Mkuu,
Watu wa ujenzi siku zote huwa tunafahamu kuwa, dawa ya matatizo yote ni kuanza. Ukisimama na kusema uyajadili kwanza ni kwamba hutafika mbali. Ndiyo maana huwa kuna plan za kazi kwa ujumla ila zile in detail zinakuwa zinafanywa kwa kila wiki inayokuja kwa kuangalia ile plan kubwa.
Matatizo ya Tanzania yanajulikana sana sana. Kwani nani hayatambui? Labda kama hayupo Tanzania au hajawahi kufuka kabisa. Sasa kuanza kusema sitaki hiki wala kile, THEN WHAT???
Inabidi kufika sehemu tuwe kama Mwanakijiji na kuanza kupigana kuibadili hiyo hali kwa njia moja au nyingine. Ningelitegemea watu waanza kusema "pale anapokaa, ataanza kuwakusanya watu ili kujenga mazingira ya usafi, kutunza barabara, kupanda miti na mauwa nk nk". Hii SITAKI haisaidii chochote na matatizo ya Tanzania yameshasemwa sana.