Sisi sote ni mafisadi/wapiga dili kwa nini tunamnyooshea tu lowasaa kidole?

tubadilike-sasa

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
681
167
SISI SOTE NI MAFISADI NI WAPIGA DILI KWA NINI TUNAMNYOOSHEA TU LOWASAA KIDOLE?

Kwa mujibu wa tafsiri ya Kamusi ya Swahili-English Dictionary neno fisadi tafsiri yake kwa kimombo ni; libertine, seducer, destroyer or evil person.
Sasa ukiangalia kuanzia mfagizi katika ofisi hadi Rais wote sisi ni mafisadi kwa namuna na viwango tofauti. Kwa mfano,kama Rais akimteua Mkuu wa Wilaya ambaye watu wanajuwa kabisa hana uwezo na alikuwa kimada wake,huo ni ufisadi.

Mtu si mdokozi wa pesa. Mwaminifu ofisini, lakini anamshawishi mfanyakazi wake wa ndani wa kike au wa kiume na kufanya naye mapenzi. Huu ni ufisadi.

Kushikwa na trafiki halafu badala ya kulipa faini,mkavutana pembeni ukampatia elfu 2 au 5,huu ni ufisadi.

Wafanyakazi wengi wa serikali mishahara midogo ambayo haiendani na hali halisi ya maisha na huvyo huangalia na kuchungulia kuona apige dili wapi.Hata karani kuangalia vocha yako ya malipo imefikia wapi,anadai umpe elfu tano. Huu ni ufisadi.

Kwenye makampuni binafsi makubwa na madogo kote huko ni dili 24/7.Nakupa hii kazi ile mimi niwekee cha juu. Huu ni ufisadi.

Ukienda kwa wenyeviti wa serikali ya mtaa kumtaka akutambulishe kule NMB bank ili ufungue akaunti,akeshaandika tena anakuangalia kwa macho mawilimawili huku mate yakidondoka mdomo,anasubiri buku 2 au 5. Huu ni ufisadi.

Ukitaka mkopo pale benki sharti afisa mkopo mkubaliane. Anakuuliza,je mkopo ukitoka utanipa sh ngapi? Huu ni ufisadi

Wewe ni mjasirimali au mfanyabiashara. Unapata tenda za serikali au Halmashauri. Ukipona tenda yako ikapita bila bila kutoa tipu,lazima utakamatwa wakati wa kutoa huduma au kuuza bidhaa. Hapa tunahitaji 10% na ili uendelee kufanya kazi ile lazima utoe na usipotoa kazi hupati anapewa mwingine. Maan katika kujaza quotation. Huu ni ufisadi.

Ukitaka mkopo wa chuo kikuu toka pale bodi,wewe toa kitu kidogo na jamaa akishavuta,anakuambia tayarisha hiki na kile akiingia kwenye komputa yake anabofya mara tatu, nay a nne unaona mkopo 100%. Lakini wewe mwenyewe hauna vigezo na umepata. Huu ni ufisadi.

Unamtongoza mke au mme wa mtu na kufanya naye ngono. Na kuanza mchepuko,unaharibu hata bajeti ya nyumabi kwako. Afu kwa sababu sasa bajeti imekuwa kubwa unaangali pale ofisini upige dili wapi na unaanza kudokoa. Huu ni ufisadi.

Wewe ni mwalimu unamrubuni mwanafunzi wako ambaye vijititi vyake vimeanza kuchipua,ukaingia tama kama fisi na ukalala naye. Huu ni ufisadi.

Una mfanyakazi wako wa ndani uwezo wa kumlipa vizuri unao lakini unamlipa kiduchu tu na manyanyaso mengi. Huu ni ufisadi

Sitaki kuandika juu ya EPA,ESCROW,MEREMETA,RADAR(ya nyoka wa makengeza), Migodi ya madini, vitalu vya Gesi na Mafuta, Vinara wa Madawa ya kulevya,nk. Wote huu ni ufisadi.

Kwa hiyo ukichunguza tu kidogo unagundua kwamba Tanzania imeoza ina uvundo,mdogo kwa mkubwa. Kiongozi na anayeongwa. Wote tu mafisadi na tofauti ya ufisadi wetu ni aina na ukubwa tu.

Hivyo kumnyooshea Lowassa kidole wakati vidole vitatu vinakuelekea wewe ni sawa na ngamia kusweka kichwa chake katika mchanga akijificha kwamba haonekani wakati matako yapo juu.

Na kwa kuwa sisi sote tu na ufisadi kuanzia wale wanaomtukana majukwaani hadi yule aliyekaa kimya ofisini akisubiri 10% yake ingie baada ya supplier wake kuandikiwa cheki,tumemfanya Lowassa aonekane kama mti mzuri wa mwembe. Wenye embo dodo zilizoiva vizuri. Na sasa watu wanarusha mawe huko kwa fujo.

Na wengi sana wamemnyoshea vidole. Kila watu 10 wanonyoshea vidole 30 wanajinyooshea wao,wakimnyooshea 1000. Yaani kila wanavyofunua chupi ya Lowassa mara moja za kwao zinafunuliwa mara tatu zaidi!

Na katika Biblia tatu(3) ni namba ya ufufuo. Kristo Yesu alikaa kuzimu au kaburi na siku ya 3 akafufuka na kuishinda mauti na kuzimu. Na tendo hili lilifanyika mara moja(1) tu. Kwa hiyo kila fisadi anayemnyooshea kidole Lowassa kwa nia ya kumzamisha kwa sababu kuwa yeye ati ni fisadi,wakati huyu anayemnyooshea kidole naye ni fisadi(Mungu anamjua ufisadi wake),anampeleka Lowassa kuzimu mara 1 na na kumfufua mara 3 zaidi.

Na mfano ni huu hapa. Baada ya sakata la Richmond,wachawi wake walidhani kuwa huyu amekwisha. Wakaanza kuimba na kumnyooshea vidole kuwa fisadi huyoo. Kila walipofanya vile yeye alianza kufufuka toka kuzimu. Wakitaja na kumzamisha kwenda kuzimu mara 1000 yeye anafufuka mara 3000 zaidi. Nyota yake ikaanza kung'aa tena na tena.

Hata sasa kila mbinu inayotumiwa na wapinzani wake kumzamisha inafeli inaangukia pua. Nyingine zinafeli kabla hata hazijaanza. Lowassa akizamishwa mara 1, yeye anafufuka na kung'aa mara 3 zaidi. Tafakari hili kupitia lensi ya ufisadi uliowahi kuufanya.

Nimalizie kwa kusema kwamba tukifunuana chupi kama ambavyo viongozi wanafunuana sasa hakuna aliye safi. Ni kama ukipanga wanaume 100 halafu ukawaambia,haya wote vua viatu. Wengine wataanza kusuasua.Halafu wakesha kuvua,harufu ya undo ni mbaya, mbaya sana. Na utashangaa unajiuliza hata huyu jamaa soksi zake zinanuka na kuwa na matundu kama ya kupita panya! Hamuna aliye safi katika ufisadi!

Tumpigie Lowassa kura,maana kapita katika tanuri la moto. Na sasa amekuwa dhahabu safi. Si malaika ila amejiandaa kuwa Commandaer-In-Chief. Kuhusu Magufuli sina tatizo naye kama mtu.Hakujiandaa kwa kazi hii. Alioteshwa ndoto na wenye chama na hakuota ndoto ya kutaka siku moja awe Rais wetu. Na yumo katika gari ya mwaka 47 (Chevrolet) iliyonoki injini. Na injini hazipo madukani. Sasa kwa nini mtu uingie gharama ya kuagiza injini nyingine "custom made" toka Marekani kwa bei gali wakati magari toka Japan yapo tele sokoni? Hiyo Chevrolet ya mwaka 47 ni kuiweka makumbusho.

Tuipumzishe CCM maana injini yake imenoki,ipate nafasi ya kujisuka upya na kurudi katika misingi yake tena.Ni upevu wa akili,hekima na busara pale chama kinaposhindwa kuleta matunda, " kudeliver" kiwekwe benchi ili kirudi na mawazo mapya na fikra mpya. Nothing personal!
 
Wewe acha tena acha kabisa, mimi simo katika mafisadi Tanzania, na labda wewe na ndugu zako. Hii hata mkude simba, hakumkatalia moja kwa moja mwanawe alipoomba kuelezwa chanzo cha Binaadamu, alimuelekeza vizuri tu. Ila mtoto akamwambia babaake alichoambiwa na mama yake, kuhusu kuumbwa kwa Binaadamu, Mkude hakumkatalia alipoelezwa na mtoto wake kuwa yeye ameambiwa na mama yake chanzo cha Binadamu ni manyani, alimjibu yuko sawa labda ukoo wao. na hii ya kwako inawezekana ukoo wenu ni mafisadi siwezi bisha.
 
Back
Top Bottom