STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,633
- 16,601
(Nimeiona sehem)
Tazama jasho linavyomtoka topeni. Yuko kazini. anapigana na maisha apate senti kadhaa. Ni MWANAUME! Ameumbwa kupambana na kutafuta na akitoka hapo ana ujira unaosubiri kugawanywa. wazazi au walezi, majukumu huku na kule, bado mambo yake binafsi. Ni mwanaume huyu
Lakini juu ya yote upo wewe anayekuita mpenzi, mke au vyovyote, upo wewe ambaye anapotaka kuupumzisha mwili wake, wewe unamueleza
"Bebi nahitaji elfu 60 nina shida nazo"
Mwanaume huyu anakuomba usubiri asubuhi au siku mbili mbele kisha atakupatia au atajiinua kwenda kukuchukulia
Pengine atakwambia anazo kidogo akupatie hizo kwanza kisha atamalizia zingine! anakupatia ulichoomba. Umewahi kumshukuru mwanaume anayetoa chochote mfukoni mwake akakupatia kwasababu wewe ni mwanamke wake? Ni wajibu wake ndiyo lakini wangapi hawatimizi wajibu wao?
Umewahi kumwambia unampenda vile anajinyima kwa ajili yako? Unadhani hizo pesa huwa hazina kazi? Huwa hana watu wa kuwapa? Hivi mtu anayekupatia kitu kulingana na uwezo wake unapomdai kitu kikubwa nje ya uwezo wake huwa umewahi kufikiria unamvuruga kiasi gani?
Kama kuna mtu anajinyima kwa ajili yako. Haijalishi ni mamilioni au hata elfu 5.... mshukuru Mungu kwa ajili yake na muombee azidi kufanikiwa! Au anaacha hela ya matumizi kila siku, aisee hebu mkande miguu na mikono siku moja. Huyo ndie MWANAUME!!
Na ukiona mwanaume wako hakupi kitu ilhali anachapa kazi kisa na wewe unafanya kazi, kuna mwingine/wengine wanapewa! Hakunaga mwanaume bahiri duniani labda tu mtekaji wake hajamfikia bado!
Pongezi kwa wanaume wote mnaotunza wanawake bila kujali vipato vyao. Mungu awafute jasho!
Sent using Jamii Forums mobile app