Sitaisahau Mombasa

Kheri ya Mwaka Mpya 2017 wana Jamvi..

Ndugu zangu wana JF katika kutafuta namna bora ya nitakavyoumaliza mwaka 2016 na kuingia 2017 niliamua kutembelea Mji wa Mombasa. Na hivi sina majukumu mengi (yaani sina Mke wala mtoto) kwa hiyo niliona gharama za safari hazitokuwa kubwa sana.

Ukweli sinaga mazoea ya kusafiri mwisho wa Mwaka (Sababu Wanasemaga Ajali nyingi hutokea mwisho wa mwaka)ila kutokana na jinsi mwaka 2016 ulivyokuwa mgumu kwangu (Nimepitia mambo mengi sana kwenye Maisha yangu mwaka 2016, nahisi nilianza kusoma namba za Kirumi kabla ya wengine)

Baadhi ya Mambo niliyopitia mwaka wa 2016.

1. Kampuni niliyokuwa nafanyia kazi ilifungwa kwa hiyo wafanyakazi wote tulisimamishwa kazi.
2. Kufuatilia Pesa zetu PPF wakasema hawatoi Pesa kwa sasa.
3. Mara hoo nasikia wadaiwa sugu bodi ya Mikopo tunatakiwa kulipa madeni.. Nitaitoa wapi pesa na kazi sina. Kwanza kazi yenyewe nilipata miaka 3 baada ya kumaliza Chuo.
4. Nikasema nilime matikiti maji (Sababu niliambiwa kuwa matikiti maji yanalipa sana), Mvua ilinyesha kubwa matikiti maji yote yakaozea shambani.
5. Nikasubiri labda na mm jina langu litakuwepo kati ya Ma DC au Wakurugenzi waliochaguliwa na Mtukufu Rais lakini wapi.. Nawaona vijana wenzangu tu waking'ara, mm sipo kwenye orodha.
6. Nikaanzisha biashara ya kusafirisha nyanya kutoka Iringa mpaka Dar lakini biashara ikafa kutokana na ukweli kwamba sikuwa na elimu ya kutosha kuhusu biashara niliyokuwa nafanya.

Back to the topic

Hivyo basi kutokana na mikasa hiyo na mingine mingi, nikaamua sio mbaya nitoke kidogo ili kurefresh Mind maana sio kwa stress nilizokua nazo.

Nakumbuka nilimshirikisha rafiki angu mmoja juu ya safari yangu hii ya Mombasa, aliniuliza swali moja tu 'Unaenda Mombasa, utarudi kweli?' Sikuelewa kwa nn aliniuliza vile.

Hatimae Safari yangu ikafanyika na nikafika Mombasa Salama..Mji wa Baharini.. Nilichojionea Mombasa hakika sitasahau..

Mombasa kila kona ninayopita nakutana na watoto wazuri sana(Wanawake).. Yaani sijapata kuona hali hii kwenye miji kadhaa niliyowai kutembelea ikiwemo South Africa, China, Dar es Salaam na Nairobi.

Hawa watoto si wa mchezo mchezo jamn

Huu ni upendeleo wa wazi kabisa, haiwezekani mji mzima watoto ni wazuri mpaka mtu mzima unachanganyikiwa hujui umchague nani.

Nilidhani Tanzania ina watoto wazuri kuliko Kenya kumbe nilikuwa najidanganya.. Na ndo mana wana ule msemo wao wa Mombasa Raha.

Nilipanga kuondoka mara baada ya kuuona mwaka mpya wa 2017 lakini mpaka sasa ticket sijakata na naona kuna kila dalili za kutafuta kazi huku ili niamie kabisa huku..

Na jinsi watu wanavyoisoma namba huko, ndo sirudi tena.. Bodi ya Mikopo waweke tu utaratibu niwalipe pesa yao nikiwa huku.. Maana sio kwa kutudai huko.

Pesa zetu za PPF hawatulipi wanasema mpaka tufikishe umri wa kustaafu ila Pesa zao za HESLB wanataka tuwalipe sasa hivi.. Si na wao HESLB wasubiri mpaka tufikishe umri wa kustaafu ili wakate pesa yao kwenye Pension zetu za PPF..

Tanzania mpaka uwe na pesa mingi ndo umiliki mtoto mzuri, huku mambo ni tofauti hata Houseboy yuko na demu mzuri coz mademu wote huku ni wazuri (Hapo nimeandika kama Mkenya vile nimeshaanza ku imitate )
Upo Mombasa sehemu Gani ??
 
Back
Top Bottom