SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,270
Habari zenu waungwana wa Chit chat,
Leo naomba niwaeleze hisia zangu jinsi mjanja fulani alivyoniingizwa choo cha kike hapa jf.Baada ya kujiunga na jf mwezi desemba 2011,nikitumia id ya HYGEIA niliendelea kusoma na kuchangia kwenye majukwaa mbalimbali.Kwenye jukwaa la mmu, ziltokeza thread zilizonifurahisha sana nikajikuta nampenda sana mleta thread.Mleta thread alikuwa na avatar ya picha ya kike na id ya utata kiasi.
Id yake ilikuwa Erotica, na mada zake zilikuwa za moto sana na zilinivutia kiasi nikashawishika kumtaka urafiki.
Sikutumia PM kwenye kumwomba urafiki ila mwezi june 2012 nilisuka thread moja kabambe ya kutamani kuwa rafiki yake.
Baadhi ya wadau walinitahdharisha kwamba huyo ninayemwomba urafiki ni dume mwenzangu lakini nilipuuzia nikaona ni mikwara ya kawaida hapa jf.
Kweli Erotica akakubali kuwa rafiki yangu na marafiki zake - Kaunga na Elizabeth Dominick wakawa wanatupamba sana. Lakini muda wote kwenye urafiki, zilitokea kejeli za hapa na pale ila haikuniingia akilini kwamba nimeuvaa mkenge.Basi tukaendelea na Erotica yeye akiniita "my caramel" mie nikimwita "my emerald".
Tumeendelea hivooo na ilipofika oktoba 2013 Erotica akadai amejifungua mapacha wa kike-Triphona na Triphonia. Kuanzia hapo Erotica akapunguza sana kutokeza JF, wiki nzima haonekani mara huyoo yupo.
Ilipofika April 2014 Erotica kimoja kapotea mpaka leo.
Hisia Zangu. Erotica ilikuwa ni id ya uongo iliyoundwa na mwanaume wa hapa JF kwa madhumuni ya kuanzisha topics ambazo asingeweza kuzianzisha akiwa na hiyo id ya kiume.Mtu huyo alipoona mambo yamechanganya sana akaacha
kuactivate id ya Erotica.
Ila nashukuru mtu huyo hakuwa na nia mbaya ya utapeli kwani angeweza kabisa kubembeleza apate hela kidogo kwa ajili ya kuumwa, etc. Hilo halikuwepo hata kidogo. Mpaka sasa hivi naamini Erotica hakuwa genuine jf member ila character iliyoundwa tu.Huyo mtu mjanja sana aliyemchonga Erotica ni nani?