Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL

Wewe na wenzio, mlioumia na system ya uongozi wa JPM, tunajua mko wengi sana,na kwa ujumla mmebanwa na kushikwa pabaya sana.
Ingawa unaongea kwa kuzidi kujaa sumu, mimi nitaendelea kukueleza ukweli.

Kwanza kauli zako ni ushahidi wazi tukuelewe, ya kwamba wewe unaweza kabisa kuwa wale wafanya matukio, halafu yakatupiwa lawama upande usiohusika.

Lakini pia usijipe" brand" kwamba wewe humu ni think tank.nasema wazi kila member humu ana haki sawa na mwingine yeyote ambaye amekidhi vigezo vya kumridhisha moderator kumuachia kuchangia bila kuvunja masharti na vigezo vya JF. (Ingawa siku zinavyosonga, kejeli na matusi yanazidi kuongezeka kwa baadhi ya wachangiaji).

Nashangaa unajiita mahiri, lakini unalipuka kwa vipande vidogo tu vya ukweli.
Je ungefanikiwa kuukwaa ukubwa wewe na unayemkosoa mna tofauti gani???.

Ungekuwa msomi lazima ungekuwa mstaarabu pia, na usingetoa vitisho vya maisha humu JF.hili ni jukwaa huru

na hupaswi kuligeuza kama jamvi la watu wa mlengo fulani na kujigeuza VIP wa JF ambaye ni untouchable.
Lakini pia ungekuwa smart usingetiririka humu hadi kufikia kutishia member maisha. Hii inaweza kuja kutumika kama• water tight evidence •

Jaribu kuacha mihemuko isiyo ya lazima na ukubali kuambiwa ukweli. Hata kama huupendi.

Nchi hii kabla ya JPM kushika madaraka ya urais, tayari tulikuwa tunaelekea kwenye mgawanyiko mkubwa kitabaka. Na enzi hizo kauli na vitisho kama hivi ulivyovitoa leo humu ndiyo ilikuwa lugha ya mtaani.

Kila aliyewahi kubahatika kuwa aidha na rafiki au ndugu mwenye madaraka,

itokeapo aidha katika hali ya kawaida iwe bar,kijiweni au hata mmepata ajali ya magari yenu kukwaruzana kidogo na hata bila kujali nani mkosefu.
Ilikuwa anapiga simu na dakika mbili kufumba na kufumbua zitatokea zitakako tokea iwe defender au whatever ,na kukusomba bila kutaka kujua nani mkosefu.

Na utasindikizwa na kauli kali kama NITAKUPOTEZA MIMI au NITAKUFICHA! nk.

Sasa hayo matabaka niliyoyatolea mfano hayapo tena. .

Acha JPM atujengee nchi na acha hizi zipakwe rangi. VIVA MAGUFULI.

.
View attachment 992205

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba usubili hizi zipakwe rangi
 

point no.2 umeamua kujazilizia tu
 
Yaani ni hivii hizi zipakwe rangi tu, katavi, mpanda, Shinyanga, Mara, Tabora, kigoma nk pia wapande ndege...hata huko kuna wabunge na wasomi,wafanyabiashara na madaktari,lakini pia hata wagonjwa wenye umuhimu na kuwahishwa kupata matibabu bila kupata adha ya kuwa kwenye magari na kuwaongezea maumivu na hata kusababishia vifo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

brand ID umeweka kichekesho leo
 
Kwa hiyo unashauri zipaki tu

Hapana ushauri wa kiuchumi nikuwa kwa vile tuna ndege za kutosha sasa kwa safari za ndani na pia kwenda nchi za jirani na pia kwavile hizo ndege mbili za serikali hazina matumizi ni bora hizo ndege mbili zikauzwa na pesa itakayopatikana itumike kwenye maendeleo ya nchi! It will be a rational decision.
 
Una uhakika gani kwamba hizo ndege zilizonunuliwa zinatosha wakati bado routes za nje hazijaanza!

Una uhakika gani na bei zitayouzwa kama itatosheleza hayo unayoyapendekeza.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe hana mshauri. MaCCM wenzake wote wanamgwaya

It is a pity that a political party that had men who could stand up against their chairman when he made stupid decisions is the same party that does not have members with the courage to stand up against the stupid decisions that are now made by a novice CHAIRMAN!!

Huko nyuma hiki chama tawala kilikuwa na WANAUME kwenye halmashauri kuu na kamati kuu ambao walikuwa hawana woga wa kumwambia mwalimu kuwa alikuwa amekosea. Marehemu Rajab Diwani, Masudi Mtandika, Mwangoka, Budodi, Kaaya, Dossa Aziz etc. hawa walikuwa wanaume waliodiriki hata kumwambia mwalimu kuwa kama alikuwa amechoka kazi basi angerudisha funguo za ofisi na wao wangemkabidhi mtu mwingine!! Bahati mbaya siku hizi hakuna tena wanaume kwenye halmashsuri na kamati kuu ya chama tawala, wamejaa wachumia matumbu tu; JIWE anajifanyia mambo anayotaka hata kuwapa vyeo watoto wa dada zake na hakuna hata mtu anayethubutu kuhoji uhalali wa teuzi kama hizo!! Ina huzunisha sana.
 
Huyo kichaa anaweza kabisa kuifanya hoteli. Janga kubwa la Taifa huyo.

Inasikitisha sana...

Vitu vya serikali na viheshimiwe jamani... hizo ndege zilikuwepo kwa ajili ya waliyopita na zinatakiwa ziendelee kuwepo kwa ajili ya atakayokuja...

Tusipoangalia tutaanza kupangisha mpaka jumba jeupe...


Cc: mahondaw
 
Una uhakika gani kwamba hizo ndege zilizonunuliwa zinatosha wakati bado routes za nje hazijaanza!

Una uhakika gani na bei zitayouzwa kama itatosheleza hayo unayoyapendekeza.



Sio lazima uanze routes ndio ujue kama ndege ulizonazo zitatumika to full capacity; kuna wataalam wanafanya kazi yao na kujua demand ya seats za kila route. Mpaka sasa hizo safari na routes unazosema compétition ni very fierce mpaka hiyo DREAMLINER imeishia kubeba MBUZI kwenda Dubai. Hizo safari za India na China mpaka leo ni ndoto; kwani hata wakienda wana uhakika gani kuwa watakuwa na passengers na cargo ya kutosha wakati wa return leg!

Kuhusu kuziuza hizo ndege you will be better off kuziuza pale unapopata bei nzuri kuliko kuzifuga bila matumizi!! Locally mpaka sasa zile Bombardier na Airbus zinatosha kabisa na hata kuwa na excess capacity so the only rational decision ni kuuza hizo ndege za serikali kwa mbei nzuri.
 
Maneno meengi point ni ileile.
Hebu tuambieni nini matunda ya mlipowahi toa ushauri kabla ya kuja kubwabwaja short cuts humu.
Hizo nchi mnazosifia kimaendeleo unadhani walifika huko bila kujaribu wao binafsi.
Leo mnang'anga'nia keyboards humu JT.
Wenzenu wanachangamkia fursa za ajira na kuyarusha hayo madege kuja tizoo!

Ndege ni biashara inayofanyika kwa vigezo vya kimataifa. Sio kama daladala au bajaj unanunua leo kesho peleka route ya magomeni no...no.

Lazima ziandaliwe hususan upande wa sales agencies internationally, ndio maana inachukua muda kuanza pamoja na flying routes certificates etc.
Mbona hiyo ya shirima wenu hamkumpa ushirikiano na consultations hadi la fail kwa fast mwewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kuuzwa na kugeuzwa kwa matumizi ya biashara lipi ni jambo jema? Mwacheni Rais atimize ndoto zake Jamani msitafute credit za Bure bure tiu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ati points kubwa
1. Maraisi wengine wamedharauliwa.. How??
2. Haijawahi kutokea duniani.."muzungu hajawahi kufanya hivyo??" So what? Katiba hairuhusu?
3. Wasaidizi wa raisi wamshauri .... nini sasa.. point iko wapi wamshauri??
4. Ningeambiwa.... ??
 
Ni assets ambazo zina depreciate with time, atayekuja anaweza akaikuta juu ya mawe. Pia kuna uzi humu jf watu waliuliza ile ndege iko wapi na inafanya nini maana haitumiki, sasa imepewa matumizi wale wale wanakuja bwabwaja kwa nini inatumiwa.
Asante sana kwa kuongelea depreciation of asset. Yaani zile ndege zikae tu, halafu hatujaongelea gharama za kutunza kitu ambacho kimekaa tu.
 
Ati points kubwa
1. Maraisi wengine wamedharauliwa.. How??
2. Haijawahi kutokea duniani.."muzungu hajawahi kufanya hivyo??" So what? Katiba hairuhusu?
3. Wasaidizi wa raisi wamshauri .... nini sasa.. point iko wapi wamshauri??
4. Ningeambiwa.... ??
Yaani ndege ziendelee tu kukaa bure, marais wawe wanakuja na kuondoka lakini ndege ziwe zinakarabatiwa na kutunzwa halafu hazitumiki.

JPM ni mchumi japo hajasomea uchumi. Wabongo tunamezwa na ufahari usio na tija.
 

KINACHOANDIKWA HAPA NI UPUUZI TU KWA SABABU HUJAELEZA MADHARA NA HASARA YA KUTUMIA HIZO NDEGE.
BINAADAM AMEUMBWA KWA ASILI KUWA NI MLALAMISHI NA ASIYERIDHIKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…