Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Makundi mengi ya wananchi wameshaitwa ikulu kuongea na mheshimiwa raisi. Sisi watumishi wa umma tutakopitwa tutakuwa na mapendekezo yafuatayo:
1. Kufuta vyama vya wafanyakazi ili asilimia mbili (2%) wanayochukuwa tuiongeze kwenye PAYE iende serikalini. Tsheti tumezichoka, serikali inaweza kututengenezea shati zenye nembo ya taifa.
2. Kutoa mshahara tarehe 31 isipokuwa tu kwa miezi inayoishia 28, 29 au 30. Zinapotoka kabla ya hapo, hesabu (naturally) inaharibika.
3. Fursa za ajira za muda mfupi kama kusimamia uchaguzi, wapewe wasomi wasiokuwa watumishi wa umma. Watumishi tayari wana riziki zao, wanaziba riziki za watu wengine.
4. Kufuta posho za madaraka za wakuu wa idara, wakuu wa vituo, wakuu wa shule na walimu wakuu na badala yake zigawanywe kwa watumishi wote kwasababu kinachotokea ni ubaguzi na utengano.
5. Kila idara iwe na sare za kazi, mfano waganga wana sare, polisi, magereza, jwtz, wanasheria, mahakimu na wengine. Hii itumike pia kwa watumishi wengine kama vile walimu. Itasaidia kupunguza gharama za kununua nguo mara kwa mara kwasababu ukiwa na sare kazi ni kufua tu.
6. Kupandisha madaraja kwa watumishi wote wenye sifa hata walioko masomoni ilimradi tu kabla ya kwenda walikuwa wamekaa miaka 3-4 katika vituo vyao vya kazi.
7. Kutengeneza mfumo wa uhamisho (online) utakaowezesha kila wilaya kubaki na idadi ileile ya watumishi yaani akihama mtu anaingia mtu.
8. Kupandisha kima cha chini cha mshahara siyo muhimu, muhimu ni nyongeza ya kila Julai hata kama ni elf 20 kila mwaka.