Sisi tunaiga muziki wa Amapiano na siyo wao kuiga Visingeli vyetu

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Bila Shaka midundo ya Amapiano ndio habari ya Mjini kwa Sasa midundo ikiwa na Asili ya Afrika kusini.

Wasanii wa Kibongo nao kama kawaida wamefwata upepo na kuiga midundo hiyo Kongole kwa Kaka Alikiba katika Albamu yake sijasikia dundo lolote la kiamapiano kasimamia lile analoliamini yeye labda kama badaye atabadilika.

Kwaito na sasa Amapiano naweza kusema ni kama identify ya muziki wa Kisouth Afrika zikipigwa ngoma hizo unajua kitu cha madiba tu hicho.

Ishu ya msingi kwanini wasanii wetu hawa kina Sholo mwamba,dulla makabila,man fongo na wengine wengi wanaoimba mziki wa singeli wasifanye wanamuziki wa South Afrika wakaiga Visingeli vyao kama wao wanavyoiga Amapiano zao,Sidhani kama utaenda Jiji la Pretoria au Capetown na kusikia Visingeli vinagongwa kama sisi tunavyocheza na dundo za kiamapiano huku kwetu.

Mpaka hapo wasanii wetu wanakwama pakubwa na kuonekana wanashindwa kusimamia kile wanachokiamini na kuwa kama Bendera fwata upepo,Ingependeza siku moja wasanii wa nje waige midundo yetu na sio sisi kila siku kucopy na kupaste tu midundo ya nje.

Kazi hii ni mtambuka kuanzia kwa maproducer wetu,wasanii wetu na wote wanaohusika na musiki wetu I mean wadau kutengeneza vyetu na kuvipa vipaumbele.

Weekend Njema.
 
Back
  1. Hemed Maneti
  2. Suleiman Mwanyiro
  3. Marijan Rajaab
  4. Suleiman Mbwembwe
  5. Joseph Maina
  6. Muhidin Gurumo
  7. Moshi William
  8. Mwalimu Enock
 
Back
  1. Hemed Maneti
  2. Suleiman Mwanyiro
  3. Marijan Rajaab
  4. Suleiman Mbwembwe
  5. Joseph Maina
  6. Muhidin Gurumo
  7. Moshi William
  8. Mwalimu Enock
Walisimamia musiki wao na ukawatoa walikataa kuwa bendera fwata upepo.
 
Imeharibu mpaka Kaswida misikitini, upigaji dufu unamezwa na midundo bandia
Kila kitu ni modern siku hizi Mara modern taarabu,Modern kaswida,Modern Bongofleva kumbe kazi yao ni kuiga tu.
 
Naunga mkono hoja 💯💯

Sema ndo hivoo...zina amsha popo hatariii...
 
Hili huwa linaniumiza kichwa saana, hivi tunashindwa kuwa na identity yetu itakayotutambulisha duniani...

SA wana kwaito ikipigwa popote duniani inajulikana hii ni kwaito from SA.
Lingala ya DRC ikipigwa tu unajua DRC hii..
Nigerian wana yao pia zikipigwa tu unajua Nigerian...

Bongo tunayumba mara lingala, mara amapiano, mara nigerian....tukomae na singeli tuiboreshi iwe yetu au dance yakina late TX Moshi, Gurumo, Sikinde, Matimila nk... tukishindwa kabisa tukomae na Baikoko basi tuiboreshe..
 
Ndio maana miziki yao inaishi kwa muda mfupi Ina half life ndogo sababu ya kuiga kila kitu,Tanzania its like dampo kwenye suala la mziki kila style ikianza nchi ya kwanza kuiga ni Tanzania.

Nafikiri lingewekwa hata shindano la Kitaifa kumtafuta producer bora atayekuja na dundo Kali la kutambulisha mziki wetu.
 
Kweli kabisa tunakwama sana bila identity..
Maproduce wakipewa hii kazi kwa kuangalia ngoma za makabila yoote then wakaja na mdundo combined wanaweza kupata kitu..
 
Hivi mziki wetu si ni midundo ya pwani.. Taarabu. Tuiboreshe tu.
Angalia Bibi Kidude alisimamia kile anachokiamini na bado akala tuzo kibao siku hizi kila kitu ni modern Mara modern taarabu,taarabu za zamani unasikiliza unapata Hisia kabisa.
 
Hivi kweli singeli ifike mahali inajulikana kimataifa ndo nyimbo ya Tanzania si mnataka tunaoishi humu ndani wote tuonekane machizi.

Nyimbo gani zile ni kupiga tu makelele mwanzo mwisho kama mkimbiza ngedere mashambani.

Hao jamaa wa Africa kusini wanacho win ni kucheza na beat ambazo zina fanya watambulike zaidi ila kwenye nyimbo wanaimba kidogo. Sasa singeli ni makelele mtindo mmoja.

Japo napenda vyakwetu nchini ila Singeli sijawahi ielewaga hata siku moja.
 
Sawa kama ni makelele toa mawazo basi warekebishe wapi Je makelele yanatoka kwa msanii au kosa ni producer anashindwa kupiga vyombo vizuri Je kama sio singeli kwanini isiwe mchiriku/mdananda au taarabu.
Tunakosea wapi
Kumbuka hata Amapiano nyingine zina kelele boss
 
Kanuni ya maendeleo ktk maisha ni mdogo kumuiga mkubwa na siyo kinyume chake.Ndiyo maana mtoto akifanya jambo zuri la kikubwa hupongezwa na kuambiwa ana akili nyingi lakini mkubwa akifanya jambo la kitoto hudharauliwa. Hivyo usitegemee SA au Nigeria au USA au ulaya wakuige wewe bali wewe ndiyo unatakiwa kuwaiga wao.
 
Back
Top Bottom