Sirro: Mjimwage mpendavyo sikuu ya Uhuru, Maulid

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

Dar es Salaam: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa limejipanga kuimarisha utulivu na amani kuelekea Sikukuu ya Uhuru itakayofanyika Desemba 9 mwaka huu na Sikukuu ya Maulid itakayofanyika Desemba 12 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, alisema wananchi wajimwage mitaani na wasiwe na shaka yoyote ya kiusalama pia wajitokeze kwa wingi katika sherehe hizo ili kusherehekea sikukuu kwa utulivu na amani kwani kutakuwa na doria za jeshi la polisi kuzunguka maeneo ya fukwe za bahari, mikusanyiko ya watu na maeneo mengine ya jiji la Dar.

Ametoa rai kwa wazazi wenye watoto wadogo kutokuwaacha watangetange hovyo peke yao mitaani na wasiache nyumba zao bila mwangalizi kwani wahalifu wanaweza kutumia mwanya huo kufanya uharifu huku akikataza disko toto.

Wakati huohuo, Sirro alisema jeshi la polisi kwa kipindi cha Desemba 2 mwaka huu limefanikiwa kukusanya Tsh.451,590,000/= kupitia tozo za makosa mbalimbali ya usalama barabarani na kuingizia serikali mapato ya ndani.

“Jumla ya vyombo vya moto vilivyokamatwa ni 13,496, ambapo pikipiki ni 1,296, daladala zilizokamatwa ni 5,713 na magari binafsi pamoja na malori ni 7,783,” alisema.

Kwa upande mwingine alisema watuhumiwa sugu 103 wamefanikiwa kukamatwa kwa makosa mbalimbali likiwemo la unyang’anyi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba usiku na kuiba, kucheza kamari, wizi wa magari na wizi kutoka maungoni.

Chanzo: TBC
 
Siro anafanya kazi yake kitaaluma na busara.

Dah long weekend
 
Je intelejensia yao kwenye hii haionyeshi kuwapo kwa vuruguu?
Au kwa kuwa wale wanaofanya vurugu wapo nje ya nchi?
 
Mods rekebisheni pale kwenye title neno sikuu lisomeke sikukuu za .....
 
bado kuna aja ya kukubaliana na wazo la gogo la shamba kwamba,badala ya kwenda uwanjani nauli zetu tuwatumie watanzania wenzetu waliopatwa na tetemeko Kagera kwani kidogokidogo ujaza kibaba
 
Hiyo siku ya Uhuru wanamaanisha wataimarisha ulinzi uwanjani au!! Maana kama mtaani hakuna mtu ambaye husherehekea kwa kunywa, kula na kuvaa kwa sababu ya siku ya Uhuru
 
Katika Makamanda wa kanda maalumu ya Dsm CP Simon N.Sirro yupo vizuri mno katika operesheni wakati wa kutekeleza majukumu yake.Huyu nahisi anaweza kuongezewa muda baadae
 
bado kuna aja ya kukubaliana na wazo la gogo la shamba kwamba,badala ya kwenda uwanjani nauli zetu tuwatumie watanzania wenzetu waliopatwa na tetemeko Kagera kwani kidogokidogo ujaza kibaba
Ungeanza na Mbowe aliyeenda ulaya kwenda kuchafua taswira ya Tanzania badala ya kuwapa hizo nauli wahanga wa tetemeko kagera
 
Ungeanza na Mbowe aliyeenda ulaya kwenda kuchafua taswira ya Tanzania badala ya kuwapa hizo nauli wahanga wa tetemeko kagera
umefanya la maana kumkumbusha Mbowe na mimi nakubaliana na hoja yako basi mkumbushe na Juma Ponda Mali labda wewe atakusikia
 
Huyu kamanda yupo imara sana,hapendi kuyumbishwa ...............Makonda mwenyewe kamshinda
 
Back
Top Bottom