Sitaki dawa


Kwangu mimi sikupi pole yaani pamoja na usomi wako wote hukuwahi kujua habari za ukimwi? Kama uliona wewe ni bingwa sana ungekuwa unatembea na kondomu muda wote au kwenu hukuwahi kufiwa na ndugu au jirani kwa ukimwi kiasi cha kukufanya uelewe ukimwi unavyopatikana? Hata hivyo kwa kuwa umeandika humu naamini hutajiuwa na dawa utakunywa na hutakufa kama unavyotarajia kwa sababu utakutana na watu wenye busara na mabingwa wa kunasihi mpaka utaianza dozi mwenyewe na baadaye utaona ni jambo la kawaida na wewe siyo wa kwanza kupata ukimwi, Hata hivyo ni ujinga kuamini kuwa wanaopata ukimwi wote na malaya kama wewe hapana ukimwi unampata mtu yeyote ila tunachokilalamikia hapa ni kupunguza percentage za kuupata wewe ulikuwa kwenye 85% ya kuupata wakati asilimia hizo ndizo zilitakiwa ziwe za kutoupata. Kama wewe ni mkristo kweli kama ulivyojinadi naamini utasoma kitabu cha isaya aya siikumbuki Mwenyezi Mungu asema hivi: Dahambi zako hata zikiwa nyekunduku yeye atazifanya kuwa nyeupe kama sufi na hapendezwi na kifo cha mtu muovu kwani mtu muovu akifa bila kutubu atakuwa ameangamia milele. Sasa wewe ka umalaya kako umeona utenda dhambi nyiiingi sana jiulize je hao wanauwa binadamu wenzao unawaweka kwenye kundi gani na wewe hauoni wewe una afadhali mara mia ? Sijaona uliposema kwamba wewe ni mwizi bali umeconfess kwa wewe ni kiwembe tu sifa zingine zote mbaya huna na ndiyo maana uliamini huwezi logwa. Mtu anayekusudia kujiuwa huwa hasemi kitendo cha wewe kujianika humu jf umepoa na kutakia maisha marefu na yenye mafanikio ukiwa mgonjwa kama walivyo binadamu wengine duniani na hii dunuia siyo yako peke yako na wewe siyo mtu special tofauti na binadamu wenzako. BADO MMOJA NAFUTIKA.
 
Deception usihangaike na mtu anaesubiri elimu na maarifa vimfate alipo
 
Mkuu nimesema trusted and reliable source kwa sababu wapo watu ambao huja na tafiti zao lakini zina proof wrong. Nitakupa mfano wa babu wa loliondo aliwapa Maji yake watu lakini hayakusaidia watu kupona HIV.
Uzuri wa vyanzo nilivyokuomba unipe taarifa ni kwamba conclusion hufikiwa baada ya jopo la wataalamu NGULI kuafikiana. Mkuu unaweza kututhibitishia kwamba W.H.O wanahusika katika kutengeneza HIV ( fake) Kama unavyoita?
 
Mentor katika ubora wake nimeisoma ikanikumbusha Verrosa story........asante kwa bandiko hili nitaprint niwapatie vijana wangu......hongera sana kwa kusaidia vijana wajitambue na wasifanye makosa ambayo itakuwa ni majuto kwao milele.....
 
Vizuri sana... Hata mim naamin atajikubali na dawa atatumia kwa sababu tupp walengwa wengi kama wew na tulishajikubali.. Kupata UKIMWI sio kwamba hutoweza kutimiza ndoto zako.. Life goes on...
 
I AM SORRY TANZANIA..I AM SORRY GUYS!

I AM SORRY JF AND ALL WHO CALLED ME MENTOR.

ADIOS...
Mentor



Tupo pamoja, mbona ukimwi kawaida, ni sehemu ya maisha. Magonjwa ya sukari, moyo, Bp, cansa na Mengi yasiyo ambukizika huua kwa haraka na kwa wingi kuliko ukimwi
 
Mentor upo vizuri katika story telling.. use your talent to earn money, getting scholarships etc

nikikumbuka mimi ni polisi, tanga yule dada wa kiarabu, verossa na hii ya leo nazidi kukubali unajua kuteka hisia za watu
 
Deception usihangaike na mtu anaesubiri elimu na maarifa vimfate alipo
Huyu mkuu anapotosha.ukiangalia kwa makini maelezo yake katika posts anazotoa anaandika jumla jumla. Atakwambia kuna watu wengi wamekuwa hivi mara wamefanya hivi.ukimbana kwa maswali anakwambia una kichwa kigumu hutaki kuelewa.
 
Ngumu kumeza .....mentor maisha yapo tu ukikubaliana na hali yko utaishi maisha marefu....SITAKI DAWA imewafanya watu jana walale na majonzi
Huu uzi ni NDI NDI NDI!!
Jana kutwa nzima kumepoa story ni hii,watu wamenyong'onyea...
Hili ni gharika!
 
Huu uzi ni NDI NDI NDI!!
Jana kutwa nzima kumepoa story ni hii,watu wamenyong'onyea...
Hili ni gharika!
Duuuh ni pagumu hapo mna yakikukuta utawaza mengi sana......hii dunia wote tunapita
 
Uandishi wa stori umesaliti uhalisia wa stori yenyewe.

Namaanisha huwezi kuwa "umevurugwa" kiasi hicho alafu few days later akili itulie kuweza kunyoosha stori kwa kiwango hiki...
 
Uandishi wa stori umesaliti uhalisia wa stori yenyewe.

Namaanisha huwezi kuwa "umevurugwa" kiasi hicho alafu few days later akili itulie kuweza kunyoosha stori kwa kiwango hiki...
Trust me watu tunatofautiana. Mimi mwenyewe hakuna muda ambao Naandika vizuri (kwa mtazamo wangu) kama nikiwa "emotional". Usishangae kuna mtu akiwa na matatizo anaandika kwenye social networks, inampa relief kubwa sana. Kila mtu ana njia yake ya kuexpress furaha au huzuni yake. Mwingine atalia, mwingine atapigana, mwingine atalewa, atatukana, ataandika etc. (Ingawa kwa story hii daah, basi tu)
 
Hiyo dawa inatibu nini?

Kuna kuathirika na VVU na kuna kuanza kupata magonjwa nyemelezi.
ukimwi haitibu...ila virusi vya ukimwi kwa asilimia 89...inaondoa...nimekujibu wewe tuu mimi sio mganga na wala sitangazi biashara
 
Mentor i can't believe? ni kweli au unatania???

Pls naomba tuonane
Kumbuka kuwa huo sio mwisho wa maisha ni bora umejifahamu na umejua pls nitafute nikupeleke kwa wanasaikolojia
 
...sisy darling, story imepoteza hisia zako? Naamini hakugusi mtu kwa mda
. Haya sasa tukapime, nakusindikiza usijali

Mentor ni msimuliaji mzuri sana, ametupa awareness tu, at least naamini hivyo.
 
Hhahaahhahaa sidhani kama ni kweli, Mentor ni mtunzi mahiri sana sana unakumbuka story yake ya Polisi? au shairi lake la Verrossa lilivyokuwa gumzo? Lisome hapa utaona jmaa ni mwana harakati dhidi ya UKIMWI

Verossa
Ninatamani aseme ni story tu ili kutuelimisha... Inaniwia ngumu kuamini hiki alichoandika. Ila kwakua imetoka kwake mwenyewe najilazimisha kuamini japo naamini akiamua anaweza kuendelea kama kawaida na maisha yake mazuri tu
 
Hapa nimeamka na kwanza nikafungua huu uzi ili nione pengine jamaa amekanusha na kusema alikua anatupa simulizi ya kutunga

Duh, story yenyewe ni km episode1, naona km anakuja na 2 yake ya kukanusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…