Sitakula siku 3 kusupport matembezi ya vijana wa magunia

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,899
Nimewaona vijana walitembea toka Geita hadi Dar kwa miguu, wakiwa wamevaa magunia katika kituo cha ITV. Nimesikia maneno yao na rafudhi zao, ni kweli ni watoto wa Tanzania kanda ya ziwa. Nimeona sura zao, zinawakilisha uwiano sahihi wa maneno na mioyo yao.

Maombolezo yao ni ya dhati. Wana uchungu na nchi yao. Wanajua nafasi yao katika taifa. Kwamba wazee wamechoka, wao ndio walinzi wa taifa. Wanahitaji kuonana na watawala. Watawala hawapo pamoja na watu. Wako busy na anasa. Wanakula, wanakunywa, na kulala usingizi mnono. Wakijua wako salama. Wanalindwa kwa bunduki na majeshi. Hawawakumbuki watanzania maskini wanaokufa na kupoteza mwelekeo wa vizazi vyao.

Watanzania hawa, hawana mtu wa kuwasaidia. Wakitaka kuonana na watawala ili waeleze hoja z.ao, wanaishia mikononi mwa polisi. Polisi ambao ndio walinzi wa watawala dharimu.

Wakiandika bila kuonekana wanapuuzwa. Wanaishia kudharauriwa kwamba ni wavuta bangi, wahuni, wasio kuwa n ahaki ya kuishi. Lakini ajabu, kodi zao zinachukuliwa na kama haitoshi wanalazimishwa kuchangia michango kwa nguvu bila ridhaa ili kuwanufaisha watawala. waliojipa uteule na haki ya kuishi maisha ya anasa milele.

Wakijaribu kupinga kelele, wanauawa na polisi. Polisi waliosahau kwamba hakuna udharimu na unafiki ulioleta usalama pale mabaya yanapokuja.

Mimi nimeamua kuungana na vijana hawa. Popote watakapokuwa, katika hali yoyote watakayokuwa nayo, na mazingira yoyote, nitakuwa nayo. Sintakula kwa siku tatu kuanzia kesho.

Naomba kama kuna mwingine anapenda kuwaunga mkono, naomba tuungane nao kwa namna yoyote inayowezekana. Hatuwezi sote kutembea kwa miguu lakini Mungu anaijua vizuri sadaka ya mioyo yetu kwa ajili ya vijana hawa na taifa.

Wale watakaoweza kufanya maombi ya kufunga, fungeni.

Watakao weza kuomba kwa Mungu bila kufunga kwa utaratibu maalumu kw aajili ya vijana hawa na taifa, ombeni. Hatutawasiliana namna na maneno ya kuomba. Roho Mtakatifu anayeomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa atamwongoza kila mmoja wetu nini cha kuomba mahala popote pale alipo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Tangu Tanzania iwepo, hakujatokea tukio kubwa la na la kizalendo kama hili la hawa vijana. Kiongozi mwenye akili hata kama si zotoe, alipaswa kuwa amelitambua na kutoa amri kwa watendaji wake kuwaacha ili apate kusema nao.

Tanzania ni yetu, itakombolewa na sisi.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki vijana wazalendo.
 
Wakiandika wanapuuzwa. Wanaishia kudharauriwa kwamba ni wavuta bangi, wahuni, wasio kuwa n ahaki ya kuishi. Lakini ajabu, kodi zao zinachukuliwa na kama haitoshi wanalazimishwa kuchangia michango kwa nguvu bila ridhaa ili kuwanufaisha watawala. waliojipa uteule na haki ya kuishi maisha ya anasa milele.

Wakijaribu kupinga kelele, wanauawa na polisi. Polisi waliosahau kwamba hakuna udharimu na unafiki ulioleta usalama pale mabaya yanapokuja.

Mimi nimeamua kuungana na vijana hawa. Popote watakapokuwa, katika hali yoyote watakayokuwa nayo, na mazingira yoyote, nitakuwa nayo. Sintakula kwa siku tatu kuanzia kesho.

Naomba kama kuna mwingine anapenda kuwaunga mkono, naomba tuungane nao kwa namna yoyote inayowezekana. Hatuwezi sote kutembea kwa miguu lakini Mungu anaijua vizuri sadaka ya mioyo yetu kwa ajili ya vijana hawa na taifa.

Wale watakaoweza kufanya maombi ya kufunga, fungeni.

Watakao weza kuomba kwa Mungu bila kufunga kwa utaratibu maalumu kw aajili ya vijana hawa na taifa, ombeni. Hatutawasiliana namna na maneno ya kuomba. Roho Mtakatifu anayeomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa atamwongoza kila mmoja wetu nini cha kuomba mahala popote pale alipo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Tangu Tanzania iwepo, hakujatokea tukio kubwa la na la kizalendo kama hili la hawa vijana. Kiongozi mwenye akili hata kama si zotoe, alipaswa kuwa amelitambua na kutoa amri kwa watendaji wake kuwaacha ili apate kusema nao.

Tanzania ni yetu, itakombolewa na sisi.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki vijana wazalendo.
 
Hakika Ee Mwenyezi Mungu umefika wakati sasa unyooshe mkono wako kwa ajili ya nchi hii,, watazame watawala uliotupa wamekengeuka na kusahau kwamba mamlaka waliyonayo ni wew ndio umewapa,, tunaomba Mungu sasa Fanya jambo kwa ajili ya nchi hii,, tuondolee watawala hawa nawe utupe wateule wako ili watu wako tupate ahueni ya maisha....... Mungu baba umesaidia mataifa mengi sanaa tunaomba sasa isaidie Tanzania yetu,, maovu ya watala hawa yamezidi kupitiliza Mungu......

Nakuomba Mungu Baba usikie kuomba kwangu kwa ajili ya nchi hii uliyotupa kama zawadi toka kwako......

AMEEN.......
 
Hoja yako ni nzuri wazalendo tuwaunge mkono vijana wenzetu. nchi hii ina utajiri mwingi lakini mafisadi wachache wanasomba kila kitu na kuhamishia nje...very sad
 
Najiuliza tu, hivi jk akiamuru hao police au mkuu wa wilaya awaruhusu vijana hao kuongea nao atapoteza nini? Mkuu wa wilaya nae simuelewi, miaka 4-5 iliyopita tuliambiwa kuna kijana toka huko huko Geita alisafiri na baiskeli hadi Dar kuja kumpongeza JK na alipewa nafasi; nyie viongozi mko tayari tu kupongezwa but sio kukosolewa!? how!?
 
Ndio hapo sasa tujue kuwa Viongozi wetu wanapenda sifa tu, kuimbiwa na kuchezewa ngoma. Ndio maana wajanja wanawapa titles tu udokta, Mara mlezi Wa vikundi Fulani ili kuhakikishiwa kura tu kwenye uchaguzi.

Vv
 
Ujinga tu huu!

Siwezi kuacha kula niwasapoti wahuni wanaotumiwa na vyama vya siasa kwa maslahi binafsi.

Badilikeni acheni kutekwa kirahisi hivyo!
 
inahuzunisha sana vijana wazalendo kutembea kwa miguu kutoka geita mpaka dar halafu wanaenda kuzuiwa kuonana na raisi na mkuu wa wilaya na kuwepelekwa central nimehuzunisha sana na huu ubabe wa serikali ya ccm ..mshindi wa mashindano ya ngono bigbrother alienda ikulu bila kuzuiwa lakini wazalendo wenye uchungu na hii nchi wanaishi mikonono mwa polisi wa ccm lakini ujumbe wao umeshafika kupitia vyombo vya habari JK amewasikia atawaita ikulu.
 
Mimi sigusi bia wala sili nyama kwa muda wa wiki moja ikiwa ni ishara ya kuwaunga mkono kwa maombolezo, na tayari nimeanza leo baada ya kuwaona
 
mim NAWAITA HAWA VIJANA NI KAKAKUONA RAIS WETU USIWARUHUSU HATA KIDOGO HAWA VIJANA WAHUNI WASIO NA UWEZO WA KUFIKILI EBU FIKILI MTANZANIA MIMI MWENYEWE NI KIJANA LAKINI KWA HAWA WAHUNI PLZ MH JK FUNGA GETI

KWANZA HAWA VIJANA WAMEBEBA BENDERA ZA CHADEMA SIKATAI NI HAKI YAO LAKINI WANATAKA KUTUAMINISHA KUWA WALIMCHAGUA RAIS JK KWAHIYO WAMEKUJA KUZUNGUMZA NAYE JAMANI HAWA WAHUNI WAKUBWA WANAUDANGANYA UMA JK PLZ USIFUNGUE GETI WAHUNI WAKAGUSA IKULU TAKATIFU

PILI NI MIAKA KUMI SASA IMEPITA TANGU JK AWE RAIS SIKUZOTE WALIKUWA WAPI? LEO WANAKUJA NA KUANZAKUMSUMBUA RAIS KWA MAMBO YA KIJINGA ILI WAPATE UMAALUFU AMBAO SOON WATAJUTA KWA NINI WAMEFANYA.

TATU RAIS JK KUWARUHUSU HAWA WAHUNI UTAKUWA UMEFUNGULIA MAGENGE YA WAHUNI WAKIDAI WAMEKUJA KUONGEA NA WEWE HII ITASABABISHA MUDA WAKO WA KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA MUDA HUU MDOGO ULIO BAKI KUPOTEA BULE

MWISHO NAOMBA KUTOA RAI KWA VIJANA WA TANZANIA RAIS WETU NI MSIKIVU SANA NA ANAPENDA VIJANA ILA KAMA KIJANA UNAZANIA UTATABEBA UTAIFA UKU UKIWA UMEBEBA BENDERA YA CHAMA FULANI HII ITAKUWA NI KUTUTUKANA VIJANA WOTE WA TZ KWANI TANZANIA INAVIJANA WENGI NA WENYE ITIKADI TOFAUTI HATA VIJANA WA CCM NA VYAMA VINGINE WANGEPENDA KUMUAONA RAIS ATATUE MATATIZO YAO.

HIVYO NINA AMINI KABISA BILA HATA KUWA NA SHAKA KWAMBA HAWA VIJANA WAMETUMWA NA CHADEMA NA SI VIJANA WALIO BEBA UTAIFA NA HILI LITAJIZIHILISHA KESHO AMBAPO VIJANA WENGINE WA CHADEMA WATAJITOKEZA NA KUFANYA FUJO NA MALENGO YAO KUFA KABISAA AHSANTENI.
 
inahuzunisha sana vijana wazalendo kutembea kwa miguu kutoka geita mpaka dar halafu wanaenda kuzuiwa kuonana na raisi na mkuu wa wilaya na kuwepelekwa central nimehuzunisha sana na huu ubabe wa serikali ya ccm ..mshindi wa mashindano ya ngono bigbrother alienda ikulu bila kuzuiwa lakini wazalendo wenye uchungu na hii nchi wanaishi mikonono mwa polisi wa ccm lakini ujumbe wao umeshafika kupitia vyombo vya habari JK amewasikia atawaita ikulu.

http://2.bp.blogspot.com/_HO8ijU76ZcQ/TPYjHvLbhEI/AAAAAAABUh0/v9Gf_3f4THg/s1600/8E9U2498.JPG
 
Raslimali na muda waliopoteza kufanya haya maigizo wangeweza kujenga hata kisima cha maji huko kijijini kwao! Wahuni sio watu!
polisi wa ccm mmechelewa ujumbe umeshafika JK atawaita ikulu kuwasikiliza nyie wahuni wachache mnapoteza muda wenu humu
 
Back
Top Bottom