comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,939
Dar es Salaam: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa limejipanga kuimarisha utulivu na amani kuelekea Sikukuu ya Uhuru itakayofanyika Desemba 9 mwaka huu na Sikukuu ya Maulid itakayofanyika Desemba 12 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, alisema wananchi wajimwage mitaani na wasiwe na shaka yoyote ya kiusalama pia wajitokeze kwa wingi katika sherehe hizo ili kusherehekea sikukuu kwa utulivu na amani kwani kutakuwa na doria za jeshi la polisi kuzunguka maeneo ya fukwe za bahari, mikusanyiko ya watu na maeneo mengine ya jiji la Dar.
Ametoa rai kwa wazazi wenye watoto wadogo kutokuwaacha watangetange hovyo peke yao mitaani na wasiache nyumba zao bila mwangalizi kwani wahalifu wanaweza kutumia mwanya huo kufanya uharifu huku akikataza disko toto.
Wakati huohuo, Sirro alisema jeshi la polisi kwa kipindi cha Desemba 2 mwaka huu limefanikiwa kukusanya Tsh.451,590,000/= kupitia tozo za makosa mbalimbali ya usalama barabarani na kuingizia serikali mapato ya ndani.
“Jumla ya vyombo vya moto vilivyokamatwa ni 13,496, ambapo pikipiki ni 1,296, daladala zilizokamatwa ni 5,713 na magari binafsi pamoja na malori ni 7,783,” alisema.
Kwa upande mwingine alisema watuhumiwa sugu 103 wamefanikiwa kukamatwa kwa makosa mbalimbali likiwemo la unyang’anyi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba usiku na kuiba, kucheza kamari, wizi wa magari na wizi kutoka maungoni.
Chanzo: TBC