Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,651
- 5,989
Dah imebidi nisome visa vya wenzangu nicheke. Ilikuta miaka kadhaa iliyopita wakati nimemaliza six nimetafuta sana tempo shule za sekondari nikakosa nikaamua kutulia kitaa nawaza ntatokaje huku nikisubiri matokeo ya mitihani. Ndipo nikakuta tangazo classified (matangazo madogo madogo, yanakuwa mengi kwenye page 1) kwenye gazeti sikumbuki jina.
Nikapiga simu ikapokelewa nikaambiwa kesho niende ofisini Magomeni kati ya Mapipa au Usalama ila ni maeneo hayo hayo karibu na Magomeni Mikumi. Mimi huwa sikeep bad memories in details. Kufika nikaonana na vijana wenzangu wakaka na wadada. Picha linaanza unapewa mtihani wa interview vimaswali na hesabu za kiboya wakati mi ndo nimetoka kupiga EGM yangu a few days ago.
After kama nusu saa hivi majibu yakatoka. Tukawa tunaitwa mmoja mmoja....mtu akiingia huko ndani ofisini kwa boss harudi. Zamu yangu ikafika. Lakini wakati wote nilikua nasikia kelele za watu kama vile wanapasha misuli au wanacheza karate nyuma ya nyumba huko. Nikajiuliza maswali bila majibu, watu hao wanafanya nini.
Nilipofika ndani kwa boss akaniambia hongera sana umefaulu kwa 95% na hivyo kazi umepata. Pembeni kuja jamaa kachoka choka....shati limepauka, kiatu kimelika soli kinyama na suruali yake nyeusi na bonge la tai. Akaambiwa utaenda naye huyu (mimi) umpe maelekezo leo siku nzima nami nikaambiwa niwe msikivu kwa mkufunzi wangu. Tukatoka, hapo sijahoji chochote zaidi ya kuitikia maelekezo. Jamaa akanitoa kupitia mlango mwingine nikakuta majagi, mabeseni, viti vya kukaa watoto ku poop, makontena na vikorokoro vingine vya plastic. Jamaa akabeba kadhaa akanipa namimi nibebe viti vile vya watoto...safari ikaanza. Akaniambia tunaenda Mabibo.
Tukapanda daladala mpaka Mabibo. Tulivyoshuka tukaanza kuingia mtaani, nakumbuka ni maeneo yale ya chuo cha NIT. Tukazunguka hukoo mitaani tunauza, tukiona watu wamekaa hasa wamama tunawaface. Moyoni nlikua nawaza tu nsije kutana na mtu anayenifahamu....aibu yake ingekuwa kubwa sana. Sijui ningeificha wapi sura yangu. Maana nimechoka, nna njaa, nimeloa jasho, kiatu kina vumbi balaa. Yule jamaa alinitembeza kutwa hatukula kitu. Tuliuza vitu vichache tu.
Tukapanda daladala tukarudi ofisini jioni saa 11. Wakaniambia hongera sana mmefanya kazi nzuri na mwanzo mzuri. Inabidi uende nyumbani uje kesho, ila kesho uje na tai.
Nilivyotoka pale nikasepa home nikaapa kutorudia tena. Kuna mwana tulikua naye, tuliexchange namba wakati tunasubiri majibu ya usaili yeye walienda Kinondoni huko. Jioni tulivyopigiana simu tukacheka sana. Jamaa alicheka sana kwenye simu dah.
Mwaka jana nikiwa na majukumu yangu kikazi nikapita ile mitaa ya NIT mtaa ule ule tulioanza kutembeza vile vitu, nilivyopark tu na kushuka niliduwaa kama sekunde 30 hivi nikasikitika peke yangu.
Mungu ni mwema, maisha yanasonga.