Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

usipotoshe wenzako bwana wale ni wapiga dili. kila mchungaji ana Mungu wake na kiwango cha sadaka hivi lini Mungu alidemand certain sum?
 
"Sadaka unatoa kanisani maskini anakufa mtaa/ huo ni unafki wa kidini na siyo imani kabisaa/" ..Motra the future
Mtu anaenda kutoa milioni kwa Mzee wa upako halafu njiani kampita ombaomba ambaye angeshukuru hata shilingi mia.
 
Makanisa ya leo mchungaji ndio mweka hazina, ndio katibu wa kanisa, n.k Au mama ndio msaidizi na watoto ndio wazee wa kanisa unategemea nini?? Toa wale!

Kwa makanisa yanayojielewa sadaka zina mlolongo ambao sio rahisi mtu kutumia kujinunulia Brevis au helikopta!
 
ila wengi ni wezi wa sadaka. hayo mamilioni ya pesa wanayatoa wapi?
 
haswaa uzuri ni kwanza there are people who live on the stupidity of others. let them give
 
usipotoshe wenzako bwana wale ni wapiga dili. kila mchungaji ana Mungu wake na kiwango cha sadaka hivi lini Mungu alidemand certain sum?
Hiyo certain sum ni uongo sadaka unatoa chochote ni sawa na unavyosaidia yatima unatoa chochote huko kwa certain sum sijawai sikia anadhani asipotoa ndo huyo mchungaji atakua maskini .?
 
Hiyo certain sum ni uongo sadaka unatoa chochote ni sawa na unavyosaidia yatima unatoa chochote huko kwa certain sum sijawai sikia anadhani asipotoa ndo huyo mchungaji atakua maskini .?
hata sisi hatutaki wachungaji wawe maskini ila wasitajirike kwa sadaka.
 
Hata nami niliacha kutoa baada ya kumuona mchungaji wetu kanunua canter mbili za tani mbili mbili,wakati hana Njia nyengine za kujipatia kipato cha kumuwezesha kununua magari hayo.
 
usipotoa wenzako watatoa na soon
Mchungaji wako atamiliki hammer au chopa
 
Naona uende tu huko huko Katoliki maana hakuna namna. Kumbe wewe huenda kumtolea mchungaji?? Kakae chini kwanza ujiulize maana ya sadaka yako. Ati utawapa masikini. Bwana Yesu akasema; Masikini mnao siku zote. Nadhani umeingiwa na ile roho mbaya ya Yuda Iskariote wewe.
Nimekaa nkajiuliza; Mtu huyu alikuwa anatoa kiasi gani hapo kanisani?? Kiasi kwamba uliweza kumfanya mchungaji akanunua migari hiyo ya hali yajuu kwa mkupuo!!!
Mtu weye, chunga sana usemacho kwani nadhani wewe ni wale wenye kukaa na kuhesabu waendao kumtolea Mungu wao. Pesa yako ni yako ikiwa mfukoni mwako. Ukiamua kuitoa kama sadaka maana yake ni kuwa unamtolea Mungu si mchungaji. Laiti ungeliujua maana ya wito. Watu wameacha kazi zao nzuri zenye malipo makubwa wakaja kusotea sadaka hii ya kukejeliwa na watu ka wewe!! Mungu akusaidie tu.
 
Usipotoa sadaka unategemea mchungaji akale wapi?. Wenda ana wafadhili uko nje na marafiki wanamsaidia.
 
Wewe unatolea mazabahu si unampa mchungaji akinunulia magari ni shauri yake
 
hiii utabarikiwa '' daah sauti za wachungaji bwana '' wanatoa mpaka namba za simu ., '' sijui zamani walikuwa wanatoa anuani za nyumba zao? ili ukiwa na sadaka upeleke nyumbani? hatari
 

Makanisa yaliyo wordwide ndo makanisa, sadaka zao zina mchanganuo mzuri na wanatoa taarifa kwa waumini ...lakini makanisa ya single pastor kila siku injili za utajirisho na uponyaji hilo changa la macho kaka...wanakukamua tu hamna lolote
 
 
Makanisa yote ya kilokole hayatangazi mapato na matumizi. Wachungani wa Anglican, Lutheran na RC wana maisha yanayofanana na waumini wao.
 
Wewe unaenda kutoa sadaka Makanisa ya Kilokole unategemea nini..??

Makanisa yanayojielewa kama Katoliki, KKKT na Anglican ni mahala pa kutoa sadaka...Maana huko Mashule, vituo vya watoto yatima, hospitali zinajengwa..

Siku hizi wote wako sawa. Hakuna tofauti kati makanisa yanayojielewa na ya makanisa ya kilokole katika pesa. Hayo mashule, na hospital yamejengwa kwa misaada ya mashirika ya kidini kutoka nje ya nchi. Na ndio maana kila mara tunasikia migogoro katika makanisa. Tofauti iliyopo ni jinsi wanavyo ishughulikia migogoro hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…