Sitasahau usiku ule: Alinifukuza kwake usiku kisa mwanamke!

Mdigokhan

JF-Expert Member
May 2, 2022
843
1,923
Kuna kipindi nilipoteza kazi na kufikia maisha yangu kuyumba sana, hivyo ikapelekea mimi kuanza kuuza vitu yyangu yya ndani ili nipate mtaji nianze biashara ili kujikimu.

Jiji la Dar ukiingia kwa mara ya kwanza unaweza usilielewe ukajionea kero tu na ukaona bora urudi zako mkoa, ila ukikaa kwa muda ukalizoea basi kuondoka jiji hili hata ije ile ya kubebea makontena Bandarini hutoki ng'o!

Basi bwana pamoja na kuuza vitu vyote vya ndani ila hata biashara iligoma na nililala chini na hata kodi ilipofika nilishindwa kulipa, hivyo ikanilazimu niombe hifadhi kwa rafiki yangu mkubwa nikae kwenye geto lake.

Huyu rafiki yangu kuna nyakati nyingi nilimfaa sana kwenye shida zake. Nilimsaidia sana hivyo akili yangu Ilimuwaza yeye kuwa niende kwake niombe hifadhi kwa muda usiojulikana nikijipange, sababu hajaoa ni geto tu analo. Basi nikamchek hewani, nikampanga na akakubari kiroho safi.

Basi Nilitoka zangu Gongo la mboto baada ya kukabidhi chumba kwa mama mwenye nyumba, then safari ya kuelekea kwa rafiki yangu Tegeta ikaanza mida ya saa 7 mchana. Safari ni fupi ila foleni la kufa ilifanya nikafika tegeta mida ya sa 12 ji0ni hivi. Nikam-chek hewani, jamaa akasema anajiandaa kutoka job Kariakoo hivyo itabidi nisubiri nje/

Nilikaa njee mpaka mida ya saa 4 usiku. Nililiwa na mbuu sana, nikajitembeza tembeza barabarani ilimradi kupoteza muda jamaa afike, nilipigwa na baridi nje nikimsubiri, basi mida ya saa 4 jamaa akawa kafika. Akanipokea freshi sababu tulishaongea kwenye simu na mazingira yangu anayajua hivyo hakukuwa na hadithi mingi.

Tukaingia ndani stori mbili tatu nikawa navuta usingizi maana nilichoka, pia mawazo kibao nikiwaza kesho yangu, je, itajitafutia yenyewe?! Tegeta nilishawahi kuja sana kwa mambo mengine, ila sijawahi kukaa sana, sijui mishe zozote za pale Tegeta pia sijazoeana na watu, yaani ni mgeni.

Kwakuwa nilitoka Gongo la Mboto nimekula mchana, ila mpaka mida ile ya kulala sijala kitu na nilimuangalia rafiki yangu kumwambia kuwa sijala, na sikuweza kula usiku sababu sikuwa na hela, yaani nilibaki na shilingi mia saba tu na niliiwaza niihifadhi hii chenchi ili kukikucha nipande gari niende zangu Ilala nikaangalie mishee mishee, halafu nauli ya kurudia ntajua huko huko basi nililala na njaa.

Nikiwa usingizini jamaa alianza niamsha hivyo nikaamka, kuangalia saa ni saa 6 usiku, yaani hata usingizi haujakolea vizuri. Akaanza nambie kuwa mpenzi wake anakuja hivyo inabidi mimi nilale kwenye kochi na hataki mpenzi wake ajue kuwa mimi nipo mule ndani. Maana mpenzi wake alimkataza kulaza marafiki, hivyo nilale kwenye kochi then anifunike na nguo Ili mpenzi wake asinione. Dah, nikaona freshi, no mara waaa!

Nikalala kwenye kochi akaweka nguo kama zote juu yangu, yaani kupumua nikawa napumua kwa pembeni. Basi dakika kadhaa mpenzi wake akaingia nikawa namsikia anamlalamikia jamaa tabia ya kuweka nguo kwenye kochi, ila jamaa akawa anajitetea anazipanga kesho hivyo walale zao. Basi wakalala zao kitandani, dakika 20 nyinyi nasikia wanaanza kutekenyana mara miguno wakaanza kufanya yao.

Mimi nikiwa kwenye kochi nikiwa nimejaziwa minguo, hewa nzito sipumui vizuri nikahisi uvumilivu unanishinda, maana joto na hewa nzito nashindwa hata kujigeuza vizuri kwakuhofia mpenzi wake atasikia kurupushani zangu. Nikasubiri wamalize walale ili nipate kujifunua nipate hewa, ila wapi. Sijui jamaa alikuwa na upwiru, yani hawamalizi.

Aah, uvumilivu ukanishinda nikanyanyua zile nguo nikainuka, maana nilihisi kufa kufa kwa lile joto na hewa nzito. Mpenzi wake alistuka akapiga kelele, jamaa akamtuliza akaenda washa taa. Dah, yule msichana alilia sana, akasema tulitaka kumpiga mtungo.

Kila akielekezwa haelewi, ikabidi jamaa aanze kunilaumu kwanini nilinyanyuka, ila nae kila nikimuelekeza kuwa nilikuwa nakosa hewa kaka ila haelewi! Ikabidi anifukuze usiku ule ule na begi langu mgongoni nitoke ndani mwake.

Nilimuombana sana maana Tegeta mimi mgeni, na usiku ule ni mkubwa na hakuna pahala napafahamu ila rafiki yangu yule hakuthamini hata chozi langu lililokuwa linaomba msaada kwa usiku ule tu. Hakuwa na chembe hata ya huruma, wala kufikilia urafiki wetu, wala mangapi nilimsaidia kipindi cha nyuma!

Alinifukuza usiku ule kisa mwanamke!
 
Back
Top Bottom