Siri za kushinda ubunge Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri za kushinda ubunge Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mbunge wa CCM, Nov 5, 2010.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Kuwa karibu na wanachi hadi wakuzoee na kukuamini.
  2. Ujichanganye na wananchi hadi wakuone ni mwenzao.
  3. Utumie kwa uangalifu ushawishi wako na elimu yako hadi ilete mwanga mawazoni mwa wanachi na katika matarajio yao mbalimbali ya maendeleo
  4. Jitofautishe na wowote wanaoaminika kuwa wana potentials za kugombea ili wewe uonekane unang'ara zaidi
  5. Weka ratiba yako wazi na shughuli zako zote uzifanyazo ziwe wazi
  6. Tenga muda wa kukutana na kubadilishana mawazo na makundi yote katika jamii kama wazee, vijana, akina mama nk
  7. Onyesha upeo wako halisi juu ya mapinduzi ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi kwa ujumla; itakupa uzito zaidi kama upeo huo ni sahihi kwa mazingira tuliyonayo
  8. Zifahamu vizuri sera za wapinzani wako na uzifafanue vizuri bila husuda kwa wapiga kura wako kabla hujaonyesha wapi zilipo na mapungufu.
  9. Jivunie bila haya chama chako na historia yake ya kuongoza mageuzi nchini mwetu. Hapa unapaswa kujivunia hata kama chama chako si maarufu
  10. Jenga ushirikiano na wanasiasa wengine wenye ushawishi na wananchi wajue hilo hata kama wako nje ya jimbo lako

  Kwa leo niishie hapa, siku nyingine nitawaletea siri zaidi za kuibuka na ushindi katika chaguzi za kidemokrasia

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
   
 2. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tunashukuru kutupa darasa mheshimiwa
   
 3. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  11.Uwe na Kamati za ufundi na consultants Witch Doktas from Nigeria,Gambia etc
  12.Kikosi kazi madhubuti cha Kuchakachua bila Aibu
  13.Usione Tabu kukanyaga watu Vichwa ili uupate Uongozi-By any Means Necessary
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mhh...... siamini hayo usemayo ndugu.............

  lakini mheshimiwa mbunge katusaidia sana wengine japo mnambeza.... hili ni darasa tosha kabisa, nimeona watu wakikosolewa hapa mara nyingi juu ya starategy zao za kugombea, wengine wanaonekana majimboni wakati wa uchaguzi tu, ukiisha wanarudi mjini wawe washndi ama vinginevyo ....... sasa hapa kuna shulle ya bure kabisa, tena toka kwa mheshimiwa realy.......

  hongera mheshimiwa..... hope tutagongana mjengoni siku moja............ inshallah............
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu rushwa kwa kisingizio cha misaada wakati wanabaki tegemezi wa ahadi hewa?
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Darasa lako ni powa lakini hilo nililo highlight haliwezekani. Kimeshakuwa Kigumu na kinaelekea kaburini. Heshima yake itarudi mkipata viongozi safi. Kikwete na Makamba si wasafi na hawawezi kukivusha chama mbali na kwamba wataplelekea nchi katika machafuko.
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  uchakakachuaji una nafasi gani
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kwa nini unai-support ccm?
   
 9. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  huwezi kuiondoa CCM madarakani.. chakufanya jiungeni CCM then mfanye harakati za kubadili sera za CCM ziwe na manufaa kwa wananchi
   
 10. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni suala la kujipanga tu, kama iliingia basi inaweza kutoka pia
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hakuna kitu kisichowezekana chini ya jua! Hata Roma ilidhani isingeanguka! Hitler alisema watatawala miaka 1,000! Sembuse ccm?
   
 12. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sure bro
   
 13. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  toa rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni
  nunua shahada za vijana na akina mama unofikiri ni wapinzania ili wasipige kura
  waonge wasimamizi wa uchaguzi kama mhe mahanga ili utangazwe hata kama haujashinda
   
 14. A

  Alaigwanani Member

  #14
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma Namba 1 na 2 tu
  1. Kuwa karibu na wanachi hadi wakuzoee na kukuamini.
  2. Ujichanganye na wananchi hadi wakuone ni mwenzao.

  Namba moja inaonyesha sikuzote haupo karibu na watu ila unajifanyisha kumbe kunakitu unataka(ubunge), kama kuwalia timing hivi

  Namba 2 kumbe kama sio ubunge usingejichanganya

  Hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
Loading...