Sisi tumelala, Rwanda na wanaleta Madaktari wao Kusoma Tanzania

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Sielewi shida ni kwenye miti mingi hakuna wajenzi au la.

Kila mwaka Rwanda inaleta wanafunzi kibao (hususani wa udaktari bingwa) kuja kusomea kozi mbalimbali kwenye vyuo vyetu Tanzania.

Nenda Muhimbili ukaone kozi za Hematology, Pathology, Radiology, Pediatrics na kadhalika zikiwa na wanafunzi kibao toka Rwanda. Hapo hujaenda UDSM wala SUA.

Sisi tunalalamika hatuna wataalamu. Tunaacha madaktari bingwa wa kozi fulani wakizeeka bila kutumia ujuvi wetu.

Nadhani shida kubwa tuliyonayo ni katika kuweka vipaumbele...
 
Shida sio vipaumbele,shida tumetanguliza SIASA KWANZA MENGINE BAADAE. TATIZO HILI(Tunaua morali za wataalamu)
 
Sasa mtoto wa mkulima anawezaje kwenda kusoma MUHAS bila mkopo kwa miaka 5?

Mtu katoka Nachingwea huko kaenda DSM
-Hana mkopo
-Hana Hosteli
-Hana ndugu Dsm
-Hana uwezo ..

Tz tuweke miundombinu ya kusoma kabla ya kulalalmika
 
Rwanda wamekuwa na huo mpango kwa zaidi ya miaka saba sasa, kufikia 2020 watakuwa wamekamilisha Phase One ya mpango wa miaka kumi wa kutengeneza wataalamu wao katika fani za sayansi katika vyuo vikuu vya Tanzania.
Namibia nao wameanza huo mpango mwaka huu, tayari wameleta zaidi ya wanafunzi 20 kuja kusomea udaktari bingwa pale KCMC.

Hawa wenzetu wako serious sana kwenye mambo yao ya maendeleo.
Sisi bado tunaendelea kuwachukua Maprofesa na kwenda kuwapa ukuu wa wilaya na ubunge wa kuteuliwa badala ya kuwatumia kuzalisha wataalamu wengine wazuri.
 
Sielewi shida ni kwenye miti mingi hakuna wajenzi au la.

Kila mwaka Rwanda inaleta wanafunzi kibao (hususani wa udaktari bingwa) kuja kusomea kozi mbalimbali kwenye vyuo vyetu Tanzania.

Nenda Muhimbili ukaone kozi za Hematology, Pathology, Radiology, Pediatrics na kadhalika zikiwa na wanafunzi kibao toka Rwanda. Hapo hujaenda UDSM wala SUA.

Sisi tunalalamika hatuna wataalamu. Tunaacha madaktari bingwa wa kozi fulani wakizeeka bila kutumia ujuvi wetu.

Nadhani shida kubwa tuliyonayo ni katika kuweka vipaumbele...
Vyuo Vya Tanzania Vimejaa Maseneta Wenye Vijiba Na Ghiliba Tu Zisizokuwa Na Mpango, Yaani Mtu Unaweza Kuzuiwa Kusoma Kozi Au Chuo Fulani Bila Sababu Za Msingi.

Vyuo Vya Tanzania Vinaongoza Kwa Kuua Ndoto Za Watu.
 
Sasa mtoto wa mkulima anawezaje kwenda kusoma MUHAS bila mkopo kwa miaka 5?

Mtu katoka Nachingwea huko kaenda DSM
-Hana mkopo
-Hana Hosteli
-Hana ndugu Dsm
-Hana uwezo ..

Tz tuweke miundombinu ya kusoma kabla ya kulalalmika
Hakuna Mwanafunzi Undergraduate MUHAS Asiye Na Mkopo, Toa Mifano Yenye Uhalisia
 
Kama wanakuja kusoma hapa kwetu yaani Wataalamu wetu ndio wanaowafundisha hakuna tatizo!. Ila sema tunaogopa kudukuliwa Siri za Taifa letu!!
 
Wewe si bure unaweza kuwa taahira akili yako imeshindwa kabisa kujua haya

  • Wanaleta wanafunzi tuna vyuo bora wasionavyo
  • Wanaleta wanafunzi wao sababu Tanzania tuna wataalamu wabobevu
  • Wanaleta wanafunzi Tanzania sababu elimu yetu ni bora kuliko ya majirani zetu wengine.
  • Wanafunzi wa kigeni Wanaleta pesa kwenye vyuo vyetu na kukuza uchumi wetu.
  • Wanafunzi wanapata accommodation Tanzania ambapo pesa inaingia kwa wenye nyumba, vyakula, stationery na mahitaji mengine
  • Wanakuza jina la Tanzania kwenye sector husika nje ya mipaka ya Tanzania
  • Ajira ya uhakika kwa University stuff na auxiliary stuff kwenye enrollment ya course yao katika nyanja tofauti Tanzania...........
Haya yote akili yako haijayaona?
 
Hakuna Mwanafunzi Undergraduate MUHAS Asiye Na Mkopo, Toa Mifano Yenye Uhalisia
Nikishangazwa na michango ya wachangiaji wengine, tena wenye kuleta picha kuwa ni "wasomi"...
...ni swali najiuliza, tunaweza boresha hali ya taifa letu kwa kuchanganya uzushi, na majungu kwenye tafakari zetu?
 
Back
Top Bottom