Sitamsahau Mama Wa Kambo! Sehemu Ya 2.

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
495
375
Mod unganisheni hii na ile ya kwanza.

Baada ya kufika Bukoba yaani Nyumbani sasa, Mzee alienda kazini na Sisi tukabaki pale nyumbani, jioni mzee aliporudi alimuita ba mdogo na kumuuliza imekuwaje hadi akaambatana na mimi hadi Bukoba? ndipo ba mdogo alipomuelezea, lakini mzee alionyesha kukasirika sana akasema "Sitaki huyu kijana akae hapa" labda akasomee mbali na hapa" basi ndo ba mdogo alipomsihi kuwa "kaka msomeshe huyu kijana hebu tumuite tumuhoji kama anataka kusoma" niliitwa na nikahojiwa "unataka kusoma?" nikasema ndiyo! mzee akanyamaza kimya nikaambiwa rudi chumbani"

Kesho yake nikaambiwa nikapige picha za passpot size na akapiga simu Geita Sekondari kuulizia nafasi ya Form Five akaambiwa ipo na form ikatumwa nikajaza, wakati huo wote ma mdogo alikuwa ameninunia sana hataki kuongea na mimi na kwa bahati mbaya sana Mungu hakumjalia mtoto hadi sasa, basi ikafika siku ya kwenda Geita sekondari wakati huo ikiwa private school, baba alinipeleka hadi shuleni hapo na tulimkuta headmaster aitwaye Luhemeja baadae alikuwa Mwenyekiti wa CCM Geita, alinipokea na kweli nikapata nafasi, sasa kumbuka nilikuwa na Dvn 4-27 na nilikuwa na CREDIT 2 tu, kwa hiyo ikabidi nifanye kazi mbili kwa wakati mmoja, kwamba nasoma form 5 wakati huo huo nikijiandaa ku-resit paper ya form 4 ili nipate CREDIT Moja ziwe tatu ili ni-qualify kufanya mtihani wa form 6, Mungu alinijalia sana kwani paper ya form 4 nilipata CREDIT na mtihani wa form 5 kwenda 6 nilifaulu vizuri sana, na Final exam yaan NECTA ya form 6 nilifaulu vizuri sana kwa kweli mama mdogo alichanganyikiwa sana lakini akawa anasema kuwa sitafika ,mbali, tupo hapa!

Mwaka 2008 mwezi wa kumi nilichaguliwa kwenda Mzumbe University kusomea Sheria Mungu mkubwa nikamaliza salama salimini na sasa nimepata kazi, Mama wa kambo yupo kimya sana, sasa hapa nilipo na mimi sijui nilipe kisasi kwa kutomsaidia kitu chochote kabisa, hata senti moja asiiyone! yeye hadi sasa huu ni mwaka wa 13 hajapata mtoto na anavyoonekana ana mawazo sana ya jinsi ya kujirudi kwangu, ataanzaje? si alinidharau? kwa hiyo huu ni ujumbe tosha kuwa kama hakuna sababu ya msingi ya kumuacha mke wako usifanye hivyo, au usikubali kuambiwa tu na wewe fanya underground investigation, msidharau watoto hata kama si wako wa kuzaa!....mwisho.
 
msidharau watoto hata kama si wako wa kuzaa!....mwisho.

Mimi nadhani huo ndo ujumbe wa muhimu zaidi.

Bosi wangu anapenda kusema, "Unayemdharau leo, ndiye atakayekusaidia kesho"

Ben Carson's mother said, "Do not look down on people, for, the people you meet on your way up are the same people you will meet on your way down"

naam, na TUPENDANE.
 
Ina ujumbe mzuri ila ulivyoandika sehemu ya 1 na ya 2 ndio umetutoa kwa reli wengine.
 
mkuu kaswali kangu naomba ukajibu kwa ufasaha, ni kwanini wanawake wengi huwa hawawapendi watoto wa mume kuliko mwanaume akikutana na mwanamke anawatoto huwahudumia na kuwapa mahitaji yao tofauti na wanawake
tofauti yake ni ipi

mbe, habari ya hapa, swali gumu sana hili kulijibu. Ila maybe one day nitakuwa na jibu.

hadithi yako imenigusa

Sijui na mimi ntatoka?? Niwatie aibu hawa mahasidi!!

Mkuu, kama lengo lako ndilo hilo <bold> basi naomba kuungana na wewe kujiuliza hilo swali, "Sijui na wewe utatoka??"
 
Last edited by a moderator:
^^
Mama kambo wana mambo! Ama kweli Be nice to people as you go up You may meet them as you go down
^^
 
mkuu kaswali kangu naomba ukajibu kwa ufasaha, ni kwanini wanawake wengi huwa hawawapendi watoto wa mume kuliko mwanaume akikutana na mwanamke anawatoto huwahudumia na kuwapa mahitaji yao tofauti na wanawake
tofauti yake ni ipi
Inategemea na situation, mwanamke akimkuta mume tayari anawatoto akawachukia lazima anamatatizo na roho mbaya. lakini watoto wa kambo ambao wanazaliwa baada ya mume kuoa, tena kwa kumnyanyasa na ku m-cheat mkewe, uyasikie tu yasikukute wanasononesha moyo na kuondoa amani katika familia nyingi. Ndio mtoto hana kosa lakini upatikanaji wake lazima ulimuathiri mke na watoto, ndo maana inakuwa ngumu mwanamke kukubali mtoto wa kambo wa aina hiyo. Na wanaume wengine alizaa kabla anaficha siku yakimzidi ndo utasiki unajua niliwahi kuzaa, inakera na kuondoa amani maana hapo mke anakaa akiwaza amedanganywa mangapi. Lakini pia wapo wanaume wengi tu wasiopenda watoto wa wake zao waliozaa kwingine, ndo maana mara nyingi mwanamke aliyezaa akiolewa anaacha mtoto kwao.na wengine wanasimanga sana watoto wa wake zao wengine wanawafanyia mambo ya ajabu mpaka kuwabaka. Mtoto wakambo aje kwa sababu maalumu, mfano mke/mume kafa, lakini kizazi hiki kijana anaoa tayari mtaani anawatoto 2 tena mama tofauti, bado akioa nje vidumu kibao. hao watoto watapendekaje?
 
Asante mkuu nimekuelewa
 
Back
Top Bottom