Sitaisahau siku ya interview

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,583
Habarini Wakuu.

Naomba tuianze Wikiendi kwa namna hii.

Maisha yalibadilika sana, kila mara nilikuwa mtu wa kukaa ndani kama mwali aliyetolewa mahari ya kisukuma. Wapi niende mimi Joka jeusi, sina hela na hata vile viwalo vyangu nilivyomaliza navyo chuoni vilishaanza kuchakaa. Kismart foni changu ndio hivyo tena kilipoteza mwonekano wa kibrazameni. Si yule Joka jeusi wa enzi zile nikipita mitaa ya Yombo 4, Cafteria, na katika Viunga vya mdigrii. Joka jeusi niliyekuwa na hisa kubwa ya mademu wakali chuoni. Kila nikiyakumbuka maisha ya chuoni nilibaki kuumia na kusononeka kusiko elezeka.

Sikujali masomo kivile nilipokuwa chuo, mara nyingi nilikuwa nadoji vipindi hasa vile vya jioni, vya ijumaa na jumatatu. Group discussion nilikuwa sishiriki mpaka ikafikia hatua ya kukataliwa na wenzanguhivyo mara nyingi nilikuwa napiga kazi mwenyewe tena kwa kuchelewa. Alihamdulilahi chuo nilimaliza nikiwa na Ka-GPA kamanati.

Kila nilipo-apply niliambulia jibu la mjinga Yaani sikuwahi kuitwa kwenye Usaili wowote Ule. Pengine ni haka Ka-GPA kangu ka-32 ndiko kanako nifanya nisiitwe kunako usaili. Niliwaza sana kwa nini sijawahi itwa hata mara moja tuu angalau nitoe gundu mbona wapo baadhi ya vilaza wangu wameitwa tena wengine na kazi wamepata. Kuna wakati ilibaki kidogo niamini huenda ninakifungo kama Manabii wa dot.com A.K.A Manabaii Uchwara wanavyojinasibu huko madhabahuni kuwa kuna watu wamefungwa wasipate kazi.

Awali mtaani kwetu nilipomaliza shule watu walinipongeza na kunitia moyo kuwa japokuwa kazi zimekuwa ngumu lakini Mimi nitapata tuu. Moyo ulizingirwa na matumaini makubwa na roho ya ushindi ilinivaa kama wigi la Giggymoney. Muda ulienda na hali ya wasiwasi ilipiga hodi nafsini mwangu. Watu wale wale walionitia moyo kuwa nitapata kazi mapema leo ndio hao hao walioniambia kulikoni mpaka sasa hivi unaranda randa tu mtaani na kulala lala mithili ya paka wa kijerumani.

Kuepuka maswali kutoka kwa majirani niliamua rasmi kukaa ndani tuu. Mademu zangu wako wapi. Wameenda wapi. Mbona walikuwa wakinisifia na kuniambia vinyimbo na mapambio kama vile ya chama fulani hapa nchini. Zile bilinge bayoyo zimeishia wapi. Masikini Joka jeusi. Nilikumbua demu mmoja mmoja na viapo vyao. Nilibaki kujicheka na kujidharau kwani nilijiona ni kijana mjinga ambaye nilistahili kupewa adhabu kali bila huruma. Si mimi niliyekuwa nahonga videnti vipesa vya bumu kama mtoa misaada Ya USAIDs. Mbona leo hata hela ya kula inanitoa kamasi. Si mimi niliyekuwa na kimbizana na fashion kama mwanamitindo wa kimataifa kumbe Masikini wa kutupa. Mbona sasa sina hata troza moja ya mtoko. Loo Salaleh!!

Ya Mungu si ya Dr. shika Bahati ikaja. Bahati ya Joka Jeusi kupaa angani na dreamline sijui bombadiee mtajua wenyewe.
"HABARI JOKAJEUSI, UNAHITAJIKA KESHO SAA 08:00 ASUBUHI HAPA POSTA JENGO....... KWA AJILI YA INTAVIU, AHSANTE"
SmS hiyo ilinipasua moyoni, nilihisi nimeona nyota ya kadril. Sasa nitavaa nguo gani, hii ndio ilikuwa changamoto. Kusota miaka minne kitaa si lelemama Jombaa. Unaishiwa mpaka boxer ya kubadilisha unakata tuu vijinsi ndio vinakuwa vipensi kama vya komando kipensi.

Potelea pote nilifika na idadi ya wasailiwa ilikuwa si haba. Wapo waliokuja na mikoko, wapo waliokuja na suti, wengine mikanda nje. Kwa wadada nao hawakuwa nyuma kufanya tukio lile liwe la kipekee. Wapo waliokuja na viguo vifupi ungedhani ni maonyesho ya mapaja na hipusi(hipsi). Wengine walivalia mawigi basi tu ilimradi walivyoona. Wenzangu na mie tulivaa masulupwete na lakuchumpa.

Sikujali, muda wa usaili nilikaa na kidosho mmoja dizaini wakimataifa hivi si unajua tena kazi za bombadiee Lazima vitoto zikali kama hivi havikosekani. Basi yule binti kuna swali akakwama akipiga jicho kwenye paper yangu mimi ndio naishia mstari wa mwisho ili nigeuze ukurasa. Mapigo yake ya moyo yalikimbizwa na hofu ya kufeli. Joka nikaona isiwe kesi, nikauza mechi kisela naye hakufanya hajizi na mimacho yake mikubwa ungedhani ni kitenesi cha gofu.

Usaili uliisha tukatoka, demu alinishukuru sana ungedhani mimi ni masihi. Tulibadilishana mawasiliano kisha tukaagana. Nilimsindikiza na macho nikashangaa demu anafungua mlango wa gari aina ya Harrier modern. Si kwamba sikuamini bali nilijishtukia kuwa huenda Bwana amenena nami kwa ishara. Aligeuka nyuma akaniomba anipeleke home. Duu sasa si msala huu. Yaani nimpeleke kule kwa Bibi Nyau kwa kina Diamond. Niliapa kimoyo moyo siwezi kabisa kumpitisha malaika kwenye shimo la taka taka. Kwa wasioifahamu Tandale ni kuwa, Tandale ndio kata pekee duniani inayoongoza kwa uchafu. Kama ni hivyo sikuona kosa lolote alilonitendea yule demu kiasi nimlipe kwa kumpeleka Tandale.

Mawasiliano yalianza rasmi kwa njia ya Watsapu. Manzi alijitambulisha kwa jina "Jemy". Nilipojitambulisha kama Joka Jeusi alishtuka sana. Aliniuliza kwa nini naitwa Joka jeusi. Nikamjibu ni jina nimelirithi tu kutoka Babu yangu. Aliniuliza pia kuwa ninalipenda, nikamjibu bila shaka.

Basi mapenzi huzaliwa popote, huzaliwa pasipo matarajio Japokuwa hukua kulingana na jitihada za wapendanao. Taratibu tulizoeana, jemmy alitaka tuonane ila mimi mara kwa mara nilikuwa natoa udhuru. Si kwamba nilikuwa nakataa hasha ni kutokana na kutokuwa na pamba za viwango.

Siku moja niliamua liwalo na liwe, nilifungua kabati langu la nguo na kuanza kuchangua changua kuona ni nguo ipi ingenifaa. Huuuu! nilishusha pumzi kwa kuchoka. "kweli sina nguo" Nilisema nikiwa nimeegemea ukuta na mgongo kama mtu aliyekata tamaa. Mwisho nilichukua zile zile nguo za siku ile ambazo kimsingi ndizo zenye nafuu. Embu wewe fikiria umepanga ukutane na demu mkali then unavaa nguo ya kuchomekea mithili ya Marehemu Papa Wemba(Mungu amrehemu).

Tulikutana katika moja ya hoteli zilizopo mikocheni. Moyo wangu ukiwa kama bahari iliyochafuka. Sikuwa na amani, muda wote nilikuwa na hofu na wasi wasi ungedhani ni Fisadi anayenyemelea mfuko wa JPM. Si kingine kilichokuwa kinanisumbua zaidi ya kutokuwa na pesa, na miguo mibaya niliyoivaa. Embu ipige picha ya kijana wa umri wa miaka 24 akiingia hoteli ya gharama akiwa kavaa miguo kama kituko, mabwanga yasiyo na haiba. Aibu ilinishika mkono nami nilikubali.

Jemmy alikuwa kapendeza sana nusura ni msahau. Alivaa kigauni kivupi sana ambacho kilishindana na mapaja yake makubwa yaliyokuwa yakimeremeta sana. Rangi yake ya kahawia iliyopakwa mafuta yenye harufu ya uturi uturi ilizidi kunifanya nihisi nipo peponi. Jemmy licha ya uzuri wa uso ulioshahibizwa na macho makubwa na pua iliyoundwa vyema pia alikuwa ana umbo ambalo wengi wa wanawake hulitafuta kwa udi na uvumba.

Watu wengi kwenye ule ukumbi walimtizama mithili ya luninga ionyeshayo michezo ya hisia. leo mrembo huyu alikuwa mbele ya Joka Jeusi kijana niliyekuwa nimevaa mabuga buga tuu. Si wewe tuu hata mimi siku ile nilidhani ni stori ninayoiota ndotoni lakini kila kitu kilikuwa Mubashara na wala sio stori ya kutunga.

Tulizungumza mengi, na ndipo nilipogundua kuwa Jemmy alikuwa mtoto wa balozi mmoja kutoka nchi za nje (jina kapuni). Alieleza namna alivyovutiwa na mimi mbali na msaada niliompatia. Nami nilimwambia asiwe na hofu, Joka jeusi ni Asali ya wadada wakali kama yeye. Alitabasamu lakini alikunja uso kisha akaongea akimaanisha. "Mimi sitaki uwe Asali ya warembo. nataka uwe Asali yangu" Maneno hayo yalijirudia jirudia kichwani mwangu kama mwangwi katika pango.

Alinisogelea karibu na kuniegemea. Muda wote nilihisi ni hadithi kama wewe msomaji unavyohisi. Lakini ndivyo ilivyokuwa. Tuliingia room tukiwa tumekumbatiana kama zabibu katika kichala chake.

Jemmy ni mzuri jamani, heri tu ni wahadithie tuu kuliko mngeona wenyewe. Zaidi ya yote nilimtafuna kwa taratibu kama vile slow learner, kisha nikaenda mwendo wa hakatwi mtu hapa. Hapo ndipo niliposikia lugha halisi ya Jemmy. Jemmy aliongea ki-thailand kabisa. Moyoni nikajua kumbe jemmy ni chotara la kibongo na Kitailand.

Tulimaliza, na mwisho tuliagana.
Jemmy aliitwa kuanza kazi mimi nikabaki na GPA Yangu 32.

Kwa sasa Jemmy yupo Kwa Tirampu, Mimi nipo kwa Bibi Nyau.

KARIBUNI WIKIEND
 
Back
Top Bottom