SoC03 Sitasahau jinsi bangi ilivyonipa ujasiri wa kuwa mwendawazimu

Stories of Change - 2023 Competition

EDOGUN

JF-Expert Member
Jul 9, 2023
256
296
Nakumbuka vizuri kuwa ilikuwa ni mwaka 2001 nilipoanza kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.Tofauti na watumiaji wengi wa dawa hizi kuanza kuzitumia wakiwa kwenye umri wa balehe ambao kwa wengi huwa ni muda wa kujaribu kila kitu, Mimi nilianza kuvuta bangi nikiwa mtu mzima kabisa, mwenye elimu na ufahamu wangu.

Nilijikitaa tu nimeanza kutumia bangi ili kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo lililokuwa likinikabili lililosababishwa na kitendo cha mke wangu kipenzi, Mariam, kunikimbia na kwenda kuolewa na rafiki yangu wa chanda na pete.

Kitendo alichokifanya mke wangu, kilinisababishia msongo mkubwa sana wa mawazo kuweza kuuhimiri.Nikiwa kama kijana mtu mzima nilijaribu mbinu tofauti tofauti za kukabiliana na hiyo hali lakini hazikunisaidia.

Mbinu niliyoona inafaa na hata inashauriwa sana na wataalam,ni kujichanganya na watu na kuepuka kukaa peke yangu lakini nayo ilishindwa kabisa kunisaidia, kwani kila nilipojaribu kukaa kwenye vijiwe vya wacheza drafti,bao na karata niliambulia kusemwa kimafumbo kitu kilichofanya niviepuke vijiwe hivyo kama ukoma na kufikiria ni kitu gani kingine nifanye kuusahau ukatili alionifanyia mke wangu.

Nikaamua kujaribu kunywa pombe lakini nayo haikunikubali,kwani nilipokuwa nikinywa kidogo tu natapika nusu ya kufa,kingine pombe ilikuwa na gharama kubwa kulinganisha na hali ya uchumi wangu kwa wakati huo hivyo niliona itakausha haraka mifuko yangu.

Nikakata shauri kuhamia kwenye uvutaji bangi ambayo kwangu niliona itakuwa ni nafuu sana kulinganisha na pombe,maana kwa shilingi mia tu nitaweza jipatia stimu za uhakika kabisa.

Kwahiyo nikawa nimefikia maamuzi ya kuvuta bangi kama tiba ya tatizo langu,lakini kumbe nilikua nayafungulia mlango matatizo mengine lukuki kuja kuniangamiza.

Wakati ninayapitisha maamuzi haya,nilijiona nimefanya maamuzi ya busara sana,ya kiutu uzima sana,lakini kumbe sikujua.

Sikujua kuwa nilichokifanya ilikiwa ni sawa na mtu kuamua kufuga mbuzi,ili amsaidie kufukuza paka wanaodokoa dokoa mboga jikoni kwake.

Sikujua kuwa nilichokifanya ilikiwa ni sawa na mtu kuung'oa mlango wa chuma cha pua,kisha kuweka pazia la kitambaa kizito,ili kujilinda dhidi ya tishio la wezi watumiao mawe makubwa kuvunja milango.

Huenda ni kweli nilikuwa na nia njema tu ya kukabiliana na msongo wa mawazo kupitia uvutaji wa bangi,lakini kumbe sikujua.

Sikujua kuwa kitendo changu cha kujiharalishia matumizi ya bangi kwa kisingizio cha kukabiliana na msongo wa mawazo kingeniongezea matatizo lukuki kwenye maisha yangu.

Kama utani vile,nikaanza kuvuta bangi,ingawa haikuwa rahisi kama nilivyofikiria.Wakati nimeamua kuvuta bangi ili zinipe lifti ya kupambana na mawazo,nilifikiri itakuwa rahisi sana,maana kazi ni kuwasha,kuvuta moshi kidogo kisha mawazo yote yanayonisumbua yanapotea yenyewe lakini kumbe haikuwa rahisi kama nilivyofikiria.

Nilifikiri kuvuta bangi ni kama kuwasha swichi ya umeme,unagusa tu kitufe cha ON,giza linapotea lenyewe lakini kumbe haikuwa hivyo,nilikuwa ninapotea.

Nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi mida ya saa kumi na mbili jioni,nilipoanza kuvuta bangi rasmi,baada ya wiki kadhaa za kubishana na mawazo yangu mwenyewe.

Baada ya kuvuta moshi wa kwanza tu,nilipatwa na hali ya ajabu sana,kwanza nilikiona kichwa changu kimekuwa kizito mno kiasi cha kuhisi siwezi kumudu kukibeba pasipo usaidizi wa watu.Nikaamua niongezee tu kuvuta moshi mwingine na mwingine huenda nitakaa sawa tu.

Nikaamua pia kwenda nje ya nyumba ili angalau nipate upepo, ila cha ajabu nilipotoka nje nikawa nawaona watu kama wako nusu hivi,nilikuwa nawaona watu kuanza kiunoni kwenda juu,miguu sikuiona kabisa.Nikakaa hapo nje nikistaajabishwa na hiyo hali ya watu kuwa nusu mpaka giza likawa limeingia.

Basi,kama utani nikawa tayari nimekuwa mvuta bangi.Licha ya bangi kufanikiwa kunipunguzia msongo wa mawazo kwani kila nilipoitumia iliniwezesha kutokujali sana kejeli na maneno ya watu juu ya kukimbiwa na mke,lakini hali hii ya kutokujali kitu ikaenda mpaka kwenye mambo ya msingi kabisa,ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo humtofautisha binadamu mwenye akili timamu na mwendawazimu.

Kwanza,nikaamua niache kwenda kazini,"kwa nini niutese mwili wangu kuhangaikia vitu ambavyo nikifa naviacha,kazi isiwe msalaba jamani."Nilijiambia.

Pili,nikaamua niache kunyoa nywele,maana nazinyoa ili iweje,kama nywele ingekuwa hazihitajiki kichwani zingeacha kuota.

Tatu,nikaamua niache kuoga, kwani kuoga ni kupoteza muda tu na ni uharibifu wa maji kwa nini nitumie zaidi ya ndoo nzima kuoga kila siku wakati kuna mamilioni ya watanzania wenzangu wanatumia masaa zaidi ya matano wakipambania kupata ndoo moja ya maji.

Nne,nikaamua niache kupiga mswaki kwa nini nikitese kinywa changu kwa kukisugua sugua na brashi ngumu,kwanza nasafisha ili kuondoa uchafu gani unaokuwa kinywani.

Tano,nikaamua niache kufua nguo,kwa nini nipoteze muda wangu wa thamani kufua wakati muda ni Mali.

Sita,nikaamua niache kunyoa ndevu na kuziachia kucha za mikononi na miguuni bila kuzikata

Saba,nikaamua nihamie mtaani, eti kwa nini nipoteze fedha nyingi kulipia nyumba wakati naweza kulala tu chini ya daraja bure.

Mwisho, nikaamua niwe nakula jalalani,kwani eti ni ujinga kutumia mamilioni ya fedha kila siku kununulia vitu vinavyopatikana bure jalalani.

Basi huo ukawa ndio mtindo wangu mpya wa maisha na sikutaka kabisa kuusaliti.

Opiyo sasa nikawa siogi,sifui nguo, sipigi mswaki, sinyoi nywele na wala sijisumbui kukata kucha.

Opiyo sasa nikawa nakula na kulala jalalani.

Kama utani vile, Opiyo nikawa mwendawazimu kamili, wakaazi wote wa Tarime wakajua kuwa Opiyo sasa ni mwendawazimu.Hakuna aliyejisumbua kunipeleka hospitali ili nipate tiba, sio ndugu zangu, sio marafiki zangu, wote waliniacha na kunitazama tu nikila na kulala jalalani.

Madaktari, manesi, viongozi wa mitaa, maafisa ustawi wa jamii wote waliniona ila hawakuona kama wanao wajibu wa kujua kipi kimenikuta, wao walijua tu mji wa Tarime umepata kichaa mpya .

Kula jalalani na kuongea peke yangu ikawa ndio maisha yangu mapya.Laiti kama Mungu mwenyewe asingeingilia kati, mpaka leo hii hayo ndio yangekuwa maisha yangu ya kudumu kama ilivyo kwa vichaa wengi tunaowaona wakiranda randa hovyo mitaani kwetu na kutojisumbua kabisa kuchukua hatua kuwasaidia ili warudie hali zao za kawaida.
 
Kumbe nimeingia cha kike,nilidhan huku ni km kule tu

Haya nielekeze namna ya kupiga kura nione km nitaweza kukupigia hiyo kura
Tafadhali bonyeza haka kaalama kenye umbo ^ kaliko chini ya huu uzi wangu na utakuwa umepiga kura & utapokea maua yako

Kingine,nakushauri hata wewe uweke andiko lako mkubwa kwani bado muda unaruhusu
 
Acha ujinga wew,unanipa maua ili iweje
 
Nakumbuka vizuri kuwa ilikuwa ni mwaka 2001 nilipoanza kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.Tofauti na watumiaji wengi wa dawa hizi kuanza kuzitumia wakiwa kwenye umri wa balehe ambao kwa wengi huwa ni muda wa kujaribu kila kitu, Mimi nilianza kuvuta bangi nikiwa mtu mzima kabisa, mwenye elimu na ufahamu wangu.

Nilijikitaa tu nimeanza kutumia bangi ili kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo lililokuwa likinikabili lililosababishwa na kitendo cha mke wangu kipenzi, Mariam, kunikimbia na kwenda kuolewa na rafiki yangu wa chanda na pete.

Kitendo alichokifanya mke wangu, kilinisababishia msongo mkubwa sana wa mawazo kuweza kuuhimiri.Nikiwa kama kijana mtu mzima nilijaribu mbinu tofauti tofauti za kukabiliana na hiyo hali lakini hazikunisaidia.

Mbinu niliyoona inafaa na hata inashauriwa sana na wataalam,ni kujichanganya na watu na kuepuka kukaa peke yangu lakini nayo ilishindwa kabisa kunisaidia, kwani kila nilipojaribu kukaa kwenye vijiwe vya wacheza drafti,bao na karata niliambulia kusemwa kimafumbo kitu kilichofanya niviepuke vijiwe hivyo kama ukoma na kufikiria ni kitu gani kingine nifanye kuusahau ukatili alionifanyia mke wangu.

Nikaamua kujaribu kunywa pombe lakini nayo haikunikubali,kwani nilipokuwa nikinywa kidogo tu natapika nusu ya kufa,kingine pombe ilikuwa na gharama kubwa kulinganisha na hali ya uchumi wangu kwa wakati huo hivyo niliona itakausha haraka mifuko yangu.

Nikakata shauri kuhamia kwenye uvutaji bangi ambayo kwangu niliona itakuwa ni nafuu sana kulinganisha na pombe,maana kwa shilingi mia tu nitaweza jipatia stimu za uhakika kabisa.

Kwahiyo nikawa nimefikia maamuzi ya kuvuta bangi kama tiba ya tatizo langu,lakini kumbe nilikua nayafungulia mlango matatizo mengine lukuki kuja kuniangamiza.

Wakati ninayapitisha maamuzi haya,nilijiona nimefanya maamuzi ya busara sana,ya kiutu uzima sana,lakini kumbe sikujua.

Sikujua kuwa nilichokifanya ilikiwa ni sawa na mtu kuamua kufuga mbuzi,ili amsaidie kufukuza paka wanaodokoa dokoa mboga jikoni kwake.

Sikujua kuwa nilichokifanya ilikiwa ni sawa na mtu kuung'oa mlango wa chuma cha pua,kisha kuweka pazia la kitambaa kizito,ili kujilinda dhidi ya tishio la wezi watumiao mawe makubwa kuvunja milango.

Huenda ni kweli nilikuwa na nia njema tu ya kukabiliana na msongo wa mawazo kupitia uvutaji wa bangi,lakini kumbe sikujua.

Sikujua kuwa kitendo changu cha kujiharalishia matumizi ya bangi kwa kisingizio cha kukabiliana na msongo wa mawazo kingeniongezea matatizo lukuki kwenye maisha yangu.

Kama utani vile,nikaanza kuvuta bangi,ingawa haikuwa rahisi kama nilivyofikiria.Wakati nimeamua kuvuta bangi ili zinipe lifti ya kupambana na mawazo,nilifikiri itakuwa rahisi sana,maana kazi ni kuwasha,kuvuta moshi kidogo kisha mawazo yote yanayonisumbua yanapotea yenyewe lakini kumbe haikuwa rahisi kama nilivyofikiria.

Nilifikiri kuvuta bangi ni kama kuwasha swichi ya umeme,unagusa tu kitufe cha ON,giza linapotea lenyewe lakini kumbe haikuwa hivyo,nilikuwa ninapotea.

Nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi mida ya saa kumi na mbili jioni,nilipoanza kuvuta bangi rasmi,baada ya wiki kadhaa za kubishana na mawazo yangu mwenyewe.

Baada ya kuvuta moshi wa kwanza tu,nilipatwa na hali ya ajabu sana,kwanza nilikiona kichwa changu kimekuwa kizito mno kiasi cha kuhisi siwezi kumudu kukibeba pasipo usaidizi wa watu.Nikaamua niongezee tu kuvuta moshi mwingine na mwingine huenda nitakaa sawa tu.

Nikaamua pia kwenda nje ya nyumba ili angalau nipate upepo, ila cha ajabu nilipotoka nje nikawa nawaona watu kama wako nusu hivi,nilikuwa nawaona watu kuanza kiunoni kwenda juu,miguu sikuiona kabisa.Nikakaa hapo nje nikistaajabishwa na hiyo hali ya watu kuwa nusu mpaka giza likawa limeingia.

Basi,kama utani nikawa tayari nimekuwa mvuta bangi.Licha ya bangi kufanikiwa kunipunguzia msongo wa mawazo kwani kila nilipoitumia iliniwezesha kutokujali sana kejeli na maneno ya watu juu ya kukimbiwa na mke,lakini hali hii ya kutokujali kitu ikaenda mpaka kwenye mambo ya msingi kabisa,ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo humtofautisha binadamu mwenye akili timamu na mwendawazimu.

Kwanza,nikaamua niache kwenda kazini,"kwa nini niutese mwili wangu kuhangaikia vitu ambavyo nikifa naviacha,kazi isiwe msalaba jamani."Nilijiambia.

Pili,nikaamua niache kunyoa nywele,maana nazinyoa ili iweje,kama nywele ingekuwa hazihitajiki kichwani zingeacha kuota.

Tatu,nikaamua niache kuoga, kwani kuoga ni kupoteza muda tu na ni uharibifu wa maji kwa nini nitumie zaidi ya ndoo nzima kuoga kila siku wakati kuna mamilioni ya watanzania wenzangu wanatumia masaa zaidi ya matano wakipambania kupata ndoo moja ya maji.

Nne,nikaamua niache kupiga mswaki kwa nini nikitese kinywa changu kwa kukisugua sugua na brashi ngumu,kwanza nasafisha ili kuondoa uchafu gani unaokuwa kinywani.

Tano,nikaamua niache kufua nguo,kwa nini nipoteze muda wangu wa thamani kufua wakati muda ni Mali.

Sita,nikaamua niache kunyoa ndevu na kuziachia kucha za mikononi na miguuni bila kuzikata

Saba,nikaamua nihamie mtaani, eti kwa nini nipoteze fedha nyingi kulipia nyumba wakati naweza kulala tu chini ya daraja bure.

Mwisho, nikaamua niwe nakula jalalani,kwani eti ni ujinga kutumia mamilioni ya fedha kila siku kununulia vitu vinavyopatikana bure jalalani.

Basi huo ukawa ndio mtindo wangu mpya wa maisha na sikutaka kabisa kuusaliti.

Opiyo sasa nikawa siogi,sifui nguo, sipigi mswaki, sinyoi nywele na wala sijisumbui kukata kucha.

Opiyo sasa nikawa nakula na kulala jalalani.

Kama utani vile, Opiyo nikawa mwendawazimu kamili, wakaazi wote wa Tarime wakajua kuwa Opiyo sasa ni kichaa.Hakuna aliyejisumbua kunipeleka hospitali ili nipate tiba, sio ndugu zangu, sio marafiki zangu, wote waliniacha na kunitazama tu nikila na kulala jalalani.

Madaktari, manesi, viongozi wa mitaa, maafisa ustawi wa jamii wote waliniona ila hawakuona kama wanao wajibu wa kujua kipi kimenikuta, wao walijua tu mji wa Tarime umepata kichaa mpya .

Kula jalalani na kuongea peke yangu ikawa ndio maisha yangu mapya.Laiti kama Mungu mwenyewe asingeingilia kati, mpaka leo hii hayo ndio yangekuwa maisha yangu ya kudumu kama ilivyo kwa vichaa wengi tunaowaona wakiranda randa hovyo mitaani kwetu na kutojisumbua kabisa kuchukua hatua kuwasaidia ili warudie hali zao za kawaida.
Hebu screenshot hako kaalama alaf unitumie maana nimeangalia sijakaona
 
Back
Top Bottom