sitosahau jinsi nilivyoibiwa redio yangu ya mkulima.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Nilikuwa nimejilaza kwenye mkeka nje, kibarazani kwangu chini ya mti wa mpera huku nikiwa nasikiliza kipindi cha muziki wa zilipendwa katika redio yangu ya mkulima inayotumia bateri kubwa(1.5V) nne ambayo niliiegesha sentimeta kama 100 kutoka nilipojilaza huku redio nikiwa nimeipa mgongo.
Wakati muziki wa Jojina ukiendelee huku kwa mbaali kausingizi kakiwa kananinyemelea, ghafla muziki ukazima na nikasikia "samahani ndugu wasikilizaji tunakatisha matangazo kwa muda wa sekunde20 kisha muziki utaendelea.."
'Sekunde20 tu! Nitasubiri.' Nikajisemea.
Lakini akili ikafanya paa! Nikasema hii sauti mbona kama haikutoka redioni(si ya mtangazaji kutoka redioni!)!
Nikakurupuka. Lo! Nikaambulia kuona kijana akiwa ameishikilia redio yangu huku akitimua mbio na kutokomea nayo.
Kumbe ile sauti niliyoisikia ni ya yule kijana mwizi mkubwa anajua kweli kuiigiza sauti ya mtangazaji.
Maskini redio yangu.
 
Umenikumbusha redio yangu ya National made in Japan niliyoachiwa na mareh.baba yangu iliibwa nikiwa drs la6...sitoisahau daima sanasana kutokana na uwezo wake wa kulipasua anga kana kwamba nilikuwa na mitambo yote ya sattelite pale nyumbani
 
Duuu wezi noma kama hyo akili angeitumia kuzalisha umeme tusingekuwa na mgao.
 
Mwana hiyo muhusika alikuwa Ndumila kuwili gazeti la sani enzi za John Kaduma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom