Sisi tusio na uwezo tutahemea wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi tusio na uwezo tutahemea wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwakajila, Jul 17, 2012.

 1. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Leo asubuhi nilikuwa ninamsikiliza msemaji wa TCRA akielezea kubadilishwa kwa mfumo kutoka analojia kwenda digitali huku akifafanua kwamba tunahitaji kuwa na ving'amuzi ili tuweze kuona chaneli mbalimbali kwenye runinga zetu.Nashindwa kuwaelewa hawa mabwana kuhusu kutuangalia sisi wa kipato cha chini wenye antenna zetu zu tubelight tutapata taarifa mbalimbali kupitia nini kama hata chaneli za TV mnatunyang'anya?Nasema hatuna uwezo wa kulipia hao star times,easytv,zuku potelea mbali DSTV..Mnatuongezea gharama za maisha wakati yenyewe yameshapanda..
  Mnatunyanyasa....
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,370
  Likes Received: 2,990
  Trophy Points: 280
  Huu n mzigo mzito kwa watumiaji wa tv,mbaya zaidi mamlaka inasema tu bila kujua watu hawalingani uwezo. Tuseme ni DHAIFU au LIWALO NALIWE.......
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,482
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Yuko bwana mkubwa mmoja wa zamani sana akiitwa Dialo aliwahi kusema nyama zote zitauzwa supamaketi na sio mabucha yetu yale ya magogo....BAHATI YAKE sili nyama!!
   
 4. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,004
  Trophy Points: 280
  Nikupe hii: LIKE!
   
 5. next

  next JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 601
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  mabadiliko yoyote hasa yanayo husisha kuongezeka kwa gharama, watanzania tumekua wagumu sana kuyakubali hata kama ni mazuri na gharama si kubwa
  gharama ya king‘amuzi ni kati ya 70,000 na 150,000.’ na malipo ya mwezi ni kati ya 9,000 na 40,000 (ukiacha dstv)
  hapo wewe unajiweka kundi la wasio na uwezo, ila unamiliki sim ambayo inauwezo wa internet hivyo haipungui 70,000, na unatumia zaid ya 10,000 kwa shughuli zisizo kuingizia kupato.
  me nakushauri uangalie jinsi ya kumiliki king’amuzi chako. changamoto iliyopo ni kuhakikisha makampun yanayohusika na kurusha haya matangazi kupitia ving’amuzi warushe all local chanells as mandatory na waweke ushindani kwenye chanels za nje.
   
 6. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  next hii ni biashara ya watu bwana wakubwa hao wanaona watauzaje wewe unaishi wapi unazungumzia 70,000/=tsh ni kubwa sana kumbuka vitu hivi havina giarantee wewe ndugu mshukuru mungu ninakuambia ni wachache sana wataaford vijijini tumewapoteza na tv zao ndugu yangu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Next sidhani kama unaelewa kipato cha mtanzania wa kawaida shukuru hiyo 70,000 unaipata sisi wngine ndio mshahara wetu wa mwezi kwa muhindi hizi posts ni internet za ofisini tu na sio cmu..maisha ni magumu ndugu yangu hiyo 9000/=kwa mwezi ninaitoa wapi?hiki kingamuzi ni kutubebesha mzigo tusiouweza kila kitu kimepanda,unga,mchele nk bado unadai haya ni mambo mazuri kwa gharama kidogo zile antenna zetu zina shida gani?siwezi sema sana kwasababu uwezo wetu unapishana..ila jua kwamba hali yetu watanzania ni mbaya sana na hatuwezi hata hiyo milo mitatu..
   
Loading...