Mungu ni mkuu hakuna linaloshindikana kwake. Wasamehe wote walio kukwaza kwa njia moja au nyingine kwa sababu mungu amekuinua kutoka kwenye unyonge. Kumbuka adui yako ni adui wa mungu mwachie mungu apambane nae, mungu amesema mpende adui yako, wewe wasamehe then utaona baraka za mungu zitakavyo kushukia. Mimi baba alifariki nikiwa darasa la saba nilipitia changamoto nyingi ila nilimtumaini mungu bila kuwa na kinyongo na mtu yeyote leo hii ni mtu mwenye thamani mbele ya jamii inayo ni zunguka. Nimefurahi sana ushuhuda wako, mungu anapo tubariki ni lizama tusimame na kushuhudia ili kila mwanadamu ajue mungu tunaye mwabudu ni mwema siku zote. Mungu akubariki na akupe roho ya kusamehe ili neema na baraka zake ziendeleekuwa juu yako.
nimeona habari ingekuwa ndefu sana!! lakini nitarudi tena na Part II usijali
hii ni kweli tupu, haina hata chembe ya uongo kaka tena mambo mengi tu sijayaweka humu!!! mambo ya aibu!!
Hamna anaesema wote!Hao hawawakilishi kundi zima la wanawake.
Binadamu huwa wanasahau kwamba aliyemdogo leo kesho atakuwa mtu mzima na ataweza kujihudumia mwenyewe, ubinafsi na umaskini ni chanzo cha dhuluma kwa watoto yatima na wajane, lakini pia shida hizo huwa zinajenga immunity hakuna litakalokubabaisha ukubwani. pole sana
Pole mpendwa wangu kweli bila Neno la Msamaha kujaa ndani yako huwezi kusamehe kabisa,Namshukuru Mungu aliyejaza Neno la msamaha ndani yenu kwani ndiyo mlango wa mafanikio, na kingine Mungu aendelee kuwafanya Kichwa na wala si Mkia.
Abariki kazi ya mikono yenu Kituo chenu mnachokiandaa Kibamba Mungu akitumie kuwafuta machozi yatima wengine.
Pole sana Suzy siku zote tunaishi katika yeye atutiaye nguvu, pia maandiko yanaongeza msaada wetu unatoka wapi? Msaada wetu u katika BWANA ASISINZIAYE ATULINDAYE, pia majaribu ni sehemu ya maisha mtazame AYUBU. Naamini katika yeye atutiaye nguvu Umeshinda. Ntaendelea kuclose my finger tips to pray for you my love.
Dia nilitaka kushangaa leo sijakuona kabisa, Da Dena ndio kalia mpk kakimbia kabisa!! Nashukuru sana, maombi yako ni ya muhimu sana katika maisha yangu!!!