika na majengo ya serikali chukua hatua haraka au tukulilie kwa Magufuli au waziri mkuu uone moto utakaokuwakia.Nina hakika huyu mzee atakuwa na nyumba zake nyingi tu Dar na ahamie huko haraka.
 
Tuliposema hii serikali itaumbuka kuna watu walibisha haya sasa watu wameanza kufunguka.

Niligusia pia "agenda za kisiasa" na "political infuence" na hapa ni dhahiri mojawapo itahusika.

Huu ni mwanzo tu.Tusubiri.
 
Mleta mada siku ingine ukileta mada tafadhali hakikisha imekamilika. Si kila mtu anajua kinachoendelea
 
raha sana kuona watu kama Sitta wanalalama hivi.

tafsiri ni.....wanaisoma namba!

kiaina!
 
why did they keep quiet? by the way for how long was he a minister there?

What about Mwakyembe?
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mzee Stta amekamatwa PABAYA.
Utetezi wa Sitta ni dhaifu sana. Ni mwasheria aliyekwajuka. Suala la msingi ni kuchukua hatua(to take action against the vice), siyo kujua tatizo. SITTA na utawala wake walijua tatizo, LAKINI hawakuchukua hatua ili kulinda mali za taifa. Udhaifu wa kutochukua hatua ni prima facie case kuwa Sitta na kundi lake WALIUNGA MKONO UFISADI HUO KWA SABABU WALINUFAIKA NAO. Sitta ni JIPU. We want actions not words. Magufuli/Majaliwa go on. Achana na kelele za vibaka hawa walionufaika na utwala wao wa kifisadi.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
MWANASIASA mashuhuri na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta, ameandika barua kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kueleza kuhusu mtazamo wake wa utumbuaji majipu katika Mamlaka ya Bandari za Tanzania (TPA), Raia Mwema limeambiwa.

Katika barua hiyo, Sitta ambaye alikuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne ameeleza kuwa ni vema serikali ikachunguza zaidi kuhusu Bodi ya Wakurugenzi ya TPA iliyovunjwa pamoja na menejimenti yake; kwa maelezo kwamba hawakuwa wakihusika na matatizo yaliyokuwepo kabla yao.

Katika mazungumzo yake na gazeti hili wiki hii, Sitta amesema kwamba yeye anaunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli na serikali yake; lakini anaamini kwamba kwa ujasiri uleule wa kutumbua majipu, serikali pia inapaswa kukubali kurejea maamuzi yake, pale inapobaini kuwa ilifanya makosa.

“ Katika barua yangu kwa Waziri Mkuu, kwa mfano, nimemueleza kwamba ile bodi ya TPA iliyovunjwa ilikuwa imefanya mkutano wake mara moja tu tangu iteuliwe. Kwa vyovyote vile, haiwezi kuwa inahusika na makosa yaliyotokea kabla yenyewe haijateuliwa.

“ Hivi sasa serikali ya Magufuli imebaini mianya kadhaa ya ukwepaji kodi kupitia bandari kavu yaani ICD lakini ukichunguza kwa makini, utaona kwamba ni menejimenti mpya ya TPA iliyoteuliwa ndiyo iliyofanya kazi ya kubaini mapungufu hayo. Sasa watu kama hawa, kwa maana ya bodi na menejimenti wanapoitwa majipu, inaumiza kwa kweli.

“ Kuna wanataaluma na watu ambao walikuwa wamejitolea, pamoja na vitisho na mazingira mengine magumu ya kazi, kuwa wazalendo na kutetea mali ya taifa. Hawa watu, kama wamekosea, sawa, lakini kama wamekaa kwenye bodi kwa kufanya kikao kimoja tu na baadaye kufukuzwa kwa namna ile, nadhani kuna haja ya kutazama haya mambo,” alisema Sitta ambaye sasa ametangaza kustaafu siasa.

Katika mazungumzo hayo, Sitta alisema anafahamu kuwa nia na dhamira ya serikali katika kupambana na ufisadi ni thabiti lakini yeye ametoa mawazo yake hayo kwa sababu ni mtu anayefahamu mazingira ya TPA na alihusika na uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo.

“Kuliko mtu mwingine yeyote, mimi nafahamu mazingira yaliyokuwepo pale TPA kabla ya bodi ile kuundwa. Mimi ndiye niliyevunja bodi iliyokuwepo na kuunda bodi mpya. Ninafahamu kuwa ilikutana mara moja tu, mwezi Oktoba na miezi miwili baadaye ndiyo imetangaza kuvunjwa.

“ Nyingi ya tuhuma zilizopo sasa kuhusu TPA na mambo mengine zilitokea kabla ya bodi ile kuundwa. Mimi ndiyo niliwaomba wale watu waje kusaidia kama wajumbe wa bodi. Sasa, kama mimi nisipojitokeza na kusema ninachokijua, huenda serikali isipate maelezo halisi. Ndiyo sababu nikaandika barua ile kwa Waziri Mkuu ambaye nafahamu amekuwa akifuatilia masuala ya bandari kwa karibu,” alisema.

Alisema utetezi wake kuhusu menejimenti unafanana na ule wa bodi kwa sababu ni menejimenti hiyo ndiyo iliyochunguza na kubaini matatizo –yaliyokuja kuwa sehemu ya ripoti aliyokabidhiwa Majaliwa kuhusu TPA na ambayo ndiyo inafanyiwa kazi na serikali hivi sasa.

Rais Magufuli alitangaza uamuzi wa kuvunja bodi ya TPA, menejimenti pamoja na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka. Uamuzi huo ulitangazwa na Majaliwa baada ya kufanya ziara bandarini mwezi Desemba mwaka jana.

Waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo ni Dk. Tulia Akson - Mhadhiri Mwandamizi, ambaye sasa ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Injinia Mussa Ally Nyamsigwa, Donata S Mugassa,

Haruna Masebu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa EWURA, Injinia Gema Modu, Dk. Francis Michael ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Crescentius Magori ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango (NSSF) na Flavian Kinunda Mkurugenziwa Masoko Mstaafu, Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Joseph Msambichaka, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo mwezi Januari, mwaka 2013, akichukua nafasi ya Raphael Mollel, ambaye uteuzi wake ulikuwa umetenguliwa.

Menejimenti ambayo uteuzi wake umetenguliwa na Magufuli ilianza kazi Januari mwaka jana, kwa Awadh Massawe kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, akichukua nafasi ya Madeni Kipande.

Akizungumzia siku 100 za Magufuli, Sitta alisema amebaini ni kiongozi anayekwenda kwa kasi na viwango ambavyo yeye alitamani rais wa Awamu ya Tano awe navyo, na akatoa wito kwa Watanzania kumuombea kiongozi huyo ili atomize ndoto zake za kuondoa kero za wananchi.

Sitta alisema anafahamu kuwa kuna vikwazo na vitisho mbalimbali ambavyo Magufuli atapitia katika kutekeleza majukumu yake na akamtaka asiwe muoga na awe jasiri kwani Watanzania wote wako nyuma yake.

“Ombi langu kubwa kwa wasaidizi wake ni kuwa nao wanatakiwa waende na kasi yake. Nashukuru kuwa nimeona mawaziri wake wakitembelea sehemu na maeneo ambako kuna kero za wananchi. Huu ni mwanzo mzuri kwani wakimuacha peke yake, inaweza kuonekana kuwa wanapea,” alisema Sitta
Six ni mpuuzi mwili mzima; baada ya kuvuruga mchakato wa katiba mpya KIHUNI na kwa KUCHAKACHUA; hakuna hata moja analoweza kusema watu makini wakamsikiliza; hakuna! Likafie mbali huko limwachwe JPM aplay part yake jinsi anavyajua yeye wao walikumbatia uozo now their time is gone watulie wasubiri kunyolewa if necessary!
 
hili zee jizi limefumukia wapi tena..he is trying to raise his ugly head again,..mtu mmoja atuwekee picha yake na yule dogo mwizi wa hsc wakiwa ndani ya business class...
 
Ametoa maelekezo yake na maoni yake jinsi ilivyokuwa na ni muhimu yakaheshimiwa
Kuheshimu maoni ya mtu kama sitta ni sawa na kuzipumzisha akili kwa muda na kujifanya hayawani; Sita hafai hata kidogo
 
Back
Top Bottom