Sisi ndio wanaume bwana!

Bishanga,alieanza kukosa ni eve sioa adam.Ndo maana akasema huyu mwanamke ulienipa ndo amenisababisha,in short mwanamke ndo mwanadam wa kwanza kutenda dhambi,hizo point zingine hazina kitu kama ukisoma vizuri uzi wa Aspirin,utaelewa maana ya MWANAUME!
 

...nice one mwj1....jino kwa jino....ng'ang'ana hapa hapa mpaka wakukimbie hawa...
Mwanaume hajisifii bana, mwanaume anasifiwa kwa uanaume wake!



....pamoja kamanda, ile sredi yako sikuweza changia mdahalo wake kwasababu ya muda,
lakini hapa tutabanana na hawa wenzetu wanaojisifia u kidume wao...

Yaani kabisa unaweza simama hadharani ukasema uanaume wako wakati rohoni huna uhakika
kama mtoto/watoto ni wako au sio wako?.... ebana mimi najiskia kumwagia tenki zima la petroli kwenye moto huu!
potelea mbali
afe aliyekuwamo na asiye kuwamo...
 

Loh hii attack Mbu wangu itakucost darling but ni ukweli kabisa. It is a woman ambaye anwezakukuhakikishia uanamume wako. Unaponipa starehe kwa six ninapopiga kelele unajiaminisha kuwa umeniweza?? Kwako sipindui?? Una uhakika gani kama kelele zangu ni za kweli?? Mbu amezungumzia swala la watoto, unawezapita barabarani na kujisifia kifua mbele kuwa una watot kadhaa wa kiume na kike, my son, my daugther ilhali huwezithibitisha kuwa ni wako kweli (Unless kwa msaada wa DNA)- Achilia mbali wana unawezathibitisha kwa DNA

Haya huyo mwanamke unayedai kummiliki una uhakika gani?? Unawezatimiza majukumu yote, chakula n.k wakati amani na furaha iliyopo nyumbani kwako unayojivunia nayo ni kwa msaada wa Shamba boy, family driver au jirani yako pembeni.

Eh nalog out nsijemwagiwa radhi na Babu bure.
 
MJ1 akhiiiiiiiiiiiii!!:smash: na zawadi yako ya chupa ya wine shiiiiiiiiiiiiiii usiwaambie sana waache waendelee kujiaminisha mpenzi wangu.


 

...haya sasa, ndio utetezi gani huo?

mwanaume anatakiwa kusimamia maamuzi yake bana!
hakuna cha oohh, huyu ndio kanisababishia...UANAUME ni mwiko kumtafuta mchawi
mfano; leo hii mbu nifumaniwe na mke wa mtu (God Forbid) unadhani nitajitetea ati sio kosa langu,
mie nimeletewa tunda nile?...

...hata kama kaja na mabaunsa wake, nimejikubalisha kufa kishujaa bana, ama zake ama zangu!
 

Mbu wakakti wa kushambuliwa na Babu na watu wake sitakuwepo kukutetea
Hapa kwa kweli ni balaa wakija hao wanaosema kidume ni lazima utoke nje au kidume lalzima ukae baa mpaka usiku
Kwa kweli sitakutetea mkuu
 
Mbu,msingi wa point yangu haikua excuse ya mwanaume bali nilikua namjibu bishanga kuhusu kosa la Adam na Eve,lakini kumbuka kuwa lile tunda alilokula Eve halikuleta shida mpaka alipokula Adam,hiyo inaonesha ukuu na UANAUME wa Mwanaume maana yake nini!
 

Hahahahahhahahahhahahahahahahahhaaaaaaaaaaa......................ohhh my God. Umenifanya jioni yangu iwe ya vicheko visivyo na mwisho. Asante mwaya.
 

...la ...la ...la usikimbie bana...

endeleza mashambulizi hapa, maana haya mambo bana bila uwazi na ukweli huwa tunaishia kujidanganya sana
kwenye viti virefu!....

maisha ni script ya sinema ambayo kama director atakuwa mwanaume, starring ni mwanake and vice versa....
sasa usiombee ukute huyo starring ndiye aliyeidhamini hiyo production nzima...yaani hata director akileta za kuleta
starring anamtimua kazi "kanumba!"

Mtazamo wangu kimaisha bana umeathiriwa na matukio mengi ya kiukweli na kihalisia kuliko dhana na hekaya za kusadikika.
The real man is humble....asiye na makeke wala makuu,...asiyetafuta kujikweza wala kujisifia...
Mwanaume wa kweli uanaume wake unaonekana kwa vitendo... vya ndani na vya nje...
sio anakuwa double faced, ....uani anajiliza anaonewa, hadharani anatunisha kifua ati yeye ni mwanaume wa shoka!


 

Mkuu huo ndio ukweli halisi ambao wanaogopa kuusema akina Babu
mambo yanayotendeka ndani ya maisha ya watu na walikopitia ndio haya wanayotuletea ila uhalisia wa maisha hauko hivyo
Kuna vingi ambavyo vinamtambulisha mwanaume na hata walivyovitaja vinakubalika ila sio katika msingi kama huu waliouleta
Mkuu utashambuliwa sana kwa msimamo wako huu
 
Mkuu Eiyer mimi ni muumini wa hoja,unasema point zangu hazina kitu,fine,naomba unifafanulie point kwa point from 1 to 6 kwamba ni kipi hukubaliani nacho na kwa nini badala ya kutoa a blanket reference kwamba niende kwa Aspirin,huko nshaenda ndo mana nikapingana naye.
 
11. Mwanaume ni mlinzi mkuu wa familia, ikitokea hatari kama ujambazi na kadhalika uwe tayari kufa kwa ajili ya familia.
Hivyo kila wakati usalama wa familia uko mikononi mwako. Huo ndio uanaume. Jasiri,shujaa
12. Mheshimu sana mkeo, mwelewe,umjue na mpende, mwanamke akikasirika ni hatari sana anaweza akaua familia nzima.
13. Kwa mujibu wa biblia, tumeumbwa kwa mfano wa mungu......
14. Ni kweli sisi ndio wanaume, siku zote tunamshukuru mungu kutuumba hivi kuwa wanaume.
15. Ukiwa mwanaume kumbuka kutenda,haki kwa familia na wengine.
16. Kwa namna yoyote ile simama peke yako,usitegemee pesa ya mkeo,pesa yako ni yake na yake ni yake.
17. Wewe ndie kiongozi mkuu wa familia, tuliza kichwa chako kabla hujaamua jambo. Vinginevyo unayumbisha familia.
18. Elewa policy ya familia, inahitaji nini kimaendeleo na wewe utakuwa mstari wa mbele kuitekeleza.
19. Pafanye nyumbani kwako pawe mahali pazuri pa kuishi..''home sweet home'' kwani hakuna kero,uonevu
dharau.kwa ajili hiyo kila mwanafamilia atapenda kuwa home muda wote.
20.TAFUTA PESA HALALI KWA BIDII ZOTE.............KWELI SISI NDIO WANAUME.
21.NI WAGUMU WA KUTOA MACHOZI/KULIA HADHARANI, TUKIZIDIWA TUNAENDA PEMBENI TUNALIAAA TENA SI KWA KUTOA SAUTI BAADAE TUNARUDI.
USO MKAVU.....HAPO UNALIA KIMOYOMOYO MWANAUME.
 
Mkuu,nguvu ya maji ni ulaini wake,ndo maana huwa inapasua miamba.
 
Reactions: Mbu
Mbu wakakti wa kushambuliwa na Babu na watu wake sitakuwepo kukutetea
Hapa kwa kweli ni balaa wakija hao wanaosema kidume ni lazima utoke nje au kidume lalzima ukae baa mpaka usiku
Kwa kweli sitakutetea mkuu

....lol....ndio maana nikasema mwanaume haji na wasaidizi, aje mwenyewe tupimishane ubavu bana...
anyway, haitotokea hii kwani "mbu ameokoka!"...nilitolea mfano tu bana...


...dahhh, mkuu sasa huu ni mdahalo mpya kwakuwa Adam alishakatazwa asile hilo tunda
hata kabla Eve hajaumbwa (mwanzo 2:9)....

je wewe? mpaka sasa usha shawishika "kula tunda" mara ngapi sababu ya mwanamke?
-does that make you less of a man? au ukishakula "tunda" ndio unajiona umekamilika?
 
Sasa ODM,mmoja tu pasua kichwa wawili si ndo balaa!Mi sitaki wawili nataka mmoja tu tena awe hajui kusoma wala kuandika,sitaki awe anajua haya mambo ya globolaizesheni,ni tabu tupu!Yeye ni kupika na kuijali nyumba tu!

umeongea point man.....Baadhi ya wasichana waliosoma siku hizi wanajifanya wapo juu zaidi yetu!
 

...na aliye msafi awe wa mwanzo kunitupia jiwe...lol...!
 
Mbu!To make this clear,faham kwamba tunda linalozungumzwa kwenye Biblia ni tunda kama tunda,sio maana unayotaka kuleta hapa,kufanya makosa kwa hawa Adam na Eve hakukupunguza ubinadamu wao bali kulifafanua mamlaka waliyonayo yanayotofautiana,Eve alianza kula hakujitambua kuwa yuko uchi,alipokula Adam ndipo macho yao yakauona utupu wao!Umeelewa ninachosema hapa?Kwa kukusaidia,jiulize ni kwanini alipokula Eve peke yake asijione mtupu mpaka alipokula Adam?
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…