Siri yafichuka! CCM mwaka 2020 jiandaeni kupambana na huyu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Taarifa za ' Kiudukuzi ' kabisa na ambazo hadi kupelekea Mwandishi wa huu ' uzi ' kuzipata ilibidi afanye ' Kazi ' ya ' ziada ' na ambayo bila ya ' ulinzi ' na ' kudra ' zake Mwenyezi Mungu hivi sasa yangekuwa mengine ni kwamba aliyekuwa ' Mtia nia ' mmoja ndani ya Chama Tawala cha CCM na ambaye hata katika 10 ' bora ' kisha katika ' 7 ' bora alikuwepo amepanga ' mkakati ' mkali sana wa kujiunga rasmi na Upinzani ili kuweza ' kugombea ' Urais kwa kushindana na Rais wa sasa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mwaka 2020.

Habari za ' udukuzi ' na zilizotukuka kabisa zinazidi kusema kuwa ' Kada ' huyo wa CCM ambaye kwa sasa hafichi tena ' unafiki ' wake ndani ya Chama Tawala cha CCM anafanya mazungumzo ya ' Siri ' kabisa na Viongozi wa Vyama viwili ambacho kimoja kimeshajizolea ' umaarufu ' japo hadi sasa kimeshia tu kuja na ' matamko ' ya hapa na pale na yasiyotekelezeka huku Chama kingine kikiwa ni kidogo lakini ambacho kiliweza ' kuwashtua ' Watanzania mwaka jana 2015 kutokana na ' Sera ' zake zenye ' maono ' hasa ukizingatia kuwa kina ' zawadi ' ya kuwa na Mwanasiasa ' Kijana ' ili aweze kujiunga navyo na aweze kupambana na Rais Dkt Magufuli mwaka 2020 kwani anasema kuwa ana uhakika wa ' kushinda ' kwa jinsi alivyojipanga.

Taarifa zaidi za ' Kidukuzi ' zimeenda mbele na kusema kuwa ' mkakati ' wake wa kwanza ni mwaka 2018 kujiunga ' rasmi ' na moja ya hivyo Vyama ' tajwa ' kimafumbo hapo juu ili aanze kutambulishwa, kukijua hicho Chama vizuri kisha aanze kuzungushwa nchi nzima katika moja ya ' Kampeni ' ya Chama kimoja ambayo wanapanga kuifanya mwaka huo wa 2018 ili kujijenga na kujipanga kwa ' ushindani ' katika ' Uchaguzi ' Mkuu mwaka 2020 huku akiwa na ' jeuri ' ya kuungwa mkono na nchi kubwa tatu duniani za Ujerumani, Canada na Uingereza.

CCM najua fika kuwa leo mnaanza ' Vikao ' vyenu vidogo chini ya Mwenyekiti wenu wa ' Taifa ' hivyo jitahidini na hili mliangalie kwa umakini wenu mkubwa kwani huyo ' Nyoka ' mwenye ' Sumu ' kali bado mpo nae humo humo na sasa amekaa ' kimya ' tu lakini akikusanya ' Sumu ' ambayo kama hamtaiwahi kuimaliza mapema kutokana na ' uzoefu ' wake mkubwa na kukijua Chama vilivyo huku akiwa na 'mbinu ' zote za ' Kidiplomasia ', ' Propaganda ' na hadi za ' Usalama ' mwaka 2020 mnaweza kupata wakati ' mgumu ' pengine hata kuliko wa mwaka jana ( 2015 ) kwani katika hivyo Vyama viwili ambavyo anajipanga kujiunga na kimoja wapo kuna Watu wawili ambao wana ' ushawishi ' mkubwa sana katika ' Jamii ' yetu na ambao pia wanajua kupanga ' mikakati ' vizuri mno kitu amacho kinaweza kumrahisishia huyu ' Kada Mnafiki ' wa CCM kuweza ' kuchafua ' kabisa hali ya hewa.

Baada ya ' Kazi ' ngumu ya ' Kudukua ' naomba niishie hapa tafadhali na nisali huku nikimshukuru Mwenyezi Mungu kwani naamini bila kunipa ' ujasiri ' na kuniongoza kwa ' nguvu ' zake nisingeweza kutokana na ' unyeti ' wake.

Kila la kheri.
 
Hata Kama Benard Membe atahamia UKAWA au ACT hata kama akishinda, hatatangazwa kuwa Rais, Unless, Polisi, Tume ya Uchaguzi, na Watanzania wote wajitambue.

Siasa si Uadui, Membe anaweza kukaa Meza moja leo na Lowassa, Hii ndiyo siasa.

Sasa UKAWA Mwaka 2020 watashinda tena kwa kishindo kikubwa, lakini hawatatangazwa na TUME ya Uchaguzi, hapo ndipo wanatakiwa waanzie kupaweka sawa kwanza kabla ya yote, ni kwa namna gani Watalinda Ushindi wao na hadi kutangazwa?
 
Ndoto za mchana, 2020 jpm ataendelea kushika msikani

Mkuu nalijua hilo na wala halina ' ubishi ' kuwa Rais wetu Kipenzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atashinda lakini amini usiamini ' mikakati ' ya huyu ' Kada Mnafiki ' wa CCM ikikaa sawa nakuhakikishia Mwenyekiti wetu anaweza pengine kushinda kwa hata tofauti tu ya kura 2 au 3 na hata akishinda pia lazima atakuwa ' hoi '. Mkuu huyu ' Jamaa ' yuko vizuri na bahati nzuri ni kwamba michezo yote ya ' figisu figisu ' kwake ndiyo Headquarters na hata Wana CCM wanaomjua watakubaliana nami juu ya hili. Achunguzwe kwa ' uangalifu ' mkubwa na ikiwezekana apewe tu mkono wa kwaheri ndani ya Chama Tawala mapema hii ili asije akaachwa halafu akazidi kukusanya ' Sumu ' zake nyingi kisha akienda huko aanze kuzitumia hizo hizo ' Sumu ' kuwadhuru.
 
Alifika saba bora...
Ni Mama au Baba..
Uzoefu diplomasia..
Germany,Uk,France.
Wafikirie hawa:Asha Rose..Amina...Membe..January.
Nimesema tu...lakini muhimu ni Amani na Upendo na kumuomba Mwenyezimungu wa kweli atuongoze na siyo Mungu mtu.
 
Mkuu pole sana kwa kazi yako ya udukuzi ..ila ingependeza ukaweka majina

Mkuu ' uandishi ' wangu 100% ni wa ' Kufumba ' hivyo ' jitahidi ' sana kunielewa na usitegemee nikamtaja hapa ila kama ' Ubongo ' wako uko ' active ' nina uhakika hata katika ' maelezo ' yangu tu nimeshamtaja. Kazi kwako!
 
Alifika saba bora...
Ni Mama au Baba..
Uzoefu diplomasia..
Germany,Uk,France.
Wafikirie hawa:Asha Rose..Amina...Membe..January.
Nimesema tu...lakini muhimu ni Amani na Upendo na kumuomba Mwenyezimungu wa kweli atuongoze na siyo Mungu mtu.
Kama ni hao basi mwenye nguvu na mikakati hapo ni January, wengine hamna kitu. Membe pumzi ishakata.
 
Back
Top Bottom