B.G TANTAWI
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 495
- 375
Mod unganisheni hii na ile ya kwanza.
Baada ya kufika Bukoba yaani Nyumbani sasa, Mzee alienda kazini na Sisi tukabaki pale nyumbani, jioni mzee aliporudi alimuita ba mdogo na kumuuliza imekuwaje hadi akaambatana na mimi hadi Bukoba? ndipo ba mdogo alipomuelezea, lakini mzee alionyesha kukasirika sana akasema "Sitaki huyu kijana akae hapa" labda akasomee mbali na hapa" basi ndo ba mdogo alipomsihi kuwa "kaka msomeshe huyu kijana hebu tumuite tumuhoji kama anataka kusoma" niliitwa na nikahojiwa "unataka kusoma?" nikasema ndiyo! mzee akanyamaza kimya nikaambiwa rudi chumbani"
Kesho yake nikaambiwa nikapige picha za passpot size na akapiga simu Geita Sekondari kuulizia nafasi ya Form Five akaambiwa ipo na form ikatumwa nikajaza, wakati huo wote ma mdogo alikuwa ameninunia sana hataki kuongea na mimi na kwa bahati mbaya sana Mungu hakumjalia mtoto hadi sasa, basi ikafika siku ya kwenda Geita sekondari wakati huo ikiwa private school, baba alinipeleka hadi shuleni hapo na tulimkuta headmaster aitwaye Luhemeja baadae alikuwa Mwenyekiti wa CCM Geita, alinipokea na kweli nikapata nafasi, sasa kumbuka nilikuwa na Dvn 4-27 na nilikuwa na CREDIT 2 tu, kwa hiyo ikabidi nifanye kazi mbili kwa wakati mmoja, kwamba nasoma form 5 wakati huo huo nikijiandaa ku-resit paper ya form 4 ili nipate CREDIT Moja ziwe tatu ili ni-qualify kufanya mtihani wa form 6, Mungu alinijalia sana kwani paper ya form 4 nilipata CREDIT na mtihani wa form 5 kwenda 6 nilifaulu vizuri sana, na Final exam yaan NECTA ya form 6 nilifaulu vizuri sana kwa kweli mama mdogo alichanganyikiwa sana lakini akawa anasema kuwa sitafika ,mbali, tupo hapa!
Mwaka 2008 mwezi wa kumi nilichaguliwa kwenda Mzumbe University kusomea Sheria Mungu mkubwa nikamaliza salama salimini na sasa nimepata kazi, Mama wa kambo yupo kimya sana, sasa hapa nilipo na mimi sijui nilipe kisasi kwa kutomsaidia kitu chochote kabisa, hata senti moja asiiyone! yeye hadi sasa huu ni mwaka wa 13 hajapata mtoto na anavyoonekana ana mawazo sana ya jinsi ya kujirudi kwangu, ataanzaje? si alinidharau? kwa hiyo huu ni ujumbe tosha kuwa kama hakuna sababu ya msingi ya kumuacha mke wako usifanye hivyo, au usikubali kuambiwa tu na wewe fanya underground investigation, msidharau watoto hata kama si wako wa kuzaa!....mwisho.