Biashara zinazolipa sana January to March mwaka huu

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Ukitaka kutoboa ndani ya muda mfupi wa Mwezi January hadi March kuna biashara maalumu za kufanya, japo zinahitaji mtu asiye na aibu aibu, pia mwenye wito wa kibiashara. Ni biashara ndogo ndogo ambazo ukizizingatia kwa ufasaha, ndani ya miezi miwili iliyobaki unaweza tengeneza hela ya kununulia Boxer mpya kabisa

1. Biashara ya Maji Bahari

(Kwa wakazi wa Dsm)
Usiulize ni kwanini! Kodi guta, ingia Kawe, chota maji ya bahari madumu matatu hadi matano (kulingana na jitihada zako). Tafuta vichupa vya maji vya plastic vile vya Afiya. Pita mtaani, itapendeza kama utakuwa na kitangazo kinachoimba "Maji Dawa kwa bei poa". Uswazi, uza kikopo kimoja kwa Tsh.500, ukifika Sinza ama Oestabay, uza kimoja kwa Tsh.2000

Kama utauza vikopo 100 kwa siku ~ 100 × 500 Tsh (Bei ya Uswazi) ~ 50,000 Tsh, kwa miezi miwili ~ 30 × 50k ~ 1500k ~ 1.5m

2. Biashara ya maji moto yenye majani ya Chai Bora
Chemsha chai yenye hayo majani, ipooze kidogo, kisha pakia kwenye thermos, tafuta kijikombe cha Yatima, kisha pita mtaani, mwendo ni uleule "Pata Chai Tiba kwa bei nafuu". Ukipita maeneo ya changanyikeni, utajizolea wateja wa kutosha. Unaweza tengeneza mpaka 100k kwa wiki. Na hii pia ni kwa wana Dsm

3. Biashara ya miwani myeusi
Kwa wakazi wa Dar, wakulima wa miwani wanapatikana karibia na Bandari ya Mama. Hapo utauziwa miwani kwa Tsh.2500 kila mmoja tofauti na kununua kwa wapaguzi ambako utauziwa Tsh.4500. Hapo utanunua kuanzia Miwani 100 ~ 100 × 2500 ~ 250k ambapo kila miwani utaiuza kwa Tsh 10,000. Ni lazima kununulika kivyovyote vile. Kila miwani itakutengenezea 7.5k, utapata faida ya 750k per day. Je ukipiga kwa miezi yote miwili!!?

Vijana, tuacheni tabia ya kujitupa kwenye bahari kwa kusingizia eti maisha ni magumu, badala yake tutumie fursa tajwa hapo juu kujikwamua kiuchumi

Mtanikumbuka
 
Uza lemonade flani ivi matata watu wanapenda new things kama ilivyoanza alkasusu kuna mzee alipiga ela sanaa pale kati manzese miaka iyo 2018 hivi
 
Back
Top Bottom