Sita & jaji warema wachunge midomo yao kabla ya kuongea!!!-dk silaa

sijafulia

Member
Mar 26, 2010
86
2
Dk Slaa awashukia Spika Sitta na Werema
broken-heart.jpg
Hemed Kivuyo, Arusha

MBUNGE wa Karatu Dk Wilbrod Slaa, amewashukia spika wa bunge, Samuel Sitta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Warema kuhusu rais kudanganywa katika sheria ya matumizi ya fedha katika uchaguzi.

Kutokana na hali hiyo,amewataka waache kutoa majibu mepesi kwenye hoja nzito tena bila kufanya utafiti.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametaka sheria hiyo irudishwe bungeni katika kikao cha 19 kinachotarajiwa kuanza Aprili ili kifungu ambacho rais Jakaya Kikwete amekisaini bila kujadiliwa bungeni, kiondolewe.

Katika barua yake aliyomwandikia spika wa bunge kulalamikia kauli hizo, Dk Slaa alisema kifungu hicho namba 7(3) cha sheria ya uchaguzi kimemhadaa rais Kikwete na hivyo kwenda kinyume na demokrasia.

"Hivyo,Naomba Serikali ichukue hatua kuwasilisha "miscellaneous Amendment" katika Mkutano wa 19 yaani Bunge la Aprili, ili kifungu hiki ambacho ni kinyume na demokrasia kiondolewe kwenye aheria ambayo rais ameisaini,"inasema sehemu ya taarifa ya Dk Slaa

"Angelikuwa amesoma Mhe. Spika angelikuwa mwangalifu kutamka aliyoyatamka. Mheshimiwa Spika anakiri kulikuwa na mjadala, lakini hakutamka mjadala ulihusu nini, na wala hakumnukuu mwenyekiti wa siku hiyo ambayo alikuwa Mhe. Naibu Spika alitoa maagizo gani.

"Ni hatari kwa viongozi wetu kutoa matamko kwa mambo mazito bila kufanya utafiti angalau mdogo. Mhe. Spika atakubali kuwa kwenye Hansard, hakuna popote ambako imejadiliwa achilia mbali kukubaliwa kuwa timu ya kampeni itathibitishwa na msajili(kwa mgombea urais) au katibu tawala (kwa mgombea ubunge) au na mtendaji wa kata kwa (mgombea udiwani). Hii ni dhana mpya kabisa, siyo tu haijajadiliwa wala haikufikiriwa kama Hansard inavyoonyesha," alisema Dk Slaa.

Alifafanua kilichokuwa kimejadiliwa katika mjadala huo ni hoja ya mbunge wa Bariadi Mashariki Andrew Chenge ambaye alitaka kufanyia mabadiliko hoja ya mabidiliko kuhusu pendekezo la serikali kwamba kifungu cha 7(2) na alitaka makundi ya sanaa yaingizwe baada ya neno "Voters".

"Hivyo ni vyema naye Spika akiri tu kuwa utaratibu wa kutunga
sheria umekiukwa. Haifai kubishana kwa sababu wakati Hansard ndiyo ushahidi wa wazi wa jambo hilo, anaeleza katika barua hiyo.

Dk Slaa anaeleza kwamba anamwona mwungwana mwanasheria mkuu wa serikali kukiri mapungufu hayo, lakini anasikitishwa na kauli yake kwamba anastushwa na kauli ya Dk Slaa.

"Kwanini mwanasheria mkuu aanze kufikiria siasa badala ya kuchukua Hansard,Bill iliyowasilishwa Bungeni, na kuisoma ili kujua kilichoazimiwa na Bunge. Huu ndio utafiti siyo kukurupuka kujibu mambo mazito, hata kama anatumia nafasi yake ili kuficha makosa yake, hali hii haikubaliki katika dunia ya sasa kwa sababu watu ni waelewa.

"Hivyo,Naomba Serikali ichukue hatua kuwasilisha miscellaneous Amendment" katika ,kutano wa 19 yaani Bunge la Aprili, ili kifungu hiki ambacho ni kinyume na demokrasia kiondolewe kwenye Sheria ambayo Rais ameisaini.

Dk Slaa aliyasema hayo huku akionyesha nakala ya barua aliyomtumia Spika wa Bunge, Samuel Sitta akimtahadharisha kuwa makini na matamshi ambayo amekuwa akitoa mara kwa mara bila kufanya utafiti wa kina. Alisema baadhi ya vyombo vya habari viliwanukuu kwa nyakati tofauti Spika Sitta na Jaji Werema wakisema kuwa hawaamini na hawadhani kama tuhuma hizo zina ukweli na kwamba Dk Slaa anapaswa kuelimishwa zaidi ili kufahamu vifungo hivyo vya sheria ya gharama za uchaguzi na kudai kuwa kauli zao zinakiri na kukataa hivyo kujichanganya .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom