Siri yafichuka: Sababu ya wabunge kucheza "kitorondo" bungeni

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Baada ya "Rasimu ya Sitta" kupitishwa na Bunge maalumu baadhi ya wabunge walilipuka kwa furaha na wengine wakakata mauno hadharani, huku mbunge wa Njombe kaskazini Deo Sanga akicheza "Kitorondo" na kukata mauno mbele ya halaiki.

Pia kuna wabunge wengine walikua wakicheza kwa kufuatisha milio ya miziki iliyokua ikirindima kupitia simu zao za mkononi.

Watu wengi walihamaki kitendo cha wabunge kufurahia Rasimu hiyo hadi kufikia hatua ya kujitoa akili.

Hii hapa siri ya furaha ya Wabunge hao..

RASIMU YA WARIOBA ILIPENDEKEZA:

1. Mbunge akigombea vipindi vitatu basi, awaachie wengine.

2. Mbunge akivurunda ktk utendaji wake, wananchi wana uwezo wa kumuondoa na kuchangua mwingine.

3. Hakuna mbunge kuwa Waziri, Mkuu wa mkoa, m/kiti wa bodi ya shirika etc. (kwanini vyeo vyote mjilundikie nyie?).

4. Elimu ya mbunge iwe angalau stashahada (diploma) na kuendelea.

RASIMU YA SITTA (ILIYOPITISHWA) IMEPENDEKEZA HIVI:

1. Ukomo wa Ubunge usiwe vipindi vitatu.. Hata wazee waliokaa bungeni miaka 50 kama Kingunge, waendelee tu kugombea. Vijana wanaotaka kuwa viongozi labda wakajaribu kwny SACCOSS sio UBUNGE.

2. Mbunge akivurunda wananchi hawawezi kumfanya kitu chochote hadi miaka mitano iishe na mbunge apewe pensheni yake (Mil.160).

3. Ruksa Mbunge kuwa waziri, Mkuu wa mkoa, DC, Mwenyekiti wa shirika, na vyeo vingine kadri anavyoweza kujilundikia. Wanaosema mbunge asiwe na vyeo viwili au zaidi, wana "wivu wa kike" (according to Pius Msekwa).

4. Elimu ya Mbunge iwe kama ya Deo Sanga (mbunge Njombe Kask), yaani kujua kusoma na kuandika tu inatosha. Rasimu ya Sitta inasema si lazima mbunge awe na degree, diploma, au cheti.

Si lazima mbunge awe na elimu ya sekondari. Si lazima Mbunge awe amemaliza elimu ya msingi. Hata kama alisoma akaishia darasa la 3 lakini anajua kusoma na kuandika RUKSA KUGOMBEA UBUNGE.

Sasa je katika mazingira haya wabunge wataacha kukata mauno na kucheza "kitorondo" kwa Rasimu hii kupita??

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.

Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!
 
Attachments

  • 1412498027481.jpg
    1412498027481.jpg
    34.1 KB · Views: 3,520
Nakubaliana na katiba ya Sitta.
Ni kweli ila huna hoja bali unajua utawala mbovu ukibaki madarakani utaendelea kula vizuri. Na unajua kabisa mnawaingiza mkenge wananchi kama wakulima, wafugaji, wasanii nk ili waipitishe katiba ya mabavu na mtawapanga polisi walazimishe ipite. Hizo haki zao sasa, wakulima, wafugaji watachora chini, kwani wakulima watafanya nini wakati viongozi wao watakuwa wamenunua madaraka kwa rushwa na hawana uwezo wa kuwatoa.
 
Hata. MSALANI amefurahia kwa maana yeye hajui kusoma wala kuandika!!
_ila tangia lini mtu akajitungia sheria?
_ingefaa waliotunga katiba wasiruhusiwe kupewa uongozi hadi miaka 10 iishe
 
Last edited by a moderator:
Hata. MSALANI amefurahia kwa maana yeye hajui kusoma wala kuandika!!
_ila tangia lini mtu akajitungia sheria?
_ingefaa waliotunga katiba wasiruhusiwe kupewa uongozi hadi miaka 10 iishe
ni kweli mkuu kuwapa maharamia wa ccm watutengenezea katiba ya wananchi tulikosea sana lakini bado hii rasimu ikija kwetu wanancha tutaipigia kura ya HAPANA hatuwezi kukubali huu upuuzi wa rasimu ya ccm
 
Ni ndoto kutegemea kupata katiba bora chini ya utawala wa ccm. Kenya waliweza baada ya kuondoa chama tawala
 
Hivi huyo mzee kumbe ni mahiri sana eeee ! Kanga moko kazi mnayo !
 
Mantiki iko simple acha wananchi wenyewe...kupitia sanduku la kura waamue, wanaweza wakuamua wabunge wakimaliza miaka 5 wasirudi... lakini ni kupitia kura sio kulazimisha au kufanya udikteta!
 
Ni ndoto kutegemea kupata katiba bora chini ya utawala wa ccm. Kenya waliweza baada ya kuondoa chama tawala

Ccm wa mmefikia hatua wamejihakikishia uwezo wa kufanya chochote kwa maslahi yao na kwa namna yoyote ile na hakuna wa kuwafanya kitu. Kwenye uchaguzi wanaiba kura mchana kweupe na hawafanywi kitu. Wanaingia mikataba ya kifisadi ya kuihujumu nchi haqafanywi chochote. Wanaua raia kila uchao bado watz wanachekelea. Juzi wameendelea kuonesha jeuri yao kwa kupiga sn waandishi wa habari lkn mpaka leo waandishi karibia wote wanaipamba ccm na katiba yao haramu. Ndipo tulipofika. Prof J hakukosea kwenye wimbo wake. Watz wanakibwagizo cha NDIO MZEE
 
Baada ya "Rasimu ya Sitta" kupitishwa na Bunge maalumu baadhi ya wabunge walilipuka kwa furaha na wengine wakakata mauno hadharani, huku mbunge wa Njombe kaskazini Deo Sanga akicheza "Kitorondo" na kukata mauno mbele ya halaiki.

Pia kuna wabunge wengine walikua wakicheza kwa kufuatisha milio ya miziki iliyokua ikirindima kupitia simu zao za mkononi.

Watu wengi walihamaki kitendo cha wabunge kufurahia Rasimu hiyo hadi kufikia hatua ya kujitoa akili.

Hii hapa siri ya furaha ya Wabunge hao..

RASIMU YA WARIOBA ILIPENDEKEZA:

1. Mbunge akigombea vipindi vitatu basi, awaachie wengine.

2. Mbunge akivurunda ktk utendaji wake, wananchi wana uwezo wa kumuondoa na kuchangua mwingine.

3. Hakuna mbunge kuwa Waziri, Mkuu wa mkoa, m/kiti wa bodi ya shirika etc. (kwanini vyeo vyote mjilundikie nyie?).

4. Elimu ya mbunge iwe angalau stashahada (diploma) na kuendelea.

RASIMU YA SITTA (ILIYOPITISHWA) IMEPENDEKEZA HIVI:

1. Ukomo wa Ubunge usiwe vipindi vitatu.. Hata wazee waliokaa bungeni miaka 50 kama Kingunge, waendelee tu kugombea. Vijana wanaotaka kuwa viongozi labda wakajaribu kwny SACCOSS sio UBUNGE.

2. Mbunge akivurunda wananchi hawawezi kumfanya kitu chochote hadi miaka mitano iishe na mbunge apewe pensheni yake (Mil.160).

3. Ruksa Mbunge kuwa waziri, Mkuu wa mkoa, DC, Mwenyekiti wa shirika, na vyeo vingine kadri anavyoweza kujilundikia. Wanaosema mbunge asiwe na vyeo viwili au zaidi, wana "wivu wa kike" (according to Pius Msekwa).

4. Elimu ya Mbunge iwe kama ya Deo Sanga (mbunge Njombe Kask), yaani kujua kusoma na kuandika tu inatosha. Rasimu ya Sitta inasema si lazima mbunge awe na degree, diploma, au cheti.

Si lazima mbunge awe na elimu ya sekondari. Si lazima Mbunge awe amemaliza elimu ya msingi. Hata kama alisoma akaishia darasa la 3 lakini anajua kusoma na kuandika RUKSA KUGOMBEA UBUNGE.

Sasa je katika mazingira haya wabunge wataacha kukata mauno na kucheza "kitorondo" kwa Rasimu hii kupita??

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.

Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!

Wewe hiyo ndio unaiita ni siri.kepengelre hicho kilichopitishwa na warioba ni mapendekezo ya watu wavivu kufikiri.kwa nini umuweeembuge ukomo?
 
Tunisia vuguvugu lilianzia kwenye mitandao na kumalizikia kwenye maandamano,kama kweli watu wameona katiba ni chukizo kwao basi
hamasa zitaanzia humu
 
Mkuu uyuu Deo Sanga kuna siku alikuwa amealikwa kwenye ufunguzi wa shule"English medium",wakati wa kuwasllisha matatizo ya shule msoma risala akaomba kamusi yaani dictionary ziongezwe maktaba.Sasa mkuu Deo wakati anajibu risala akauliza kwani izo dictionary zinatakiwa tripu ngapi.Hawa ndiyo walikuwa wanajadili rasimu iliyoandaliwa na wasomi!!!!
 
ni kweli mkuu kuwapa maharamia wa ccm watutengenezea katiba ya wananchi tulikosea sana lakini bado hii rasimu ikija kwetu wanancha tutaipigia kura ya HAPANA hatuwezi kukubali huu upuuzi wa rasimu ya ccm

Hatuwezi!! Ikiwa tumeshindwa kudhibiti kura 500 ni vipi tutamudu ktk vijiji maelfu?CCM itaendelea kushinda na kufanya itakavyo mpaka hapo shule za kata zitakapoyoa div 1 za kutosha.Tumezidiwa tukubali tu.
 
Wewe unajua kwa nini CCM hufurahia zaidi watu wajinga na wanafiki kuliko walioelemika na waadilifu? Mjinga na mnafiki hata siku moja hawezi kuhoji wala kutafakari. Siku zote kazi yao huwa ni kusifu na kuitikia chochote alichokitamka na anachotaka aliyempa ulaji. Hawa huwa wanajua kabisa kuwa kwa uwezo wao hawawezi kufika kokote. Lazima wamtumikie aliyewapa ulaji bila stahili. CCM inawapenda sana watu wa namna hiyo na ndiyo waliojaa CCM. Hata b7 wote hakuna mwenye kazi yoyote ya kumpa kipato zaidi ya ofisi ya Lumumba. Hawa kwao CCM ni zaidi ya chama.cha siasa. Kwao CCM ndiyo chakula, matibabu, ada za watoto na matibabu ya familia zao.

Back
Top Bottom