Sitathubutu kumtukana kiongozi hadharani

jidula mabambasi

Senior Member
Jan 26, 2016
125
102
Kumekuwa na mambo mengi sana hasa kwa marais wetu wastaafu na waliopo madarakani, ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa mtu ambae alilifanyia taifa la Tanzania chochote cha kukumbukwa.

Kama yupo Tanzania anathubutu kusimama hadharani au kwenye media kuponda viongozi wetu hasa kwa ndugu yetu muheshimiwa Magufuli na kudhihaki juhudi anazozichukua kisa ni kwamba labda yeye au ndugu yake ni muhanga wa matukio ya ubadhirifu mkubwa wa mali za umma

Sasa binafsi najiuliza huu wizi ingeachwa tuu ili watu wachache waishi kama peponi hapa au?

Je, wangeachwa wangesemaje?

Nafurahia juhudi za rais pamoja na watendaji wake wakiwepo mawaziri.

Watanzania tuwe na kawaida ya kushukuru japo rais ni binadamu kama wengine anakosea tusimhukumu kwa uchache wa makosa yake tumhukumu kwa wingi wa wema wake.
 
Majitu yamekuwa ya ajabu sana mkuu. Kuna watu wameguswa na fagio la Chuma. Sasa wanapita huku kwenye mitandao na kuitukana Serikali. Watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi. Yakikamatwa majambazi majitu yanapinga...yakitumbuliwa mahujumu Uchumi majitu yanapinga...yakifanyika mambo kwa ajili ya Maendeleo ya nchi majitu yanapinga. Sijui Kipi ni bora kwa haya MADUBWANA.!!????
 
Ebu kuwa muelewa ndugu mtoq mada hapa dhana si kutukana bali ni kukosoa na wala si makosa mtu kukosoa pale anapoona panamakosa ila unajua kwann watu wqnachukia au kwann wanasema haki haitendeki mkuu usipende kusifia vitu huku unatambua kuna baadhi ya watu wanajiona bora kuliko wenzao kwasabab wqlisoma vyuo fulan maarufu na watu wakubwa serkalin ndo ifanye wachache waonewe au unadhan majipu yalivyotumbuliwa mtu wa chin kapata nafuu gani mpaka sasa hivyo usitishe watu kila mtu anauhuru wa kuongeq kwenye nchi yk bhana
 
Kuwaita Madubwana ni kuwakosea heshima madubwana wenyewe mana hao ni Zaidi ya MADUBWANA lol.
 
Kuwaita Madubwana ni kuwakosea heshima madubwana wenyewe mana hao ni Zaidi ya MADUBWANA lol.
Tehe tehe...umenishtua katika kuyakosea heshima madubwana. Maana madubwana hayastahili heshima hata chembe.
 
Wakati Mwalimu Nyerere na Sokoine wanawashughulikia wahujumu Uchumi, hamna mtu aliyesikitika zaidi ya hao wahanga wenyewe. Sasa hivi eti wasishtukizwe mara serikali itawalipa fidia nyingi na misamiati lukuki.Namuomba Magufuli na serikali yake kuwashughulikia hawa wahujumu uchumi kwa ukamilifu wake.
 
Mmepewa hongo au system ni system tu miaka 1000 mtakuwa mnadanganywa tu fisiem achana nao kabisa mkuu we fanya kazi axha kupaniki km unamkubali ww au kakuhonga usimlazinishe kila mtu amkubali ww km mtu anakosea lazima akosolewa APHEAVEL AROUND DA CORNER
 
Kwa hili sakata la umeya wa jiji la Dar na huko kilombero, acha watu waseme yote mabaya juu yake kwa kuwa amekuwa mnafiki, alisema yeye ni rais wa watanzania wa vyama vyote but maeenda kinyume. Kila binadamu ana hisia zote kama yeye, maumivu yanakikomo chake, pa kutukanwa wacha watu wafunguke pa kupongezwa atapongezwa pia, kwani yeye nani? Mitume na manabii wameyapitia itakuwa huyu?
 
Ebu kuwa muelewa ndugu mtoq mada hapa dhana si kutukana bali ni kukosoa na wala si makosa mtu kukosoa pale anapoona panamakosa ila unajua kwann watu wqnachukia au kwann wanasema haki haitendeki mkuu usipende kusifia vitu huku unatambua kuna baadhi ya watu wanajiona bora kuliko wenzao kwasabab wqlisoma vyuo fulan maarufu na watu wakubwa serkalin ndo ifanye wachache waonewe au unadhan majipu yalivyotumbuliwa mtu wa chin kapata nafuu gani mpaka sasa hivyo usitishe watu kila mtu anauhuru wa kuongeq kwenye nchi yk bhana
''Simu janja''
 
Juhudi za kuhujumu uchaguzi wa meya wa dar ni jipu sugu kwenye mwili wa Pombe mwenyewe hadi jipu limeoza mwilini kwake yeye kajikausha tu.
 
Naangalia kamusi ntarudi, nikisema nianze kukuelezea ntamaliza kesho lol
Asmaa,
Neno dubwana sioni kwenye kamusi. Neno hili ni Colloquial nadhani, Conversional or informal language conversation au neno la mtaani....du linasimama kwa maneno mawili ambayo si matusi Bali ni udhalilishaji....dudu au dude kwa mfano wa binadamu kuitwa du....bwana dudu hilo au dude! Haya nimewapa msamiati sawa na Shaban Robert ....endeleeni na mada yenu ya Madubwana mimivnipo naitwa Nakioze!
 
Back
Top Bottom