Sitamani mapenzi, nimekinai kabisa

Sitamani mapenzi, nimekinai kabisa

redo

Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
20
Reaction score
17
Habari zenu,

Poleni na majukumu pamoja na pilika za siasa. Mimi ni mama mwenye mume na familia kiumri ni miaka 38. Ni mfatiliaji mzuri wa habari za huku leo nami nineona niwape ya kwangu. Kifupi nimechoshwa na mapenzi, sitamani mapenzi, nimekinai sitaki hata kusikia habari zake.

Mbaya zaidi siku zinavozidi kwenda sitaki hata kuhudhuria harusi au ndoa. Nikiona tukio hilo huwa linanitesa sana na hii ni baada ya kuona ndoa nyingi hazina amani, wanandoa wengi wanaishi maisha yasio na amani.

Nilibahatika kuchaguliwa nafasi ya malezi kanisani ambapo ndoa nyingi zilizokuwa zikija kuleta malalamiko kanisan nikiitwa na mch kutoa ushauri. Kwakweli nilikua naumia sana. Sikutamani hayo yanikute nilijua iwapo yatanitokea yatanitesa sana.

Sasa yamenikuta na yananitesa sana, nashindwa kujishauri japo kwa wengine nilifanikiwa kiasi fulan. Ama kweli mganga hajigangi. Kupitia kusikiliza ndoa nyingi zenye maumivu nilijitahidi sana kutimiza wajibu wangu kama mama, nilimpenda mume wangu, nilimjali sana, mara nyingi nilimsisitiza awe mwaminifu nami nilijitahi pia kuwa mwaminifu mume wangu si mlevi wa pombe ila ana kaulevi kake.

Jaman sikuamini kilichotokea, alitembea na mtoto wa kaka angu bila mimi kujua akatembea na hg na kumpa mimba. Siku niliyomfuma housegirl akakiri na kuniambia hata mtoto wa kaka yangu ametembea na baba ndio maana walikua hawapendani. Housegirl alirudi kwao na amejifungua. Mtoto wa kaka nae alirudi kwa mama ake nilimchukua baada ya baba ake kufariki. Ni zaidi ya miezi sita imepita nashindwa kumsamehe huyu mume, simtaman kabisa.

Nipo kwa kulea watoto ila ameniumiza sana. Sitaki kabisa kushiriki nae tendo la ndoa silitaman kabisa. Mara nyingi nilisikia taarifa mbaya za mume wangu nilipuuza hata nilipojaribu kumuuliza alikua mkali sana. Baada ya fumanizi hili yote niliowahi kusikia kumbe yalikua yana ukweli kabisa.

Nimeumia sana, sana. Nimemwambia na kumpa uhuru andelee tu na wao anaona wanamfaa mimi tena basi. Yaan ndoa hizi zina mambo. Polen wanandoa wote mnaopita katika kipindi kigumu. Mwenzenu nimeinua mikono.

Sijui kwanini ndoa badala ziwe na amani zinakua jehanam ya dunia. Mh!!
 
Pole sana ndoa ndoano kuta za znaficha mengi sana. Ndo maana staman hata kuoa
 
Hivi hujui kazi ya shetani ni nini jamani? Aisee polee ila usikate tamaaa Mungu yupo na atambadilisha huyo mume.. Bebaa maombi kwa ajili yakee na atabadilika. Naweza sema mtoto wa kaka yako mbaya ila mbele nikiangalia hata mumeo mbaya maana kama kaweza kwa mti mkavuu je wakwake atamuacha? Wanaume siku hizi ni magumegumee usione watu wanavumilia tuu watoto wakuwe.
 
Ndoa zingine yaan poa kweli si zote mbov
 
Asante wote. Ni kweli sio ndoa zote mbaya lakin asilimia kubwa za ndoa ni maumivu. Mke akiwa mwema mume mkorofi. Mume akiwa mwema mke mkorofi. Jaman sijui kwanini huwa tunasahau upendo wa mwanzo. Yana mume wangu
 
Pole dada, inaumiza Sana kwa kutendwa na umpendaye, kitendo cha kutembea na hg na wakaao nyumbani mwako ni unyama Sana but unapaswa kumsamehe mumeo ndo kaz ya shetan no kuua na kujeruhi
 
Lara 1 akipita hapa ataendelea kusisitiza kauli mbiu yake
 
Yaan mume wangu tangu tuoane sikuwahi kumuomba pesa ya mahitaji yangu au matumizi binafsi. Na hata mahitaji na majukum ya ndan ada za watoto nk tulikua tunasaidiana. Nguo, viatu nk nilijitahidi kumpamba hajui kununua soks underwear, mikanda sendoz vest nk. Nikienda kufanya shoping namfanyia hii ni kwa sababu nilikua nampenda na kumjali sana. Lakin tangu nigundue naishi na mtu asijua kupendwa ni nini. Nimesitisha mambo mengi sana.
 
Pole dadaangu mungu humlipa mtu ujila kulingana na kazi aliyoitenda pole xana muombe mungu akutie nguvu pia akupe moyo wa ujasili
 
Tangu ndoa ilipopoteza maana na kuwa chombo cha maadili imekua tafrani.


Ndoa ni ndoto yangu, ndoa ndoa
Ndoa ni ombi langu, ndoa ndoa
Ni usafiri wa ndoto yangu ndoa ndoa
Ni mpango wa Mungu wangu,ndoa ndoa


Lakini imegeuka mwiba, ndoa ndoa
Imeua maono yangum ndoa ndoa
Imekuwa ni mateso kwangu ndoa ndo




NAIMBA TU MIMI JAMANI.
 
Wapo wengi Wanaoteseka na Waliokata Tamaa Kama ww, Wengi wamelia sana hadi machozi kukauka na wengine Wameumia Sana Hadi Wamekuwa Sugu. Usilie na Kukufuru Mungu kwa Tatizo lako bali piga Goti Mbele Za Mungu na Kumkabidhi Tukio na Hangaiko lako Katika Maisha kwa kuwa Yeye Hajashindwa, hajawahikushindwa na Hatashindwa... Kulia sana na kukata tamaa Sio Suluhisho la ndoa yako. Mungu Akusimamie katika Hili
 
majaribu ni sehemu ya maisha... pole sana!!!

kuna wanaume nao wanalalamika hayo hayo kutoka kwa wake zao, bora ukakosea njia kuliko kukosea mtu wa kuingia nae kwenye ndoa.
 
Pole sana auntie. Tunashindwa jinsi ya kukushauri kwavile tayari mwenzetu unamaamuzi.

Any way pole sana
 
Duuu mumeo inabidi apewe tuzo maalumu ya utafunaji wa mipapure a.k.a papuchino
 
Back
Top Bottom