Siri za mikataba ya mastaa Yanga

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
UONGOZI wa klabu ya Yanga umefichua sababu za kuwasajili wachezaji kwa mikataba mifupi ni kutokana na mifumo ya soka hapa nchini ilivyo.

Klabu nyingi za Tanzania zimekuwa na utaratibu wa kuwapa wachezaji wake mikataba mifupi ikiwemo miezi sita, mwaka mmoja hadi miwili na Yanga wameweka wazi sababu ya wao kufanya hivyo ingawa hawakutaja idadi ya wachezaji wenye mikataba ya namna hiyo.
Mwenyekiti kamati ya usajili ya Yanga, Hersi Said alisema moja ya sababu kubwa ni aina ya skauti inayofanyika kuwapata wachezaji hao na asilimia kubwa wanasajiliwa bila kuwafahamu kiundani tangu akiwa chipukizi zaidi ya kuwaona wiki kadhaa tu.

“Ni ngumu sana kumfanyia skauti mchezaji hapa nchini kuanzia alipoanza mpaka ukubwani kutokana na aina ya mifumo ya upatikanaji wao ilivyokuwa, sasa kama shida iko hapo unawezaje kumsajili mchezaji kwa mkataba wa muda mrefu halafu akiharibu gharama tu za kuvunja nae mkataba sio mchezo, itakulazimu kumtumia hivyo hivyo hata kama kiwango kimeshuka,” alisema Hersi.

Hersi alisema hiyo ndiyo sababu inayowafanya kutoa mikataba mifupi tofauti kwa ajili ya maslahi ya timu na mchezaji husika.

“Halafu hizi timu hazina pesa ya kufanya sajili ndefu, mchezaji ukimfuatilia toka chini na kujua mwenendo wake unaweza kumpa mkataba mrefu lakini ni elimu ambayo inatakiwa kutolewa kwa watu maana wengine wanalalamika tu huyu mchezaji mzuri mkataba kapewa mfupi kwa sababu hawajui,” alisema Hersi.

Mwanaspoti linafahamu wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu ni Bakary Mwamnyeto, Farid Mussa, Zawadi Mauya, Yassin Mustafa, Kibwana Shomari, Deus Kaseke, Yacouba Sogne na Saido Ntibazonkiza.

Kuhusu nyota wao ambao mikataba inaelekea ukingoni alisema, hakuna mchezaji mzuri ambaye watakubali kumuachia aondoke bali watawaongeza mikataba kutokana na mahitaji ya kocha wao Nasreddine Nabi.
 
Janja janja tu kwani mchezaji akisajiliwa baada ya kufanyiwa scouting kuanzia utotoni kiwango hakishuki?
 
Uo ndio ukweli, klabu zisipo kua makin zitajikuta zinalipia gharama za kuvumja mikataba marakwamara.
 
haya akumuongezee mkataba yule ng'ombe mwenye six pack
 
Badala ya kununua wakala anakupa mchezaji kwa makubaliano maalumu, wewe unasema kwa wasiojuwa kuwa umenunua sasa wakala akitaka kuchukuwa mchezaji wake wewe unaanza andaa mazingira ya kuweka uongo wako uwe ukweli.
 
Yuko sahihi ila mashabiki wa gabacholi fc watabisha
Eti yuko sahihi utopolo bhana.Mchezaji kusajiliwa baada ya kufanyiwa scouting ya kuanzia utotoni hauna tija kwa asilimia 100.

Semeni tu hamna fedha kwa hiyo mnasajili kwa kubahatisha bahatisha na ndio maana ndani ya msimu mmoja mliwahi kusajili zaidi ya wachezaji 20.
 
Bado wanajikongoja hela za kuendesha biashra yake zinasuasua bado sana kufikia level za Simba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom