Sirro: Waandishi wa habari acheni kutisha wananchi juu ya mauaji ya Kibiti ili muuze magazeti

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
1,739
2,000
Kama ambavyo vurugu za wakulima na wafugaji zilivyozimwa na hili nalo pia limefika.
Bila shaka vyombo vya habari ndivyo vinakuza sana mambo,mbona wakulima na wafugaji wamepatana na hakuna tena uhasama baina yao wala vurugu tena.
Huko kibiti waache kabisa kuripoti,labda mpaka polisi wenyewe watakapotoa taarifa , amini nawaambia mauaji yatakoma maana promo haitakuwepo tena.
 

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,532
2,000
Anataka watu wasitaarifiwe kile kinachoendelea Kibiti! Hapana watu wanatakiwa wapate taarifa. Hawa waandishi wanatenda wajibu wao wa kuhabarisha wananchi na ukiangalia wako makini sana katika utoaji wa taarifa za Kibiti. Mara nyingi wanajaribu kuweka urari (balance) wa habari. Sikutarajia azungumze namna hiyo, kinachotakiwa angewaomba waandishi waongeze udadisi ili kuweza kuweka bayana chanzo halisi cha hayo mauaji ya Kibiti ili wao wapate urahisi wa kuyakabili.
Akumbuke tangu waanze kutangaza kwamba wananayo mikakati ya siri ndivyo mauaji yanavyo ongezeka. Na kasi ya matukio inaonekana kuongezeka kidogo siku za hivi karibuni. Kamanda Sirro anatakiwa kujitahidi kupambana, ndivyo wenzake walivyoweza kuhimili mikikimikiki ya ukubwa.
 

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
2,000
Kama ambavyo vurugu za wakulima na wafugaji zilivyozimwa na hili nalo pia limefika.
Bila shaka vyombo vya habari ndivyo vinakuza sana mambo,mbona wakulima na wafugaji wamepatana na hakuna tena uhasama baina yao wala vurugu tena.
Huko kibiti waache kabisa kuripoti,labda mpaka polisi wenyewe watakapotoa taarifa , amini nawaambia mauaji yatakoma maana promo haitakuwepo tena.
Ww , jana tu tumezika mkulima kapigwa mkuki na mfugaji, unazungumzia vurugu za wafugaji na wakulima wa nchi ipi zilizoisha!?
Migogoro haitatuliwi kwa kukataza watu kutoizungumzia
 

kilokiki

JF-Expert Member
May 3, 2016
1,366
2,000
Igp nae anasahau kuwa siku hizi hatuna muda na vyombo vya habari?
Siku hizi mitandao ya jamii inanguvu kubwa kuliko vyombo vya habari.
Mimi ninazaidi ya miezi mitatu sijasoma gazeti wa kusikiliza na kuangalia chombo chochote cha habari na najua mambo yote yanayoendelea.
Hata repot ya kesho nitaipata humu
 

SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,652
2,000
Anataka hadi wafe watu wangapi?Zama za leo hata ukizuia magazeti lakini sosho media zitakuumbua,jana imeripotiwa jumla ya idadi ya watu 38 wameshauliwa na hilo saga hataki TUJUE?
 

Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,931
2,000
Huyu naye kakosa kazi. Yanapotokea mauaji ndiyo wanaenda baada ya hapo wanarudi wote dar kumlinda mataputapu.
Kwann wasiweke kambi huko? Mauaji ya kibiti yanatisha kama kula rambi rambi za marehemu.
Wameona magazeti yanaripoti, mijasho imeanza kuwatoka mpaka sehemu za siri. Wangeambiwa kuna raia wanaandamana, utasiku siku hiyo JWTZ inafanya usafi.
Mkaweke kambi huko, tunahitaji vitendo na siyo maneno maneno kama waimba taarabu.
Ndiyo yale yale ya mataputapu ya kushutumu vyombo vya habari. Mkafanyaje kazi, magazeti kazi zao ni kuripoti tu. Mnataka magazeti yasiripoti ili mjinchimbie kwa bashite. Nendeni mkapigane na vidume vyenye silaha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom