Siri za yafichuka kuwekwa ndani mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, wananchi wasema ni chuki za kisiasa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa G/Mboto akipokelewa na wananchi wake baada ya Masaa 48 aliyowekwa ndani na Mkuu wa mkoa Dar es Salaam.
Wananchi hao wamelaani kitendo hicho na kukuta chuki za kisiasa ambazo matokeo yake siyo mazuri maana wananchi wanataka maendeleo siyo chuki za kisiasa.

Wamendelea kusema kwenye mtaa huo mwenyekiti wao ni wa UKAWA na mjumbe mojawapo katika serikali hiyo ya mtaa nikutokea CCM kwahiyo kuna kutokuelewana katika ufanyaji kazi zao.

IMG-20161126-WA0015.jpg

IMG-20161126-WA0010.jpg

IMG-20161126-WA0011.jpg
 
Tunaposema mwendokasi ni hatari watu hawaelewi

I am sorry to say this. Anachofanya JPM na hao kina RC Makonda, kina RC Mgambo wa Arusha na viongozi wengine wenye tabia kama hizi ni kuwa wanajaribu KUWANATENGENEZA KINA MWAMWINDI(Rejea kesi ya Mwamwindi)aliyempiga risasi Dr. Kleruu aliyekuwa RC huko Iringa miaka ya 1970s!
Kiongozi unapo jaribu ku-harass watu na wewe kujifanya uko juu ya sheria ni kujitengenezea maadui ndani ya jamii pasi na sababu!
Muda utaongea. I am sorry!!!!
 
Kilichoangaliwa hapo ni haki. Yule hata kujieleza ilikuwa shida
Mimi nimesikia Hays:
Mwenyekiti anapokea ushuru kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya Biashara pembezoni mwa barabara hasa karibu na stand ya gongolamboto, risiti anachapisha yeye mwenyewe na Fedha haziingizwi kwenye mfuko wa Mtaa, pia hukusanya ada za taka, so far watu wasisingizie tofauti za itikadi
 
Mwenyekiti anakula hela mtendaji yuko wapi halimashauli na management yote hawakujua hilo inamaana siku izi ukiwa na shida unamsubili mkuu wa mkoa aje ndio ushitaki siku zote nyuma walivyokuwa na matatizo waliwasilisha wapi je kny maisha yao ya kila siku mwenyekiti wa mtaa ndiye kikwazo tuacheni unafiki kwaiyo baada ya mwenyekiti kukamatwa wasio na ajila wameajiliwa hospital dawa zote zimepatikana Elimu bola wamepata maji safi wamepata Milo mitatu wamepata
 
Mimi nimesikia Hays:
Mwenyekiti anapokea ushuru kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya Biashara pembezoni mwa barabara hasa karibu na stand ya gongolamboto, risiti anachapisha yeye mwenyewe na Fedha haziingizwi kwenye mfuko wa Mtaa, pia hukusanya ada za taka, so far watu wasisingizie tofauti za itikadi
Ndg lazima ujue kitu hiki. Mradi wa kuzoa taka ni mradi wa serikali ya mtaa nawala si mradi wa halmashauri kwa hiyo halmashauri haihusiki kwa namna yoyote ktk uzowaji taka ndio maana unaona rist zinazotumika na za serikali ya mtaa si za halmashauri. Na kama kweli angekua anakula basi huu mradi ungekwisha kufa, mbona unaendelea zaidi ya miezi 9. Kuhusu vikao tulishakaa zaidi us Mara 2 lkn sisi watanzania ni wavivu wa mahudhurio ya vikao.
Huwezi kuamini mtaa mkubwa kama gongolamboto kikao cha mwisho cha mtaa tulikua wananchi wasiozidi 90 wakati taarifa tulikua nayo.
 
Bavicha mna matatizo Mbagala kuna mtu kawekwa ndani,lakini mlikaa kimya ameguswa mtu wenu mnalia.Hakuna wa kumzui Makonda asisikile matatatizo ya wananchi,hatuangalii chama kama ukela hela ni lazima sheria ichukue mkondo wake

Jana nilimuona huyo RC... Khaaaa... ni style gani hiyo ya uongozi?! Unamsimamisha mtu utafikiri wewe ni mwalimu mkuu unaanza kumuweka kiti moto huku ukimchonganisha na kumdhalilisha mbele za watu, kila swali unalouuliza humpi nafasi ya kujibu, akianza tu kuongea unamcheka kwa kejeli huku ukirusha maneno ya uchonganishi na kila aina ya kejeli na dharau... Kwani hakuna mifumo rasmi ya ufuatiliaji? Siasa gani hizi za kuwachonganisha hawa viongozi wa mitaa na wanachi wao?! Kwa kweli huu uongozi ni wa kishamba na una-lack weledi...
 
Alafu, bunge lilifungiwa supposedly ili watu wasiangalie tv wafanye kazi, sasa hii style ya uongozi kwa mkuu wa mkoa ya kupitia tv ni ya wapi? Je haya ndio majukumu ya mkuu wa mkoa? kufanya mikutano ya hadhara? Na je kazi zimeisha sasa kwa hiyo watu wanaruhusiwa kuangalia tv? Je? ni kwanini viongozi na wabunge wa upinzani walikatazwa kufanya mikutano ya aina hii hii (ambayo ipo kikatiba) ya kuongea na wananchi wao ili kuzijua kero zao, lakini huyu RC yeye anafanya hii mikutano with impunity?
 
Mimi nimesikia Hays:
Mwenyekiti anapokea ushuru kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya Biashara pembezoni mwa barabara hasa karibu na stand ya gongolamboto, risiti anachapisha yeye mwenyewe na Fedha haziingizwi kwenye mfuko wa Mtaa, pia hukusanya ada za taka, so far watu wasisingizie tofauti za itikadi
Indeed! Yaani hawa UKAWA hopeless kabisa. yaani badala kusimamia ukweli. Nilikuwa na interest kweli ya kujiunga na upinzani kumbe ni hopless kabisa. Kila kitu kupinga tu. Sasa km anachapisha risiti, that is stealing! Kwa hiyo aachiwe tu!
 
Mleta mada umeongea na wanachi wa huko wangapi hadi umekuja na hitimisho la uzi wako? Mbona na wewe unaonekana una chuki za kisiasa? Hivi vijitu vifungwe tu manake mara nyingi vimekuwa vyanzo vya matatizo badala ya tiba ya matatizo. Hapa tulipofikia kiongozi yeyote wa upinzani hata akikosea namna gani hapaswi kusemwa, halafu tunasema tunataka mabadiliko ya kweli, je ndiyo hayo!? Ila wasiishie kuviweka ndani hivi vya huku chini ilihali yale ya kule juu wanayaogopa.
 
Bavicha mna matatizo Mbagala kuna mtu kawekwa ndani,lakini mlikaa kimya ameguswa mtu wenu mnalia.Hakuna wa kumzui Makonda asisikile matatatizo ya wananchi,hatuangalii chama kama ukela hela ni lazima sheria ichukue mkondo wake
Majibu yapo kwa wananchi waliomchagua na kumpokea baada ya masaa 48. Kama huyaelewi ni kwa sababu wewe na serikali yenu mmejitoa ufahamu.
 
Back
Top Bottom