Sitaki urais, ni mzigo - Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitaki urais, ni mzigo - Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mopaozi, Jan 25, 2012.

 1. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Waziri mkuu Bw Pinda amesema kuwa hana nia wala hafikirii kugombea urais mwaka 2015 na kuwataka wanaomtangazia wakae chonjo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mgomo wa madaktari!!

  Huyu baba vp wagonjwa wanakufa kwa mgomo ye anazungimzia urais matokeo yake mantiki nzima ya mkutano wake haijaeleweka na madaktari wamekuja juu kuwa mgomo uko palepale hadi kieleweke!!

  Sitaki urais, ni mzigo- Pinda

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kutamka hadharani kwamba hana nia wala hataki kuwania urais mwaka 2015 Rais Jakaya Kikwete atakapomaliza muda wake, kwa kuwa kazi hiyo ni mzigo.

  Badala yake amesisitiza kuwa hatajisumbua kuingia katika kinyang'anyiro hicho kwani amejipanga vyema kuanza maisha mapya ya kufuga nyuki baada ya kustaafu.

  Aliyasema hayo jana ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mwelekeo wa nchi na masuala muhimu ya kitaifa yaliyojitokeza siku za hivi karibuni.

  Alisema mwaka 2015 atakuwa mtu mzima sana na haamini kuwa kwa umri huo ataweza kuyamudu majukumu ya nafasi ya urais.

  "Niliposema sitawania urais nilimaanisha hivyo na naomba watu wanielewe, urais si kazi ya kukimbilia kama kweli unataka kuwatumikia watu, kwa wale wanaotaka kwenda kuchuma sawa ni pazuri, lakini mimi naona ni mzigo, kuna wakati namwonea huruma Rais Kikwete maana kila kitu kigumu anaangushiwa yeye," alisema.

  "Mwaka 2015 nitakuwa na umri wa miaka 67, inamaana nikipata urais baada ya miaka mitano nitakuwa na 72, yanini nifike kote huko kwanini wakati nimeshalitumikia taifa langu muda mrefu sana, nimefanyakazi ya taaluma yangu ya sheria miaka mitatu tu nikaenda Ikulu ambako nimefanyakazi hadi leo hii, nimefanyakazi na Mwalimu Nyerere, nimefanyakazi na Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na hii awamu ya nne, kama watu hawajaridhika na mchango nilioutoa kwa nchi yangu inamaana hata nikiwa nani hawataridhika. Urais siutaki na wala siwazii wanaotaka waendelee tu," alisema.

  "Kuna wakati nikisema sitaki urais watu wananiambia acha kusema hivyo wewe, acha kabisa mzee usiseme hivyo, lakini mimi huwa nawaambia watu hawa kuwa huu ni uamuzi wangu na nataka Watanzania waelewe hivyo, anayetaka haya! Ila mimi sitakuwemo," alisema.

  Alisema anataka baada ya kustaafu ajikite zaidi katika ufugaji wa nyuki kwani amebaini kuwa biashara hiyo ina faida sana lakini Watanzania wengi bado hawajabaini fursa hiyo.

  Nafasi ya uwaziri mkuu tangu Tanganyika ipate Uhuru mwaka 1961 imeshikiliwa na watu tisa, wa kwanza alikuwa Mwalimu Nyerere aliyekaa kwa mwaka mmoja tu kabla ya kumwachia Rashid Kawawa; akimwachia Kawawa nafasi hiyo naye akaandaa nchi kuwa Jamhuri mwaka 1962.

  Mbali na hao mawaziri wakuu wengine ni Edward Sokoine ambaye wengi walitarajia kuwa angemrithi Mwalimu Nyerere, lakini maisha yake yalikatizwa na ajali ya barabarani Aprili 12, 1984.

  Wengine ukiacha Kawawa ambaye baada ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi alikuwa amekwisha kuwa mtu mzima mwaka 1992 hivyo kupoteza hamasa ya kuwania kiti hicho, ni Jaji Joseph Warioba ambaye mwaka 1995 alijaribu lakini hakufanikiwa; John Malecela naye mwaka 1995 na mwaka 2005 alijitosa katika kinyang'anyiro hicho lakini chama chake, CCM, kiliondoa jina lake mara mbili kabla ya kupigiwa kura kwenye vikao vya chama vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Wengine waliojaribu karata zao ni David Cleopa Msuya ambaye mwaka 1995 alijitosa kwenye kinyang'anyiro hicho, lakini kura hazikutosha kwenye Mkutano Mkuu wa CCM baada ya kushindwa na Kikwete na Benjamin Mkapa kisha Mkapa akapita katika raundi ya pili ya kura.

  Mwaka 2005 Waziri Mkuu Mstaafu ambaye alishikilia wadhifa huo kwa miaka 10 mfululizo chini ya Rais Mkapa, Frederick Sumaye, naye alijitosa katika mbio hizo, lakini aliishia NEC baada kupata kura kidogo akizidiwa na akina Kikwete, Profesa Mark Mwandosya na Dk. Salim Ahmed Salim. Kikwete aliibuka mshindi dhidi ya Dk. Salim na Profesa Mwandosya kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa mwaka 2005.

  Waziri Mkuu pekee ambaye hayatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo, ingawa huko nyuma alipata kujaribu nafasi hiyo akiwa waziri wa kawaida ni Edward Lowassa ambaye hadi sasa habari zinasema kuwa anatazamwa kama miongoni mwa wanasiasa wanaoitafuta nafasi hiyo.

  Katika mkutano wa jana, Pinda alisema watu wanaokimbilia Ikulu huenda wana jambo lao na si kuwatumikia wananchi kwani kiongozi mzuri ni yule anayependekezwa na watu awatumikie na si yeye kujipendekeza kwa wanachi.

  "Watu ndio waseme fulani unafaa tuongoze, lakini wewe kujipeleka wakati kule kuna kazi ngumu lazima kuna jambo utakuwa unafuata maana mimi nimekaa katika nafasi hii zaidi ya kazi ngumu sioni kipya," alisema Pinda maarufu kama mtoto wa mkulima.

  NAFASI ZA MADC

  Kuhusu wakuu wa wilaya kuchelewa kutangazwa, Pinda alisema sehemu nyingi kulikuwa na migogoro ya ni wapi yawepo makao makuu, lakini kwa sasa wameshamaliza na wiki ya kwanza ya mwezi wa pili watatangazwa.

  "Mzee (Rasi Kikwete), amesafiri na wakati nazungumza naye wakati wa kumuaga pale uwanja wa ndege nimemdokeza hilo akasema akirudi tu tutayamaliza, hata mimi hainipendezi suala hili kukaa muda mrefu hivi maana wakuu wa wilaya huko najua kazi haziendi wanamawazo kuhusu nafasi zao," alisema Pinda.

  UGONJWA WA MWAKYEMBE

  Kuhusu afya ya Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Harrison Mwakyembe, Pinda alisema hajui anachoumwa, lakini hata kama angekuwa anajua yeye si mtu sahihi wa kutangaza maradhi ya mtu.

  Alisema kwa kuwa maradhi ya mtu ni siri yake mwenyewe basi wanaotaka kujua anachoumwa ni vyema wanamwomba mwenyewe awaeleze na si mtu mwingine yeyote.

  AMFAGILIA MAGUFULI

  Kuhusu bei ya nauli kivuko cha Kigamboni, Pinda alimtetea Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kuwa alikuwa sahihi na alifuata sheria, ila kilichomponza ni maneno yake ya utani.

  "Magufuli anapenda sana utani na mimi nilimweleza kuwa uko sahihi katika kutekeleza sheria, lakini maneno yako yale ya utani utani ndiyo yamekufikisha hapo, nilimweleza waziwazi kuwa si kila mtu anaelewa utani," alisema.

  MAJIBU YA JAIRO ANAYO AG

  Kuhusu maazimio ya Bunge juu ya aliyekuwa Katibu Mkuu Nishati na Madini, David Jairo, alisema serikali imeyatolea maelezo maazimio yote na imempelekea Mwanasheria Mkuu wa serikali ili awashauri hatua zaidi wanazoweza kuchukua.

  "Katika maazimio yale tumetoa maelezo kila azimio na tumempa AG apitie ili atupe ushauri wa kisheria, kwa sasa anayafanyia kazi na bungeni tutatoa maelezo ya nini kimefanyika," alisema Pinda.

  POSHO KITENDAWILI BADO

  Akizungumzia posho za wabunge, Pinda alitetea posho hizo akisema kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi hivyo wakati mwingi wanatumia fedha zao kuwapa watu wenye shida.

  Pinda alisema wabunge wengi wamekopa katika taasisi mbalimbali za fedha hivyo mshahara wao wote unaishia kulipa madeni.

  "Mshahara wa mbunge ni milioni 2.3 akikatwa mkopo 800,000 anabaki na milioni 1.7 bado unakuta pale nje kuna msururu wa watu wana msubiri. Akifika jimboni hivyo hivyo, sasa kwa kweli posho hizi zinaweza kusaidia kumpunguzia mzigo," alisema.

  Alisema mapendekezo yaliyowasilishwa na Bunge kwa Rais Kikwete kwa ajili ya kuwaongezea posho wabunge hayajakubaliwa na badala yake suala hilo limerejeshwa kwake.

  "Bunge lilipendekeza suala hilo kwa Rais, na amenipa mimi nilishughulikie kwa hiyo litatolewa uamuzi ila watu wasidhani kuwa wabunge wanaishi maisha ya fahari sana jamani, wanashida kwelikweli," alisema Pinda.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mapaozi, ndo mchezo wao hawa kutaka kubadilisha burning issue mambo yanapokuwa na muelekeo kombo. Kumbuka wakati Richmond inarindima wakaanza kukimbilia Loliondo, bongo nzima burning issue ikawa babu, babu. Mie wala hanishangazi.
   
 3. n

  nandipha Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata akipotezea habari ashapata... Kesho ni kukomaa hata emergencies pia zistop.. Wanatunyanyasa na kutudharau hawa mabwana
   
 4. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Katiba mpya iweke ukomo wa mtu kuwa mbunge huyu jamaa amekaa sana kwny ubunge kama ngombare!!
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wanasiasa huwa wanayoyasema hayatoki mioyoni mwao ikifika muda utasikia ohh wazee wamekuja kwangu na kunishauri nichukue form na baada ya kusema hivyo sote tutanywea!
   
 6. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Wala usiutake uuwezi.hatutaki mtu wa kulia lia
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Mbona uwaziri mkuu ndio mzigo mzito zaidi!!?? au anajaribu kucheza na akili zetu huyu msanii?
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mh haki ya Mungu. Kama wabunge kwa mshahara wao wana "shida kwelikweli" sijui walalahoi ambao hata hawajui mlo ujao utatoka wapi wasemeje. Kauli zingine ni dhambi kwa kweli.
   
 9. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Katika wasanii na vilaaza tulionao kwenye serikali ya JK huyu ni no. 1. Hata siku moja huyu bwana hana maamuzi ni mtu wa kukwepa lawama.

  Tokea amekua waziri mkuu aliahidi kufanya mengi ambayo hata moja hajatekeleza badala yake amekuwa akitetea yale aliokuwa anapinga.Mfano alisema atashauri serikali ipunguze matumizi kupunguza misafara ya viongozi,kutotumia mavx nk

  Ona leo hii yeye antetea posho kwasababu eti wabunge wanakatwa 800,000/-Tsh kwa kukopeshwa ma v8.Anapoenda huko mikoani -kuna kipindi 2011 nilishuhudia kwenye msafara wake kuna magari takribani 30. Huyo ndio mtoto wa mkulima. Huyu ni **** ila historia itamuhukumu kwa unafiki.

  Huyu mzee hana mvuto na haiba ya uongozi.Hawezi kuwa kiongozi mkubwa kwa kuchaguliwa na wananchi.Hana uwezo wa kuleta fikra mpya za kimabadiliko na zinazotekelezeka . Yeye mwenyewe ameliona hilo ndio maana anazungumza hayo aliyoyasema.
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii imetoka wapi? wakati ialipochukua form za ubunge za 2010 alisema ni Mwisho kugombea Uongozi Nchini?

  Sasa hizi stories za Urais zinatoka wapi? viongozi wa kitanzania wanauduku wa kushangaza kweli, wana ritire wanarudi madarakani

  Hakuna Mwandishi wa habari anayeuliza swali wote wanapiga makofi na kufurahia sick sick...
   
 11. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Yesu na Maria!!!

  Yaani huyu hawezi pata kura yangu
   
 12. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  huyu na jk ni watu waliotokea kuaminiwa sana kabla hata ya kuona utendaji wao ktk madaraka waliyonayo sasa, ila sasa hii staili yao mpya ya kujitangaza imekuwa kero kwa hawa magamba
   
 13. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  That is what he replied when asked in the press conf. The quastion is hata kama angekuwa anataka, ANGEPATA?
   
 14. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Sizitaki mbichi hizi !... kuna mtu asopenda uRais jamani? watu wamekaa folen msusuru mkuuubwa wamesimamishwa wakati huo Mtukufu Rais ndio kwanza anakunjua shuka yaani ndio anaamka! huku Trafic amesimamisha watu wanasubiri mpaka Rais apite! mpaka atoke aoge amalize nyie mmesimamishwa tu mara ndio huyoooo anapita kwa kasi ya ajabu ! asitudanganye bwana !
   
 15. B

  Bakeza JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hata angeutaka! Urais wenyew husingemtaka yeye
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huwezi kujua. Labda angekuwa na maamuzi magumu
   
 17. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh!! Hii Ni aibu yani tunajifagilia tuna bonge la kiongozi Kumbe mtu mwenye we mwoga hvyo......amenifanya nikwesheni nafasi aliyonayo hv sasa......hv kuna maamuzi yeyote mazito Huyu mheshimiwa sana keshawahi kuyachukua tangu achukue ile posti kweli?! Nakumbuka moja tu aliyoisema ANAMSUBIRI bosi wake atue bondeni.
   
 18. zukuboy

  zukuboy Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  hayo ndio maneno yao siku zote tumeshawazoea?hawana jipya..ikifika siku utasikia anapigiwa simu ya maoni
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Hata mwanafasafa Plato alisema, kiongozi wa kweli ni yule anayeogopa madaraka.
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,736
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  ..lakini Pinda anasema anaogopa matatizo, siyo madaraka.

  ..wakati Pinda anaona Uraisi ni matatizo, wenzake wanaweza kuona ni an opportunity to solve those problems and do good for our country.
   
Loading...