Siri za Nape nje: Ni zile zinazomhusu Lowassa;Profesa Mwandosya pia atajwa

Status
Not open for further replies.
Jun 9, 2011
92
53


Nani leo ndani ya CCM asiyefahamu azma ya Kikwete na Nape ya kumwandalia njia Professor Mark Mwandosya ya kuwa rais wa 5 wa Tanzania? hata hivyo juhudi za Kikwete na Nape zinaonekana kugonga mwamba huku baadhi ya wana ccm wakimwambia Kikwete na Nape waachane na ngoma ya kitoto hiyo ambayo kwa kawaida haivuki saa sita usiku.

Utamu wa siasa ndani ya CCM unanogeshwa na manguvu ya kimtandao ya Edward Lowassa yanayomshinda nguvu Mwandosya kiasi kwamba amebaki kuomba msaada wa Kikwete na Nape Nauye hata hivyo nao hawawezi kuzima nguvu za Lowassa.

Najaribu kufikiria kwenye mchafukoge huu nani atakayemweza Lowassa? ikiwa huyo Mwandosya mwenyewe ambaye ndiye chaguo la Kikwete na Nape anaonekana kuzidiwa nguvu na mapigo ya Lowassa!

BAADAE:
 
Tunataka rasi kijna ,
Mwenye ubongo unaochemka na sio hawa mnaowataja taja wote wamechoka ndio hao wanao lala bungeni.

Wakati sasa umefika kuachana na hawa wanoelekea kustaafu au wamestafu utumishi wa umma wakamua kuingia kwenye siasa.
 
Hivi huyu Kipanga mlakuku na Kiwalanikwa gude ni mtu na mdogo wake? Mmoja kajiunga tarehe 8 June na mwenzake tarehe 9 Juni. Lakini malengo ya mada zao ni kuonyesha nguvu alizo nazo Lowassa ndani ya CCM.
 
Ni kama unapanga timu yenye madefender wote sasa sijui nani atashambulia. Kifo na kiama chenu ni October 2015. Mengine haya porojo, unafiki na uzandiki wa Njaa kutumwa kusafisha wanasiasa waliokwishakata tamaa.
 
Kikwete anamwandaa Asha Rose Migiro. Kikwete anajua kwamba CCM haipendwi na kete iliyobaki ni kumuibua mwanamke ili wajenge hoja kuwa huu ni muda wa mwanamke. Hoja hii ilifanikiwa kumpindua Sitta kwenye uspika. Vijana wa Nape msitudanganye.
My take; CCM itaangukia pua kama kanu bila kujali wanaleta mwanamke au mwanaume. Suala hapa ni maslahi ya nchi. Siyo jinsia, dini, kabila, rangi, urefu wa mtu, nk.
 

JF kuna vituko..!!! mara Asikofu kafunuliwa kuwa Lowasa raisi 2015, mara kikwete anampa shavu Mwandosya...mara mingiro... daaahhh, kesho mtasikia mja ndo raisi 2015....
 
Lakini Mwandosya anaumwa aliongea kama wiki mbili zilizopita akiwa Hosp. India. Je hali yake inaendeleaje wakuu.
 
Hiyo Post namba 9 - Hilo behewa lilisanifiwa vibaya, au jamaa ni warefu mno, au labda ni mambo ya Photoshop? mbona vichwa vinashindilia dari?
 
duh - mtu wa kusimama uraisi kwa CCM akakubalika simwoni - may be Magufuli anaweza walau kupata 41%. wadau wa siasa za bongo nisahihisheni kama nimekosea.
 
Hivi huyu Kipanga mlakuku na Kiwalanikwa gude ni mtu na mdogo wake? Mmoja kajiunga tarehe 8 June na mwenzake tarehe 9 Juni. Lakini malengo ya mada zao ni kuonyesha nguvu alizo nazo Lowassa ndani ya CCM.
pumba€ usimbague mtu kwa cku alyojiunga.. Jaji anacho'post
 
Prof Mark Mwandosya ni mgonjwa hafai kuwa raisi....yuko India kwa operation kubwa.

Umeniwahi Mkuu nilitaka kuandika hivyo hivyo . Nasikia chaguo la Kikwete ni yule Asha Migiro na Hussein Mwinyi. Kwa maoni yangu afadhali Asha Migiro ili sijui kama ana support kubwa ndani ya chama cha magamba na pia Kikwete hana ushawishi mkubwa wa kuweza kumpigia debe. Yule Hussein Mwinyi hastahili kabisa hasa baada ya kuvurunda katika sakata la mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto. Kwa hiyo kama Lowassa, RA na Chenge hawatemwa nadhani hawa na kundi lao jipya la mtandao ndio wanaweza kutoa mgombea toka chama cha magamba.
 


Hatuwezi changua Mgonjwa aisee! RIP Levy Mwanawasa. Kama Lt Col Kikwete ana machaguo lake na sisi watanzania Mil 40 tuna chaguo letu
 
aise hivi Mwandosya anasumbuliwa na ugonjwa gani hasa?something chronic and serious or what?
 
kagonjwa aka hatutaki Rais kimeo hatuna ela za matibabu kila Dakika, tungemweka ZITO lakini kutoa kwakwe kwatutia shaka.
 
Hatuwezi changua Mgonjwa aisee! RIP Levy Mwanawasa. Kama Lt Col Kikwete ana machaguo lake na sisi watanzania Mil 40 tuna chaguo letu

Kumbuka kuna kuchakachua pia kama mtandao/mafisadi walivyochakachua 2005 na hatimaye Kikwete kuibuka Kidedea. Hivyo 2015 pia wanaweza kuchakachua toka mgombea wa magamba na pia kuchakachua uchaguzi mkuu kama ilivyotokea 2010 na Watanzania zaidi ya milioni 40 kuachwa solemba.
 
Hivi huyu Kipanga mlakuku na Kiwalanikwa gude ni mtu na mdogo wake? Mmoja kajiunga tarehe 8 June na mwenzake tarehe 9 Juni. Lakini malengo ya mada zao ni kuonyesha nguvu alizo nazo Lowassa ndani ya CCM.

Wewe kweli ni jasusi. Heshima kwako mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…