Sisiem nimeamini ni wanafiki sana

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,705
Lazaro Nyalandu leo wanadai kuwa alitumia helcopter ya mwekezaji aliyekuwa ana tuhuma za ujangiri kufanyia kampeni zake za kuwania kuteuliwa kugombea uraisi na katika kampeni za ubunge.
Pia wanadai alikataa kusaini ili hotel zilizoko mbugani ziwe zinalipa kodi kwa serikali.
Mimi sina tatizo kama amefanya haya basi ni kweli alikosea na alitumia madaraka vibaya kuna haja ya kuwajibishwa..
Ila ninachojiuliza, hayo yametokea 2015 kurudi nyuma, na ni wazi sisiemu walikuwa wanayaona na wanayajua, ila kwakuwa alikuwa mwenzao basi wakayakalia kimya.
Leo ni zaidi ya miaka miwili imepita toka uchaguzi umeisha, ila kwa kipindi hicho chote hakuna aliyeongea kuhusu suala hili.
Ila Nyalandu kahama chama haijapita hata mwezi ndipo wameyaongea haya.
Je kutakuwa kuna madudu mangapi wana sisiemu viongozi wanayafanya ila hayasemwi kwakuwa bado hawajahama chama?
Nahisi hii nikiwatisha viongozi wengine wasithubutu kuhama sisiemu wakihama basi tuhuma zao zitaibuliwa ila wakibaki wako salama.
Nilisikia mwenyekiti wa sisiemu singida anadai Nyalandu alikuwa mzigo kwa chama na alikuwa anashinda ubunge kwa kutoa rushwa.
Nikajiuliza sasa kama walilijua hilo kwanini hawakuita TAKUKURU, wamkamate?
Ina maana walikuwa wanamlinda kwakuwa alikuwa sisiemu?
Je ni wana sisiemu wangapi wanalindwa kwa style hiyo na wanapita kwa kutoa rushwa ila inakuwa ni halali mpaka pale wanapoama chama?
Kweli TZ ya viwonder
 
Mbona haya mambo ni ya kawaida sana katika Siasa,haswa za Afrika.
Dr Slaa alipoondoka Chadema ziliibuliwa shutuma lukuki na Chadema. Wakati alikuwa ni Katibu mkuu wa Chama na mgombea URAIS kupitia Chadema. Siasa na Unafiki ni kama Uji na mgonjwa.
 
Hivi kwan takukuru siku hizi mpakaa waambiwe watu wakuwachunguzaa au wanaamua wenyewe??
 
Hivi kwan takukuru siku hizi mpakaa waambiwe watu wakuwachunguzaa au wanaamua wenyewe??
Kama uliwahi ama wewe ni kiongozi ndani ya sisiemu au serikalini mpaka waambiwe mkuu..
Kwani wewe ulisikia wamemchunguza wala kumkamata nani ambaye ni kiongozi au aliwahi kuwa kiongozi ndani ya sisiemu au serikali pasipo kuambiwa?
 
Kama n ccm haijaoza ila
Imeoza³ maana huu n ingese haki ya nani
Wanachokifanya ni kutuona ss n wehu kama wao maanina

Sasa 2020 kama watz tuko sawa tukatae hichi chama wakubwa aaaah imekuwa too much
 
Hawana akili kabisa, kwaakili za kawaida huwezi kufanya kama alivyofanya Kigwangala. Zaidi ya kushindwa kufikiri na kuona Watanzania wote ni wajinga na tuna akili kama zao na uwezo mdogo wa kufukiri kama wao. Upuuzi mtupu.
 
Back
Top Bottom